Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limetoa tahadhari kwa wananchi kuwa makani na fedha wanazolipwa ili kuepuka kubambikizwa noti bandia ambazo tayari jeshi hilo limekamata zaidi ya bandia zenye thamani ya zaidi ya shilingi 700,000.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amesema leo kuwa noti hizo zimekamatwa na askari polisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi wasamaria wema.
Kamuhanda alisema kuwa hadi sasa jeshi hilo la polisi linawasaka wahusika wa mtandao huo wa kusambaza noti bandia katika mkoa wa Iringa ili kuchukuliwa hatua za kisheria.
Alisema kuwa fedha hizo ambazo zimekamatwa katika maeneo tofauti tofauti zina namba ambazo zinafanana na hivyo kuwataka wafanyabiashara na wakulima kuwa makini na watu wanaofika kununua mazao yao .
FEDHA HALALI IMO MIKONONI MWETU!
ReplyDeleteWanyalu huko Iringa, ndugu zangu asalaleee, hakuna sababu ya kutoana damu sisi kwa sisi kwa fedha bandia na kurudishana nyumakimaisha na kimaendeleo.
Nchi yetu ina mimali kibao na fursa lukuki za kuzichonga fwedha tena za halali kiulaini!!!
Angalieni nchi yetu inakodolewa mimacho na hata majirani zetu, inagombewa kama mpira wa kona!
Tazameni tunaburuzana na Malawi juu ya umiliki wa ziwa Nyasa, pia mmeona wandugu zetu Kenya wanavyolalamika kutaka kututumia Tanzania ki uchumi kama kimbilio la soko la ajira kwa watu wao.
Zindukeni Wanyalu !!!