Kibaka alieanaswa akiiba vitu kwenye mkoba wa mama (huyo mwenye kilemba) akiwa amewekwa chini na wasamalia waliomnasa kabla ya kuanza kumtembezea kichapo alipobaini kuwa kuna vitu vingine alivyokuwa ameviiba awali.kibaka huyu amenaswa mchana wa leo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
 Kichapo cha nguzu kikaanza,jamaa analia kama mtoto mdogo huku akisema sirudiii tena jamaniiii....
 hapa ni bakora kwa kwenda mbele.
 Baadae akasamehewa na kuamria kuondoka eneo hilo.
 Msamalia mwingine alijitokeza na kumsukuma ili aondoke na asionekane tena katika eneo hilo.
Kibaka yuleeeeeee......

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. tuna safari ndefu sana katika upande huu ......

    ReplyDelete
  2. Hii ni mbaya sana,kumlimba binadamu mwenzio siyo uugwana!

    ReplyDelete
  3. Mpelekeni polisi badala ya kumpiga au mtafutieni ajira aache kuiba. Njaa tu inamsumbua.

    ReplyDelete
  4. utawala wa sheria binafsi.

    ReplyDelete
  5. njaa haziwezi kuisha ikiwa walalahoi wanashindwa kumiliki kitu mlo

    na kwa upande wa mafisadi wanashindana kwa kutaka kumiliki ndege maana magari na majumba sasa sio kitu kwa mafisadi.

    mpeni kula mfa njaa mwenzetu huyo msimuongezee shida ya kutafuta madawa kwa kumtia majeraha

    ReplyDelete
  6. Huu ulikuwa ni mkutano uliohudhuriwa na wakubwa wa nchi lakini sheria imevunjwa, watu wamechukua sheria mkononi badala kumpleka polisi.

    ReplyDelete
  7. WAZO JIPYA:

    '''NJAA HAINA UBAUNSA''''

    Nafikiri tujaribu kufungua ukurasa mpya wa maisha na sasa badala ya kuwapiga vibaka na wezi tuwakamate na kuwauliza wanaiba kwa nini?

    Wakijibu nadhani Majibu yao hayatakuwa nje ya hapa:

    1.Nina njaa sijakula.
    2.Nina majukumu nategemewa.
    3.Ninaumwa natafuta hela ya matibabu.
    4.Akili yangu sio timamu nina ugonjwa wa akili lakini pana wakati napata nafuu najitambua.

    Sasa wandugu kwa majibu mojawapo ya hayo manne (4) hapo juu, nadhani upo uwezekano wa mbadala kuliko kuwapiga!

    TUTAFANYA HIVI KWA MAJIBU YA MASWALI HAYO MANNE HAPO JUU:

    1.Jumuia hasa za Kiimani Misikiti na Makanisa watoe huduma za msaada wa chakula cha bure angalau mlo mmoja kwa siku.

    2.Wapewe kazi za Kijamii ili wapewe angalau chochote kujikimu.

    3.Wapewe Msaada wa Matibabu ya bure vituo vya Afya.

    4.Wapelekwe vituo vya Matibabu ya Afya ya akili.

    HII IWE KWA WEZI WAKIKAMATWA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...