Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Wazo lilianzia kwenye miti ya mitiki, baadae nikaongeza ufugaji wa samaki, kisha nikagundua kwamba ninaweza kuongelea chochote kuhusu kilimo na ufugaji kwa kutumia utaalam wa darasani pamoja na ule wa kienyeji (under field conditions) Nimeamua kutumia njia hii ili iweze kuwasaidia wale ambao wako mbali na wataalam wa misitu, kilimo na ufugaji. Kwa msaada zaidi na maswali tuwasiliane (mitiki1000@gmail.com)
Globu ya Jamii inampongeza mdau Chris Bennet kwa hatua hii, ikizingatia kwamba wakati sasa umefika kwa wadau kuanzisha blog za kuelimishana katika nyanja mbalimbali zenye mhemko wa kuelimisha wadau, na kwamba blog si lazima ziwe za habari tu.
Hongera sana Chris!! Kaza buti na lete vitu kila siku....
-ANKAL
blogu nyingi sana ankal, hamuwezi kushea habari kidogo. muda wenyewe uko wapi wa kutembelea blogu kumi kila siku?
ReplyDelete