Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Jeshi la Polisi Zanzibar, linawashikilia watu
65 wakiwemo viongozi sita wa kundi la Uamsho na Jumuiya ya Maimam
Zanzibar kwa tuhuma za kuchochea ghasia na vurugu zilizosababisha vitendo vya uporaji wa mali na uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Afisa
Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Insptekta Mohammed Mhina,
amesema kuwa pamoja na kukamatwa kwa viongozi hao wa Jumuia mbili za
Kidini mjini Zanzibar, Polisi pia imewakamata watu wengine sita kwa
tuhuma za mauaji ya Askari Polisi.
Insepekta
Mhina, amewataja viongozi waliokamatwa kuwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Maimau Zanzibar Sheikhe Faridi Hadi Ahmed(41) mkazi wa Mbuyuni na
Sheikhe Mselem Ali Mselem(52) wa Kwamtipura ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar.
Wengine ni Sheikhe Azan Khalid Hamadi(48) wa Mtendeni, Hassan Bakari Suleiman(39) wa Tomondo na Ustaadh Mussa Juma Issa(33), Suleiman Juma Suleimain(66) pamoja na Mussa Juma Issa(37) wote wa Makadara mjini Zanzibar.
Inspekta
Mhina amesema viongozi waliokamatwa ni wale walikuwa wakihojiwa na
Polisi tangu jana kwa lengo la kutafuta ukweli wa taarifa za kutekwa kwa
Sheikhe Farid Hadi Ahmed kulikopelekea ghasia na uharibifu mbalimbali
kabla ya kujitokeza tena hadharani juzi.
Akizungumza
na Waandishi wa habari ofisini kwake, Kamamishina wa Polisi Zanzibar CP
Mussa Ali Mussa amesema kuwa Jeshi la Polisi Visiwani humo linaendelea
na operesheni maalumu ya kuhakikisha kuwa kila aliyehusika katika ghasi
hizo anakamatwa na kukabili mkono wa sheria.
Akizungumzia
maendeleo ya Upelelezi wa Kesi ya Kuuawa kwa Askari Polisi CPL Said
Abdarahaman Juma aliyeuawa usiku wa kuamkia Alhamis wiki iliyopita,
Kamishna Mussa amesema Polisi wamefanikiwa kuwatia nguvuni watu sita kwa
kuhusika na mauaji ya askari huyo.
Amesema
hadi sasa Polisi inawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na
mauaji ya askari huyo ambapo watuhumiwa watatu walikamatwa mjini
Zanzibar na wengine watatu wamekamatwa mkoani Tanga.
Kamishna
Mussa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Abdallah Mohammed Said(35) wa
Mwanyanya, Joli Gasuli(20) wa Vuga, Bakari Juma Yusufu(22) wa Mwembe
Makumbi na Amour Rished(40) wa Bububu ambao walikamatwa mjini zanzibar siku ya kwanza lilipotokea tukio hilo.
Amewataja watuhumiwa wengine ambao wamekamatiwa Mkoani tanga na ambao tayari wamesharejeshwa Zanzibar kuwa ni Ali salum Seif(21) na Abubakari Haji Mbarouk(32) pamoja na mdogo wake Mohammed Haji Mbarouk(21) wote wakazi wa Ndagaa mkoa wa Kusini Unguja.
Kamishna
Mussa amesema Polisi bado inaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na wale
watakaobainika kuhusika na mauaji ya askari huyo watafikishwa
mahakamani.
Amesema
kwa ujumla tangu kukamatwa kwa viongozi hao hali ya usalama katika mji
wa Zanzibar imerejea upya na wananchi wameombwa kutoshabikia vitendo
vyovyote vile vitakavyoweza kupelekea uvynjifu wa amani.
Amewataka
Wazazi na walezi kutowaruhusu watoto wao kshiriki katika mikusanyiko na
kuwa chanzo cha fujo na kwamba kwa yeyote atakayekaidi agizo hilo
atashughulikiwa ipasavyo na mkono wa dola.


Yaani huyu mpuuzi alijificha ili wafuasi wake wavuruge amani, huyu Farid haitakii mema nchi yetu kuna haja sasa Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria ili wahindwe na adhma yao hawa watu wachache ya kuifanya nchi isikalike.
ReplyDeleteKwanza ukimwangalia tu unamuona ni mu OMAN halafu anataka kutuaribia nchi yetu, Si aende huko OMAN nchi nzuri na waislamu watupu?, Anangangania zanzibar kwanini? wanzanzir wote asili yao ni Bara, je anaongea lugha ghani ya huku bara? wanzanzibar ni wamakonde,wandengereko, wazaramu, wa nyamwezi je yy ni kabila gani?akijibu ndio aidai zanzibar kama hayumo ktk makabila ya bara bora aende zake OMAN
ReplyDeleteAnoy wa kwanza Naungana na wewe tena hizo hatua ZICHUKULIWE ZA KINIDHAMU ZIDI YA ZANZIBAR WAFUKUZWE KWENYE MUUNGANO KABISA KWA KUTOWEZA KUTEKELEZA MATAKWA YA MUUNGANO .
ReplyDeleteMFANO MAFUTA WANAYATAKA WAO-WAMEUNDA JESHI LAO LA KMKM WAKATI HAIRUHUSIWI,WANA BENDERA YAO WANA WIMBO WA TAIFA
KWA NINI HAWAFUKUZWI KWENYE UWANACHAMA WA MUUNGANO? KISHA IKABAKIA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZAMBIA KAMA NAIBU WAZIRI WA ELIMU WA TANZANIA ALIVOSEMA VIDEO YA JUU HAPO?
TUACHIWE TUPUMUWE...
Hata Ulimboka alijificha Mabwepande.
ReplyDeleteFungua macho yako vyema
ikiwa amejificha kwa makusudi kuchafua amani ya nchi itakuwa ni makosa makubwa
ReplyDeletelakini kabla ya kumuita mpuuzi anza kujiita wewe mdau hapo juu kuwa ni mpuuzi wa mwisho maana una uhakika gani na yaliyoandikwa?
una uhakika gani kama alijificha kwa makusudi ali alitekwa?
wananchi ni rahisi sana kushawishika na hivi vyombo vya habari maana wanaweza kutuhabarisha kuwa alijificha na kumbe alitekwa
suala la kutekwa sio jambo geni kwa hawa wana harakati maana hata kule kenya kuna mmoja alieuliwa na mwingine kutekwa je na hao ni wapuuzi?
Nyinyi watu weusi mna matatizo gani na waarabu, hawa ni raia wa tanzania kama wewe, kuwa mweupe sio tija kubaguliwa, nchi kama marekani isingepata rais mweusi kama wangefata sera kama zako wewe, manaake watu weusi asili yao Africa kwahiyo wanyimwe haki kule walipo. mwehu mkubwa, mbaguzi wa rangi, ndio baba yako wa taifa alivyokufundisha hivyo eenh
ReplyDelete