Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe Aser Msangi

Watu wasiofahamika wameingia nyumbani kwa mkuu wa mkoa wa Njombe  Keptain Mstaafu Asseri Msangi usiku wa kuamkia Agosti 26.2012  siku ya sensa ya watu na makazi inayofanyika nchini kote na kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja.

Kaptaini Msangi alisema tukio hilo lilitokea usiku wa manane wakati amelala, na alivitaja vitu vilivyoibiwa kuwa ni pamoja na kidadavuo mpakato [laptop] yenye thamani ya shilingi laki saba na nusu pamoja na simu tatu za vijana wake zenye thamani ya shilingi ya laki nne na nusu.

Kaptaini Msangi alisema tukio hilo limemsikitisha sana hasa ikizingatiwa kwamba nyumba yake inalindwa na askari wa jeshi la polisi wenye bunduki zenye risasi za kutosha.

"Nimeishi miaka mingi kwenye nyumba bila ulinzi wowote nilipo kuwa mkuu wa wilaya [DC] sijawahi kuibiwa lakini leo hii mkuu wa mkoa nina walinzi lakini nimeibiwa, mpaka hapa naona haina haja ya kuwa na walinzi"alisema Msangi, akiongezea kuwa anawatilia shaka askari polisi waliokuwa zamu kuwa wanahusika na tukio hilo.


Mkuu huyo wa mkoa aliongeza kuwa wakati mwingine walinzi hao huwa wanatoroka lindo na kwenda kunywa pombe. Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia askari wawili wa jeshi hilo waliokuwa lindo kwa mkuu wa mkoa usiku huo wa tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Njombe Fulgency Ngonyani aliwataja askari hao kuwa ni pamoja na askari mwenye namba G. 5414 PC Ombeni na askari mwenye namba G. 5455 PC Mohamed ambao wakati tukio hilo likitokea ndio waliokuwa zamu ya kulinda kwa mkuu huyo wa mkoa.

"Tunawashikilia askari hawa kwa kuwa ndio walikuwa lindo, lakini hata hivyo tumefanya uchunguzi wa awali hatujaona sehemu yoyote iliyobomolewa yawezekana watu walifanya tukio hilo la wizi walitumia funguo bandia" alisema Kamanda Ngonyani.

Akizungumzia hataua ya askari wa jeshi hilo kuwa na tabia ya kuacha lindo na kwenda kunywa pombe, Kamanda Ngonyani alisema hana taarifa hizo lakini aliahidi kulifanyia kazi, ambapo amemwagiza mkuu wa upepelelezi kufanya uchunguzi juu ya jambo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Wananchi wa kawaida wanaibiwa kila siku. Welcome the club Mr. mkuu wa mkoa.

    ReplyDelete
  2. Ahhh hii kali,

    Ndio pale unashuhudia HAKIMU anaibiwa kalamu anayoandikia hukumu Mahakamani!

    ReplyDelete
  3. Tanzania tunatakaiwa tujipange sawa sawa,

    Mambo mengi tunayachukulia rahisi rahisi sana , sijui labda ni ile mwongozo wetu wa kiujamaa au ndio nini?

    Mkuu wa Mkoa ni mtu hata inzi anashahili asikatize usoni kwake kirahisi.

    Tizameni suala la Ziwa Nyasa Malawi nchi ya watu 45 Milioni wanalisimamia watu wasiozidi 45 tu!

    Na mara zote suala hili linaonekana ni jukumu la Mwanasheria Mkuu wa Serikali peke yake na Mhe.Bernard Membe, boti linazama tunanyang'anywa ziwa,,, je Vyama vya Siasa vya Upinzani mpo wapi???

    Ndio Uzalendo kweli huu???

    ReplyDelete
  4. AHAAAAAAAAAAAAAA
    CAPTAIN ANALALA HADI ANAIBIWA LAPTOP NA SIMU. HALAFU ANALAUMU POLISI WALINZI, WAKATI NA YEYE NI ASKARI. KUNA UZEMBE PANDE ZOTE

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli kuibiwa ni kubaya na hakuna mtu anayependa aibiwe lakini wakubwa kama hawa wakiibiwa linakuwa ni fundisho zuri kwamba na wao angalau waonje taabu na mateso tuyapatayo sisi wa chini huko mitaani ambao nyumba zetu hazina hata walinzi!!! Pole mheshimiwa mkuu wa mkoa.

    ReplyDelete
  6. NJOMBE ni mkoa siku hizi?

    ReplyDelete

  7. Wakumbukeni kweny vile vi mlo vya usiku, njaa halafu wanakuwa treated like lowest lives.

    ReplyDelete
  8. Hahahahaha,

    Hapa ndiyo unashuhudia simba mnyama mkali mchana kweupeee anachinjwa na Teja wa unga kwa wembe!

    Mijizi nuksi, mnamwibia hadi 'Kanali Mstaafu' (Asikari),ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa(Raisi wa Mkoa)?

    Ebo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...