Majengo ya Machinga Complex sehemu za Ilala jijini Dar es salaam kama linavyoonekana kutoka hewani. Majengo hayo matatu yalijengwa mahususi kwa ajili ya Machinga wanaofanya biashara mitaani lakini hadi sasa mwitikio wa kuhamia humo umekuwa na kwikwi kwa sababu wanazozijua wenyewe. Hii yote ni ya kuendeleza utamaduni mpya wa kupinga kila jambo na kufanya mambo kinyume cha sheria japo huduma zinatolewa.
Home
Unlabelled
machinga complex toka hewani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ReplyDeleteHabari zisizoaminika zinasema kwamba kuna utata kwenye kugawa.
Wanachukua "ambao sio wamachinga"
Labda machinga wanahisi kuwa wakiwa jengoni watashindwa kuwafikia wateja "pale walipo" yaani njiani. Si rahisi kwa mteja kwenda jengoni kununua mali za machinga badala ya zile zilizopo kwenye maduka ya kawaida. Pia kuna Issue ya kodi am,bayo labda machinga wanaweza ikwepa barabarani lakini wanaogopa wataikwaa wakiwa jengoni. Halafu competition. Ukiwa machinga, ukiona competition kali hapa unakimbilia kule. Ukiwa jengoni hiyo ni muhali.
ReplyDeleteMi nalia na huo uwanja wa TFF a.k.a Kumbukumbu ya Karume, kwa nini TFF wasiingia patnership na NSSF/PPF n.k wakajenga kauwanja cha angalau watu 15,000 ikiwa mojawapo wa mradi wa kuiingizia mapato TFF?????
ReplyDeleteAzam FC kupitia kampuni yao mama AZAM wameweza kujenga kauwanja huko Chamazi, nje kidogo ya jiji la DSM.
TFF vyanzo vya mapato mmojawapo ni hilo wazo la Uwanja wa Karume ambao utakuwa katikati ya Jiji. Shughuli za mechi, matamasha ya muziki, injili n.k kwa kweli TFF mngelikuwa mpo mbali kifedha.
Nasubiri kauli ya TFF maana TFF hutumia sana globu hii ya jamii kwa taarifa kwa ummma. Sasa nasubiri kwa hamu kuhusu project hii ya uwanja wa kisasa wa Kumbukumbu ya Karume.
Mdau
Ilala.
Utamaduni wa CHADEMA umewaingia wananchi.. Kama Mzee Slaa akichukua muda wake kuwahimiza wamachinga kuhamia humo basi nitamuona ni mzee wa burasa na 2015 atapata kura yangu.
ReplyDeleteHuduma zinaweza kutolewa lakini zikawa na kasoro, na binadamu siyo kondoo kufuata tu yote wanayopangiwa. NO. muuundo wote wa machinga complex haukukidhi mbinu za kibiashara hizi ndogo ndogo, huwezi ukampandisha mteja anayetafuta kitambaa cha kufutia jasho ,apande ghorofa ya 3 au kibegi cha mtoto wake cha kuendea shule.Ni tabia yetu wanadamu kupenda urahisi fulani katika maisha . kwa mtizamo wangu, hii flea market ( machinga complex) ilitakiwa iwe kwenye godauni kuuubwa na very simple made na siyo migarama kama hiyo iliyotumika hapo, sasa hilo godauni linakuwa na meza meza tu na peupe bila chumba chumba tena ndani humo NO, ukiingia humo ,macho yako yanaona mwanzo hadi ubungo. Na humo humo panakuwa na sehemu ya migahawa na vinywaji, yaani unafanya shopping kwenye ukumbi wa eka 3 na unashikwa na njaa unakula humo humo,pasafiii. Ndo maana ya flea market. siyo hayo magorofa mliyojenga . Bora yauzwe na yageuzwe kuwa apartment buildings, katakata vyumba humo watu waishi.Otherwise kwa biashara ya Machinga ?? NO CAN DO. haya nimaoni yangu, naomba mniunge mkono Zebedayo msema kweli
ReplyDeleteMimi shida yangu ni huo uwanja wa karume. Ulivyojengwa mbona haukufuata usawa wa kiwanja chake? Ni lini wabongo mtajua kuipendezesha miji yenu?
ReplyDeleteAhhh umebugi Ankali!!!
ReplyDeletePicha ya juu kabisa angani pekee Michuzi, kwa nini usingemwambia Rubani ashushe ndege chini kidogo na kuzipata picha tukiwashuhudia Masupa Staa wa Bongo Daslam wakiwa Ilala Shariff Shamba wakiwa ndani ya vyoo vya Pasipoti size?
Machinga complex ni kama kitu kimpya kwa nchi yetu kwahiyo kuna mambo mengi yatajitokeza na ni mapema sana kupima kama mradi huo umefanikiwa au umefeli. Pamoja na mambo mengine kilichokusudiwa ni kuwapumzisha wafanya biashara wadogowado na hata wakubwa kuhangaika na jua mitaan kwa ajili ya juuza bidhaa zao. Sasa, kama manispaa bado inawaachia wafanya biashara wadogowadogo kufanya biashara mitaani na kusababisha msongamano mkubwa town centre, machinga complex haiwezi kupata mtu. Kinachotakiwa ni serikali kudisign policy ambay itakomesha kabisa mtu kufanya biashara ktk maeneo yasiyo ruhusiwa. Upande mwengine ni ule wa kuwassuport wafanya biashara wadogowadogo ili waweze kufanya biashara zao, kama vile mikopo na mengineyo. Kuna mengi yanaweza kufanyika kama kufanya survey kujua hasa nini tatizo lao kwa kuwauliza hao wenyewe na baadae kulitafutia ufumbuzi. Machinga complex inabaki kua ni kitu kizuri hasa kwa huko dunia inakoelekea. Mdau UK
ReplyDeleteNimeamini kuwa maoni huwa lazime yafuate matakwa yako binafsi,upendavyo mwenyewe ndiyo uyatoe.maana nimechangia more than 2x kwenye hii mada muhimu lakini noo kuyaweka. na ninahakika sija chafua hali ya hewa kwani huwa mm sio mtu wa hivyo.
ReplyDelete