TUNAPENDA KUWAFAHAMISHA WASAFIRI WETU WA RELI YA KATI
DARAJA LA TATU KWAMBA, KUANZIA SASA WATOTO
WA UMRI CHINI YA MIAKA SABA WATASAFIRI BURE NA WATAPEWA KITI/VITI.
WATOTO HAO WATATAKIWA KUSAFIRI NA
WAZAZI/WALEZI WAO NA PIA WAJE NA VYETI VYA KUZALIWA AU BARUA YA SERIKALI YA
MTAA HUSIKA KUTHIBITISHA UHUSIANO NA MZAZI/MLEZI WAKE.
MZAZI/MLEZI ATAKAYESAFIRI NA WATOTO HAO
ATARUHUSIWA WATOTO WASIOZIDI WAWILI KWA WAKATI MMOJA NA NILAZIMA AJE NA
VITHIBITISHO HIVYO WAKATI WA KUNUNUA TIKETI YAKE NA AWAANDIKISHE KWA
KARANI/STESHENI MASTA ILI WAWEZE KUPATA TIKETI ZA KUSAFIRIA.
MTOTO ATAKAYEKUTWA NDANI YA TRENI BILA TIKETI
ATALIPIA NUSU NAULI YA MTU MZIMA.
TUNAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI KUBORESHA HUDUMA HII.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano
kwa nIaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TRL Mtendaji
Mhandisi Kipallo A.Kisamfu
Dar es Salaam.
ANGALIZO: Miundo
mbinu ya Reli ni mali ya Taifa hivyo basi
shiriki katika kuitunza ili
tukuhudumie kwa ufanisi zaidi !
MBARIKIWE SANA UONGOZI WA RELI YA KATI!MMEFANYA JAMBO JEMA MNO!
ReplyDeleteHUWAMPAKA SASA NAWAZA MSONGAMANO WA DARAJA LA TATU,JOTO NA SAFARI NDEFU KAMA HIYO KWA WATOTO,,MAMA YANGU ILIKUWA HATARI SANA,,,
MOLA AKUJAZENI HIKMA NA WENGINE WAFUATE MWENENDO WENU,,
BILA NYIE VIONGOZI KUTUHURUMIA SISI RAIYA,HAKUNA ATAKAE TUONA,,NI KUBAKIA TU TUNASUBIRI NUSURA YA MUNGU
AHLAM,,LONDON
Kazi nzuri sana!
ReplyDeleteManendeleo na hali bora hutafutwa, kupangwa na kusimamiwa kama hivi.
Badala ya kulaumiana na kusemana vibaya.
Hongera sana Sana Shirika la Reli!