Sijuwi nianzie wapi Kaka Michuzi nimepitia maelezo katika blog yako tukufu inayo tuhabarisha mengi na kutuelimisha ahsante, lakini kuna moja linalo nikera mie kama mdau wa blog yako na nilikuwa sijabahatika kuwasiliana nawe kwa kuwa sikuelewa nianzie wapi.
Sasa nimewapata na ningependa kujifunza mengi kupitia blog hii, Kero ya kwanza ni ile ya TANESCO kuwalazimisha wateja kurithi madeni yalio achwa na wamiliki wa nyumba husika hata kiupangaji, nitakupa mfano wa kitongoji kimoja hapo Mwanza Mkuyuni kweny maghorofa yaliokuwa yanamilikiwa na Railway kwa sasa yako chini ya idara ya ujenzi Mwanza, hizo nyumba zinapangishwa kwa kiasi cha Tsh 50000 kwa mwezi unalipia miezi 6 sawa na laki 3, sasa basi mpangaji alie ishi hapo miaka 2 au 3 akitumia mita ya kawaida amehama na kaacha deni labda la laki au elfu sabini, sasa wewe umepewa nyumba na hutaki kuchangia umeme na wengine kwa hofu ya kero za uchangishanaji, unaamua kuweka mita yako ya LUKU, utaambiwa ulipe kwanza hilo deni ulilolikuta hapo ndio upewe umeme au utafungiwa LUKU kisha unakatwa kila mwezi kiasi ca elfu 5000 au kumi itategemea na ukubwa wa deni, ulilorisishwa kwa nguvu kwakua eti unashida ya UMEME, kwanini wasiwepo wauzaji umeme binafsi tuondokane na huo mfumo wa KIDIKTETA???
Kaka Michuzi nakuomba ulifanyie kazi swala hili na kisha uliweke bayana kwa walengwa na wadau woooote wa blog yetu hii tukufu.
AHSANTE
Wako ADAMS CHUMA
Bwana Chuma...HAISWIHI kila mtu ataadidhibiwa kwa dhambi aliyiofanya....!!!!!! Atafutwe aliyetumia na alipe....!!!
ReplyDeleteKaka Michuzi, masuala mengine ni ya kutojua sheria. Mdau asitumie jazba kutufanya nasi mbumbumbu wa sheria. Nenda kasome "The doctrine of recent possession" kiufupi Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi wa ng'ombe.
ReplyDeleteHii ndio Bongo wahusika wanapenda mtelemko. Utakayejipeleka basi ujue imekula kwako. Upuuzi kama huu upo Bodi ya Mikopo ambapo wale waanaolipa s=deni ndio wanzidi kutwishwa mzigo mzito kufidia asiyelipa. TRA wanaangalia tu kodi ya wafanyakazi, na wamiliki wa magari, ndio wanakamua kweli, lakini wafanyabiashara mitaani huko wanapeta tu. Yaani nchi sijui ina sera au haina sielewi.
ReplyDeleteBwana Chuma, utazame vizuri Mkataba wako na Landlord wako, ikiwa haukubani basi deni hilo ni la mwenye nyumba .
ReplyDeleteTANESCO utagombana nao bure, huduma lazima ilipiwe na wao wanadai mmiliki wa nyumba. Hivyo jipange kisha fanya maamuzi.
Bila shaka hii itakusaidia lakini haitakupendeza bila shaka.
Michuzi kwa wanaojua Sheria hii si Hoja, kwa kawaida unaponunua gari la wizi, ukikamatwa nalo wewe ndio unakuwa mwizi, unatakiwa kujiridhisha kwa kila jambo kabla ya kununua kitu chochote. Wataalam wa sheria wanaita The Doctrine of recent possession" Hivyo mdau aliyeleta hii mada japo TANESCO nao kunasehemu wanachemka, ajipange upya. Asitufanye sote ni vihio wa sheria. By Learned Brother.
ReplyDeleteUnashangaa nini sasa hapo wewe?
ReplyDeleteMbona wao TANESCO wameambiwa na mahakama wawalipe DOWANS mabilioni ya shilingi wakati hawakuwahi kuwa na makataba nae bali walikuwa na mkataba na RICHMOND?
Hii ndo Tz. bwana we acha tu ni UWENDAWAZIMU mtupu nchi hii.
NIJUAVYO MIMI KABLA YA KUNUNUA AU KUPANGA NYUMBA NI LAZMA UJUE ANADAIWA NINI NA NANI NDIO UINGIE MKATABA,NDIO MAANA INASHAURIWA KABLA YA KUNUNUA AU KUPANGA KUPITIA KWA WANASHERIA KUKWEPA HAYO,NA DENI LA MATUMIZI YA NYUMBA DHAMANA NI NYUMBA,KWA HIYO HILO LAKO USIKWEPE,KWANI UNGEKUTA JAMAA ALILIPA MIEZI 6 ZAIDI UNGELUDISHA TANESCO.
ReplyDeletePole kwa kuingia mkenge! Huna jinsi zaidi ya kulipa hilo deni maana ulitakiwa umbane mwenye nyumba aliyekupangisha alipe deni lake kabla hujaingia naye mkataba au mkataba unge litambua deni hilo na jinsi ya kulilipa. Vinginevyo TANESCO wanahaki ya kumdaiweny nyumba ambayo ndio ww unaishi na wakitaka kukata watakata nyumba hiyo wanayodai hata kama mmiliki si ww hawawezi kumfuata huyo aliyekupangisha huko aliko.m
ReplyDeleteHiyo du! haya, sasa na hili la kubadili software ili itutafunie vipesa vyetu vipi?
ReplyDeletetehe tehe tehe! jamani miguu yangu! sory jamani mbavu zangu! Du! n'nji ya kitu kidogo!
ReplyDeleteWA-TANZANIA TUNAPENDA MAISHA YA "DILI DILI" NDIO HAYO YANATUPONZA LAZIMA KITU UWE MAKINI NACHO NA UKICHUNGUZE KISIJE KUKUZURU HAO TANESCO WANAYO MAKOSA YAO ILA LAZIMA PIA UNAPOITAKA NYUMBA UFUATILIE YOTE YA KWENYE UPANGAJI WA NYUMBA KUANZIA MAJI NA TAKATAKA ZOTE ZA BILI MUANDIKISHANE NA NDOMANA WANASHERIA WAPO PIA UWE NA MASHAHIDI NA HIZO SEHEMU ZOTE ZA BILI WAJUE NDIO SASA UNACHUKUA HIYO NYUMBA LASIVYO UTAJIKUTA UPO NDANI YA NYUMBA NA UNAAMBIA SI NYUMBA YAKO.
ReplyDeleteBWANA CHUMA ASIKUDANGANYE MTU DENI SIO LAKE. WANASHERIA FEKIB ETI RECENT POSSESSION KWANI NI CRIMINAL CASE HIYO? TANGU LINI DENI LA UMEME LIGEUZWE WIZI? WEWE UMEIBA NINI? RECENT POSSESSION NI UNAPOKAMATWA NA MALI YA WIZI, WEWE MPANGAJI, TAREHE ULIYOINGIA NYUMBANI IPO, UJE URITHISHWE DENI LA MWINGINE TANGU LINI. WEWE UNAFIKIRI VISHOKA WANAANZIA WAPI? NDIO HAYA YA KUBEBESHANA MADENI. MIMI NAKUSHAURI UONGEE NA MWENYE NYUMBA AMFUATILIE MDENI WAKE AKISHINDWA NA WEWE MFANYIZIE. SIKU UKIHAMA ACHA LIDENI LA NGUVU, KWANI HELA ZAKO UNAOKOTA? ETI RECENT POSSESSION HII NDIO LAW SCHOOL? POLENI FIRST YEAR LLB ANATAKIWA ATOFAUTISHE CRIMINAL LAW NA CIVIL LAW.
ReplyDeleteDOCTRINE OF RECENT POSSESSION NI CRIMINAL LAW SIO CIVIL MATTER. DENI LA UMEME HALINA UHUSIANO NA HII DOCTRINE, WANASHERIA WA VIJIWENI NINI?
ReplyDeleteBWANA CHUMA MDAI MWENYENYUMBA AKIKATAA MBURUZE MAHAKAMANI
Hapo TANESCO haihusiki na hii inatufundisha kwamba unaoosainishana mkataba na mwenye nyumba kabla lazima uangalie maji yamelipwa na umeme, na hata wenye nyumba makini huwa wanakomaa kuhakikisha mpangaji wake ana settle umeme. TANESCO tunawaonea na wakiruhusu hii kwa Watz basi ndio itakuwa mchezo wa kila mtu pia itakuwa deal kwa staffs wa TANESCO, nimependa mchango wa Che Guavara
ReplyDelete