Waziri wa fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na maongezi ya uwekezaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard. (Standard Bank) hapa jijini Tokyo- Japan.
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na Makamu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedhana maendeleo ya uchumi, Mhe. Xavier – Luc Duval walipokuwa wakibadilishana mawazo kuhusu maendeleo ya nchi zao hizo mbili hapa Jijini – Japan – Tokyo.
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na wajumbe kutoka nchini Mauritius kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Maendeleo ya uchumi, Bw. Ali Mansoor akifuatiwa na Makamu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha na Maendeleo ya uchumi , Mhe. Xavier – Luc Duval walipokuwa wakielezana juu ya maendeleo kati ya nchi hizi mbili Jijini – Japan - Tokyo.
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa na Mwenyekiti wa Bodi ya uwekezaji Bw. Maurice Lam wa Mauritius wakibadilishana hati za mawasiliano Jijini Tokyo-Japan.
Gavana wa Benki Kuu Tanzania,Prof. Benno Ndullu akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bw. Servacius Likwilile wakifuatilia kikao cha Mawaziri wa Afrika Mashariki kilichoitishwa na katibu Mkuu wa Afrika Mashariki Jijini Japan – Tokyo.
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akimpokea Waziri wa fedha wa Kenya Bw. Robinson Githae tayari kwa kikao chao kinachohusu mambo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia ni waziri wa Fedha wa Rwanda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. We Michuzi we usharibu lugha ya Kiswahili bana sasa ahudhuLia ndio nini badala ya ahudhuRia.

    Mzee ruksa ametoka kwasema juzijuzi kuhusu kuharibu lugha ya Kiswahili lakini bado hamjasikia tu.

    Mngejua mnavyoniboaga mimi!

    ReplyDelete
  2. mdau mwenzangu wa mwanzo usimlaumu michuzi labda katika kabila lake hawana herufu ya R hawatumii huwa wameshazoea kutumia L. Kuna makabilia mengi tu lafdhi zao huwa wanashindwa kikiandika kiswahili na kukilsema so usimlaumu bure muache tu na pia kuna ubrother man wakimchwara mchwara watu kujidai kushokoki kimjini kufyatua maneno hapa na pale

    kiswahili bwana kiko zenji zanzibar unguja etc na siku hizi wanawafuata watu wa bara wanaharibikiwa kweli kweli kwa ujinga huu wa kukopii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...