Jengo la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam linavyoonekana kwa nje baada ya kukamilika. Jengo hilo linalomilikiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  lipo Makutano ya Barabara za Shaaban Robert na Garden Jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule (kushoto) akimkaribisha Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb.), Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Katibu Mkuu, Bw. Haule akiwakaribisha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere walipokitembelea hivi karibuni.

Wajumbe wa Kamati ya NUU na Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati akiwakaribisha.

Mhe. Azzan akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya NUU na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje. Kulia ni Balozi Rajab Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje.

Katibu Mkuu, Bw. Haule akitoa maelezo kuhusu Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama waliotembelea kituo hicho 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana Wachina, Mnatuokoa sana.
    Maana yake sisi hatuwezi kujenga wenyewe hatuna Wakandarasi Wazuri.

    Tujengeeni Kila Kitu.

    Reli
    Barabara
    Madaraja
    Majengo ya Mikutano
    Mashule
    Mabweni
    Mahoteli
    Viwanja nya Michezo
    Na Mengine yote

    Mungu atawazidishia.

    ReplyDelete


  2. Hhah we mdau wa kwanza una matatizo sanaaa,,,

    sasa unadhani Tanzania kuna mkandarasi wa kujenga vitu adimu kama hvyo?? ebu angalia mwenyewe majengo yaliyo jengwa na udsm graduates wanao jiita wakandarasi alafu linganisha na majengo ya mcina wewe mwenyewe utajua kwamba Tanzania hakuna wakandarasi ila kuna vibarua wa wakandarasi

    Linganisha mjenzi wa TCRA tower
    Angalia EXIM Tower Posta
    Angalia BOT twin Tower
    Angalia DCB Bank Magomeni
    Angalia Airtel Center

    Haya Mbongo
    Benjamin Mkapa Tower
    Utumishi Building
    Magorofa ya Kariakoo

    Hapo utajua kwamba Tanzania hakuna wakandarasi labla yule

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...