TUNAPENDA KUWAFAHAMISHA WASAFIRI WETU WA RELI YA KATI DARAJA LA TATU KWAMBA, KUANZIA SASA WATOTO  WA UMRI CHINI YA MIAKA SABA WATASAFIRI BURE NA WATAPEWA KITI/VITI.  
WATOTO HAO WATATAKIWA KUSAFIRI NA WAZAZI/WALEZI WAO NA PIA WAJE NA VYETI VYA KUZALIWA AU BARUA YA SERIKALI YA MTAA HUSIKA KUTHIBITISHA UHUSIANO NA MZAZI/MLEZI WAKE.  
MZAZI/MLEZI ATAKAYESAFIRI NA WATOTO HAO ATARUHUSIWA WATOTO WASIOZIDI WAWILI KWA WAKATI MMOJA NA NILAZIMA AJE NA VITHIBITISHO HIVYO WAKATI WA KUNUNUA TIKETI YAKE NA AWAANDIKISHE KWA KARANI/STESHENI MASTA ILI WAWEZE KUPATA TIKETI ZA KUSAFIRIA. 
MTOTO ATAKAYEKUTWA NDANI YA TRENI BILA TIKETI ATALIPIA NUSU NAULI YA MTU MZIMA. 
TUNAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI KUBORESHA HUDUMA HII.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano
kwa nIaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TRL Mtendaji
Mhandisi Kipallo A.Kisamfu
Dar es Salaam.

ANGALIZO: Miundo mbinu ya Reli ni mali ya Taifa hivyo basi 
shiriki katika kuitunza ili tukuhudumie kwa ufanisi zaidi  !

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. MBARIKIWE SANA UONGOZI WA RELI YA KATI!MMEFANYA JAMBO JEMA MNO!
    HUWAMPAKA SASA NAWAZA MSONGAMANO WA DARAJA LA TATU,JOTO NA SAFARI NDEFU KAMA HIYO KWA WATOTO,,MAMA YANGU ILIKUWA HATARI SANA,,,
    MOLA AKUJAZENI HIKMA NA WENGINE WAFUATE MWENENDO WENU,,
    BILA NYIE VIONGOZI KUTUHURUMIA SISI RAIYA,HAKUNA ATAKAE TUONA,,NI KUBAKIA TU TUNASUBIRI NUSURA YA MUNGU
    AHLAM,,LONDON

    ReplyDelete
  2. Kazi nzuri sana!

    Manendeleo na hali bora hutafutwa, kupangwa na kusimamiwa kama hivi.

    Badala ya kulaumiana na kusemana vibaya.

    Hongera sana Sana Shirika la Reli!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...