Mchora vibonzo, Nathan Mpangala (mwenye nyanya pensi), akigawa vifaa vya kuchorea kwa watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbil, Jijini Dar es Salaam, Jumamosi, 29.09.2012. Ziara hiyo ni sehemu ya maadhimisho miaka sita ya KIBONZO kinachorushwa ITV na pia ni sehemu ya shughuli za kijamii baada ya kupata tuzo ya uchoraji bora wa katuni, 2011 aliyopewa na Baraza la Habari Tanzania.
TUMWONESHE NA SISI TUNAWEZA KUCHORA VIBONZO VILEVILE. Baadhi ya watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam, wakimwonesha uhodari wa uchoraji katuni, mchora vibonzo, Nathan Mpangala, aliyechutama, Jumamosi, 29.09.2012. Ziara hiyo ni sehemu ya maadhimisho miaka sita ya KIBONZO kinachorushwa ITV na pia ni sehemu ya shughuli za kijamii baada ya kupata tuzo ya uchoraji bora wa katuni, 2011 aliyopewa na Baraza la Habari Tanzania.
Jumamosi, 29.09.2012 mchora vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala, alipata nafasi ya kutembelea watoto wanaosumbuliwa na saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuwapa zawadi na kuchora nao kama sehemu ya kuadhimisha miaka sita ya KIBONZO kinachorushwa ITV na pia kama sehemu ya shughuli za kijamii baada ya kupata tuzo ya uchoraji bora wa katuni, 2011 aliyopewa na Baraza la Habari Tanzania.
Malengo ya ziara hiyo yalikuwa;
(i) Kutoa msaada kwa watoto.
(ii) Kuchora katuni pamoja na watoto ili kusaidia kuwaondolea unyonge, wasiwasi, na kuwafanya kutoyaogopa mazingira ya hospitali kwani katuni zinachekesha.
(iii) Watoto watapata fursa ya kueleza hisia zao kuhusu saratani kupitia katuni hivyo kupeleka ujumbe kwa jamii kuupa ugonjwa huu uzito sawa kama upewavyo malaria, ukimwi nk.
Nawashukuru ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wa mbalimbali wa katuni walioniunga mkono katika zoezi hili.
Pia nashukuru wachoraji katuni wenzanu walioniunga mkono kwa kuja kuchora na hawa watoto. Natoa wito kwa wachoraji katuni wengine nchini, kutenga muda angalau mara moja kwa mwaka kutembelea watoto walio mahospitalini sehemu mbalimbali nchini na kuchora nao kwani watoto wanapenda katuni.
Katuni zina mchango kiafya. Huchangamsha akili na kupunguza msongo wa mawazo. Kwa mgonjwa, tabasamu ni jambo muhimu sana.
Kama uchoraji katuni utatumika mahospitalini, utasaidia kuwasahaulisha watoto mazingira ya hospitali kwani watajihisi kama wako nyumbani.
Mungu Ibariki Tanzania.
Kwa mawasiliano na kuona kazi zake nenda:
ReplyDeleteCancer has really being a problem in Africa countries i found out that there are very few survive compared to the western and Eastern countries i wounder what is the problem.. now look at these children,,, am so disappointed
Hongera Sana Nathan!! Ni mfano wa kuigwa kwa watu mbalimbali kufanya kama ulivyofanya wewe kwa jamii iliyoko kwenye matatizo kama hospitalini na sehemu kama hizo!! watoto wanahitaji sana upendo!!!
ReplyDeleteMpangala hongera kwa kuwapa mkono wa pole watoto Hospitalini,
ReplyDeleteMtoto Godfrey Chiweka kwa kipaji alichoonyesha anahitaji mkono wako zaidi akitoka Hospitalini kwa Matibabu umepata wa kumwachia urithi!!!