Mkurugenzi wa Women in Balance Dina Marios akizungumza na wageni waalikwa kufafanua hatua ya awali ya maandalizi ya kufanyika kwa tukio la mafunzo ya‘Kitchen Party Gala’ kwa kina mama jinsi ya kuishi ndani ya ndoa ili kujenga familia bora litakalofanyika mnamo tarehe 21 mwezi huu.

Akifafanua zaidi amesema tukio hilo la 4 litakalokuwa la mwisho kwa mwaka huu litakalofanyika kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 4 usiku litafanyika katika hali ya ubora zaidi katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Aidha amewataka wanawake kuhudhuria kwa wingi ili waweze kupata faida kwa ajili yao binafsi na kuweza kuwa waalimu bora kwa waume zao jambo litakalosaidia kuepusha migogoro ya mara kwa mara inayopelekea kuvunjia kwa ndoa.

Wadhamini wa Kitchen Party Gala ni TSN Super Market, Sossi, Coca Cola na Clouds Fm.
Mahali:Diamond Jubilee VIP hall

Muda:Kuanzia saa nane mchana mpaka saa nne usiku.
Kiingilio ni Tsh 30,000

Ukitaka kubook meza ya watu kumi piga namba 0787583132,0716485666
Safarii hii ukiacha wasemaji kuna burudani ya kila aina ukizingatia ni ya mwisho kabisa kwa mwaka huu.Bila kusahau chakula,na vinywaji laini.
 
RANGI YA SIKU.
Kwa muda kina dada/mama mmekuwa mkitoa maoni mnataka kushona nguo mtokelezee.
Basi rangi ya siku ni rangi ya chenza (tangerine tango)color of the year 2012.
Ishone utakavyotaka wewe iwe kitambaa cha kawaida,kitenge,kanga,batiki,au ukachanganya vyovyote ili mradi uzingatie rangi ya siku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Huyu Dina Marios mbona hana mume hiyo kitchen party atatwambia nini. Wewe achia wakina mama wanaojua utamu wa ndoa wandae sio upuzi huo!! pia nashauri kina baba wasiwepo maana inawafaa kina mama tu.

    ReplyDelete
  2. mdau huo ni mradi wa watu kujipatia pesa hivyo huingia wote bila kujali maadili wanaume pia ndani waliolewa na wasiolewa ndani, wanashindwa kuelewa kuwa ndoa haina formula, hivi vitu vina flow na mazingira na wakati na wakati mwingine ni kumshirikisha mungu zaidi. hata uhudhurie kitchen party gala 1000 mambo yakitaka kuharibika uharibika tu.

    ReplyDelete
  3. Dina unaijua ndoa?jipe kitchen party mwenyewe kwanza ili uolewe.Au ndo kibiashara zaidi?Nakutakia kila la kheri dada!!!

    ReplyDelete
  4. Yaani hii nchi shillingi inasakwa hata kwa mbinu zisizoeleweka...huyu yeye aandaa kitchen party ya ndoa kama nani? Eish yeye anaijua ndoa huyu? Jamani watanzania tuwe serious, sio kwa sababu ana platform ya kuzungumza anachotaka basi ndio apewe nafasi...aha inabore.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...