KATIKA kuelekea sikuu za Krismasi na Mwaka mpya pilika pilika zimeongezeka katika mji wa Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla huku vibaka pia wakiendelea na udokozi na wizi wa vitu mbalimbali.

Katika kuthibitisha hilo juzi Tanzania Daima limeshuhudia mkazi wa kijiji cha Nshara, Machame wilayani Hai,ambaye jina lake halikupatikana mara moja amenusurika kuuawa kufuatia kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kumshambulia kwa silaha za jadi baada ya kuiba kitoto cha nguruwe maarufu kama "Kiti moto".

Tukio hilo la aina yake ambalo linaashiria maandalizi ya siku kuu hizo lilitokea juzi majira saa 5.30 asubuhi kijijini humo baada ya mkazi huyo kuonekana akiwa amembeba mnyamya huyo begani akiwa katika mfuko,maarufu kama Sandarusi mithili ya mzigo wa kawaida.

Akizungumzia tukio hilo,mkazi wa kijiji cha Nshara, Husein Mbaruku alisema mtu huyo alionekana akinyata katika banda la Nguruwe akiwa na mfuko wake akiamini kuwa hakuna mtu aliyemuona ingawa wenyeji nao walikuwa wakimvizia ili kuona anachotaka kufanya.

"Huyu bwana ni mwizi mzoefu katika eneo hili ,mara kwa mara wenyeji hapa wamekuwa wakilalamika kuibiwa nguruwe wao leo naona Arobaini yake imefika ,wananchi wamemkamata na ndio hivyo kama unavyoona kapigwa sana"alisema Mbaruku.

Alisema mtu huyo alifanikiwa kuiingia katika banda la nguruwe na kukikamata mmoja ya kitoto cha nguruwe ambacho wakati wa harakati ya kuingizwa katika mfuko huo kilipiga kelele ambazo ziliwashitua majirani wengine.

Kutokana na mazingira hayo,mtuhumiwa huyo alikuwa mjasiri na kukimbia nacho hivyo hivyo jambo lililosababisha baadhi ya wananchi kuanza kumfukuza kwa kasi ndipo alipoanguka eneo la mfoni ambapo wananchi walimjeruhi kwa silaha hizo ikiwamo mawe.

Katika hali isiyo ya kawaida huku mtuhumiwa huyo akivuja damu nyingine mmoja wa raia alitaka kumchoma kwa gurudumu la gari ndipo wananchi wenzake walipoingilia kati na kumuokoa mtuhumuwa huyo ambaye alipelekwa kituo cha polisi bomangombe.

Hadi kipindi hiki kinaondoka eneo la tukio majira ya saa saba mchana mtuhumiwa huyo alikuwa hajitambui kutokana na kipigo hicho kutoka kwa raia ambao baadaye walitawanyika baada ya kuhisi wamefanya mauaji.
Mkazi wa kijiji cha Nshara Machame akivuja damu baada ya kupokea kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali kufuatia wizi wa mtoto wa Nguruwe,tukio hilo lilitokea juzi wilayani Hai.Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii - Moshi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa


  1. Temingi imekataa babaangu, kitimoto katokea puani

    ReplyDelete
  2. Wachagga mnanifurahisha sana. Mtu akiiba kidogo anauawa lakini akiiba mabilioni anaitwa shujaa na kupewa shikamoo hata kama ni mtoto mdogo.

    ReplyDelete
  3. Kama wizi ni mila ya wachagga kwa nini walitaka kumuuwa mwenzao? Au kwa vile haibi vitu vikubwa? Kumbukeni roma haikujengwa kwa siku moja.

    ReplyDelete
  4. Aisee babangu mmemuonea huyo mangi. Kwani wisi si ni mila yetu?

    ReplyDelete
  5. Mungu awasamehe awajui walitendalo

    ReplyDelete
  6. Mekuu ,mbe aithee tufanye mpango ingine bwashee!

    ...(chalii ya nguruwe/ mtoto wa nguruwe) a.k.a kitoweo ya Krismasi imeota mbawa!

    ReplyDelete
  7. ...Mimi nachukua nguruwe toto moja tu napigwa, ningeiba pesa mbee?

    ReplyDelete
  8. Ahhh mwanawane, Krismasi 'dume' Mujini Moshi !!!

    ReplyDelete
  9. Mimi Mangi kitoweo cha Krismasi kimeniponza, si afathali masee ningekula kabechi?

    ReplyDelete
  10. Mekuu ngalasoni eeeh,

    Ninge iba kwa waswahilii ningekufwaa , sasa naiba kwa sisi mnaniuwaa?

    Kisusio ya Krisimasi nungetengeneza na ninie?, na maji ya kisimanii au damu ya panyaa?

    Naulisa mie Mekuu.

    ReplyDelete
  11. Nimeiba kitoto cha nguruwe kipondo kama hiki !!!

    je,ningeiba Bilioni 1 si nisingeiona Krisimasi ningekuwa tayari Kaburini?

    ReplyDelete
  12. Mimi naiba nguruwe mchanga mdogooo Wachagga wenzangu mnanipiga kama hamnijui kabisa hapa Kijijini Moshi!

    Je, ningeliiba huko Manzese Dare salaaam kwa Waswahili si ningeuliwa eeeh?

    ReplyDelete
  13. Ofisi ya Serikali za Mitaa ya Chama cha Siasa Kinachotawala Moshi, haya yanafanyika mpo?

    Itikadi yenu ni ya jazba na mapanga mkononi, mngechelewa mngemkuta jamaa Mangi akiwa amekatwa kawoshi masikio, mikono na viungo vingine kwa mapanga na visu !

    Kisa?, nguruwe mmoja mtoto!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...