Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Jeshi la Polisi Zanzibar, linawashikilia watu 65 wakiwemo viongozi sita wa kundi la Uamsho na Jumuiya ya Maimam Zanzibar kwa tuhuma za kuchochea ghasia na vurugu zilizosababisha  vitendo vya uporaji wa mali na uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Insptekta Mohammed Mhina, amesema kuwa pamoja na kukamatwa kwa viongozi hao wa Jumuia mbili za Kidini mjini Zanzibar, Polisi pia imewakamata watu wengine sita kwa tuhuma za mauaji ya Askari Polisi.
Insepekta Mhina, amewataja viongozi waliokamatwa kuwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimau Zanzibar Sheikhe Faridi Hadi Ahmed(41) mkazi wa Mbuyuni na Sheikhe Mselem Ali Mselem(52) wa Kwamtipura  ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar.
Wengine ni Sheikhe Azan Khalid Hamadi(48) wa Mtendeni, Hassan Bakari Suleiman(39) wa Tomondo na  Ustaadh Mussa Juma Issa(33), Suleiman Juma Suleimain(66) pamoja na Mussa Juma Issa(37) wote wa Makadara mjini Zanzibar.  
Inspekta Mhina amesema viongozi waliokamatwa ni wale walikuwa wakihojiwa na Polisi tangu jana kwa lengo la kutafuta ukweli wa taarifa za kutekwa kwa Sheikhe Farid Hadi Ahmed kulikopelekea ghasia na uharibifu mbalimbali kabla ya kujitokeza tena hadharani juzi.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Kamamishina wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa amesema kuwa Jeshi la Polisi Visiwani humo linaendelea na operesheni maalumu ya kuhakikisha kuwa kila aliyehusika katika ghasi hizo anakamatwa na kukabili mkono wa sheria.
Akizungumzia maendeleo ya Upelelezi wa Kesi ya Kuuawa kwa Askari Polisi CPL Said Abdarahaman Juma aliyeuawa usiku wa kuamkia Alhamis wiki iliyopita, Kamishna Mussa amesema Polisi wamefanikiwa kuwatia nguvuni watu sita kwa kuhusika na mauaji ya askari huyo.
Amesema hadi sasa Polisi inawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya askari huyo ambapo watuhumiwa watatu walikamatwa mjini Zanzibar na wengine watatu wamekamatwa mkoani Tanga.
Kamishna Mussa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Abdallah Mohammed Said(35) wa Mwanyanya, Joli Gasuli(20) wa Vuga, Bakari Juma Yusufu(22) wa Mwembe Makumbi  na Amour Rished(40) wa Bububu ambao walikamatwa mjini zanzibar siku ya kwanza lilipotokea tukio hilo.
Amewataja watuhumiwa wengine ambao wamekamatiwa Mkoani tanga na ambao tayari wamesharejeshwa Zanzibar kuwa ni  Ali salum Seif(21) na Abubakari Haji Mbarouk(32) pamoja na mdogo wake Mohammed Haji Mbarouk(21) wote wakazi wa  Ndagaa mkoa wa Kusini Unguja.
Kamishna Mussa amesema Polisi bado inaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na wale watakaobainika kuhusika na mauaji ya askari huyo watafikishwa mahakamani.
Amesema kwa ujumla tangu kukamatwa kwa viongozi hao hali ya usalama katika mji wa Zanzibar imerejea upya na wananchi wameombwa kutoshabikia vitendo vyovyote vile vitakavyoweza kupelekea uvynjifu wa amani.
Amewataka Wazazi na walezi kutowaruhusu watoto wao kshiriki katika mikusanyiko na kuwa chanzo cha fujo na kwamba kwa yeyote atakayekaidi agizo hilo atashughulikiwa ipasavyo na mkono wa dola.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Yaani huyu mpuuzi alijificha ili wafuasi wake wavuruge amani, huyu Farid haitakii mema nchi yetu kuna haja sasa Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria ili wahindwe na adhma yao hawa watu wachache ya kuifanya nchi isikalike.

    ReplyDelete
  2. Kwanza ukimwangalia tu unamuona ni mu OMAN halafu anataka kutuaribia nchi yetu, Si aende huko OMAN nchi nzuri na waislamu watupu?, Anangangania zanzibar kwanini? wanzanzir wote asili yao ni Bara, je anaongea lugha ghani ya huku bara? wanzanzibar ni wamakonde,wandengereko, wazaramu, wa nyamwezi je yy ni kabila gani?akijibu ndio aidai zanzibar kama hayumo ktk makabila ya bara bora aende zake OMAN

    ReplyDelete
  3. Anoy wa kwanza Naungana na wewe tena hizo hatua ZICHUKULIWE ZA KINIDHAMU ZIDI YA ZANZIBAR WAFUKUZWE KWENYE MUUNGANO KABISA KWA KUTOWEZA KUTEKELEZA MATAKWA YA MUUNGANO .
    MFANO MAFUTA WANAYATAKA WAO-WAMEUNDA JESHI LAO LA KMKM WAKATI HAIRUHUSIWI,WANA BENDERA YAO WANA WIMBO WA TAIFA

    KWA NINI HAWAFUKUZWI KWENYE UWANACHAMA WA MUUNGANO? KISHA IKABAKIA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZAMBIA KAMA NAIBU WAZIRI WA ELIMU WA TANZANIA ALIVOSEMA VIDEO YA JUU HAPO?
    TUACHIWE TUPUMUWE...

    ReplyDelete
  4. Hata Ulimboka alijificha Mabwepande.

    Fungua macho yako vyema

    ReplyDelete
  5. ikiwa amejificha kwa makusudi kuchafua amani ya nchi itakuwa ni makosa makubwa

    lakini kabla ya kumuita mpuuzi anza kujiita wewe mdau hapo juu kuwa ni mpuuzi wa mwisho maana una uhakika gani na yaliyoandikwa?
    una uhakika gani kama alijificha kwa makusudi ali alitekwa?

    wananchi ni rahisi sana kushawishika na hivi vyombo vya habari maana wanaweza kutuhabarisha kuwa alijificha na kumbe alitekwa

    suala la kutekwa sio jambo geni kwa hawa wana harakati maana hata kule kenya kuna mmoja alieuliwa na mwingine kutekwa je na hao ni wapuuzi?

    ReplyDelete
  6. Nyinyi watu weusi mna matatizo gani na waarabu, hawa ni raia wa tanzania kama wewe, kuwa mweupe sio tija kubaguliwa, nchi kama marekani isingepata rais mweusi kama wangefata sera kama zako wewe, manaake watu weusi asili yao Africa kwahiyo wanyimwe haki kule walipo. mwehu mkubwa, mbaguzi wa rangi, ndio baba yako wa taifa alivyokufundisha hivyo eenh

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...