Watanzania wenzangu,
Naomba niwape tahadhari ya usanii unaofanywa sasa hivi na gereji za kichina hasa ile maarufu ya Spring City iliyopo Sayansi karibu na Rose garden.
Nilipata taarifa ya usanii huu siku nyingi hadi toka kwa insurer wangu nikapuuzia lakini baada ya kupeleka gari yangu pale nikashuhudia mwenyewe kwa macho yangu. Hawa jamaa siku hizi badala ya kufanya replacement ya spare mpya huwa wana-repair halafu wanadakudanganya wamebadilisha vifaa vyote hivyo unawalipa gharama ya vifaa vipya badala ya vile repaired. Hivi karibuni nilipata mzinga gari nikaipeleka hapo gereji.
Niliporipoti kwa bima yangu walinishtua kwa kuniambia hapo hapafai siku hizi wateja wao wengi washalizwa.
Wakanishauri niwe makini kutembelea pale kila siku kukagua kama nataka kuwaachia wanitengenezee. Usanii wao wa kwanza ni kwamba wanapandisha gharama mara 2 ama 3 ya gharama halisi ya matengenezo. Mfano gharama halisi yaweza kuwa 3 mil. wao wanaweza kukupa invoice ya 6-7 mil.
Wakibanwa sana na bima, ndio wanafanya huo usanii wa repairing. Gari yangu iliharibika sehemu kubwa ya mbele na tutakubaliana wote na bima pia kuwa sehemu zote za body zilizoharibika zibadilishwe zifungwe body parts mpya. Baada ya siku 2, fundi wa pale niliyemtegesha alinishtua kuwa washaanza usanii. Nilipofika sikuamini, sehemu zote za gari wamenyoosha ndio wanazirudishia kabla ya kupiga puti na rangi.
Nilipomfuata na kukamripia business manager wao (huwa yupo pale reception muda wote) akaniomba msamaha tena kwa dharau na kuahidi kufunga vifaa vipya. Kesho nikakuta vifaa vyote vipya vimefungwa . Pia sehemu ya matengenezo nililipia mimi, hawakunikata hata senti ya kodi (nililipa VAT exclusive tu), hii yamaanisha hata ulipaji wao wa kodi unatia shaka.
Niliwahoji mafundi wengi wa pale wakasema almost gereji zote za kichina wanafanya usanii huo sasa hivi ila hapo ndio wamezidi sana na kila siku watu wanalizwa bila kujua.
Usanii wao umenikera sana hasa ikizingatiwa wao ni wageni nchini na walitokea kuaminika sana sasa wanatumia mianya ya mifumo mibovu ya usimamizi wa foreign investments nchini kufanya uhuni huo. Serikali iziangalia upya hizi gereji zote viwango vya huduma zao na ulipaji kodi.
Mzalendo
ndugu mwandish weldone wewe nimkombozi wa wanyonge lakini jamani kama wengi walilizwa Serikali iko wapi na kama insurence inafahamu nikwamba kuna ushahidi mkubwa kwakweli wachina wanaweza Afrika tu lakini western hawaingii sbb western wanawajali watu wao!Jeulize Afrika wachina wameshauwa wangapi kwa madawa fecky?Na sasa wanauza kuku wakilo 3 kwa madawa yao yakuku na wenye mahotel wanaona bora biashara yao inakwenda lakini waje wachunguzwe hao kuku wako na madhara gani!nimeona docmentary kwenye Tv vipi hao kuku wameleta madhara kenya kutokana na uzembe wa serikali zetu zisizokuwa na wasomi!
ReplyDeleteasante sana mdau. pole sana. mimi kila siku nawaambia watu kuwa hawa jamaa ni wanjanja wakiona serikali imelala au nayo ni corrupt wanafanya mambo. kule UDOM wanachakachua kama hawana roho nzuri. hivi karibuni a young QS alijaribu kuainisha mapungufu ya . tshs 200,000,0000 wakamuambia hata ukituma report tutalipwa tu. na kweli wamelipwa. sasa huyu young Qs ananiambia next time na yeye antashiriki ili apate mgao..hiyo ndio bongo. watanzania wachache tupatupate hasira na kufanya vitu vyetu wenyewe kwa uzuri na tuwabadilishe walio wengi. huo ndio wito wangu
ReplyDeleteNI kweli hawa jamaa wanafanya hivi vitu.mimi nilipelekwa gari yangu garage moja ya kichina iko buguruni pale sokoni ,malipo yakiwa 5.7 kuweka spare mpya na rangi as nilipata nayo ajali.mwisho wa siku gari ilikuwa ok for few days baada ya hapo yani hata hutamani kuiendesha maana kila kitu ni kibovu,.msifike kabisa pale,ningewapa jina bahati mbaya silikumubuki.
ReplyDeleteHizi issue wachina sasa hivi wanatuumiza sana.nilipeleka gari yangu garage moja iko pale buguruni sokoni ,jumla gharama ikawa 5.7 ya spare mupya na kupiga rangi.gari ilikuwa ok kwa muda wa wiki chache baada ya hapo mtu huwezi tamani hata kuendesha maana almost kila kitu kibovu nadhani hata waliongezea baadhi ya spare mbovu wakatoa zenye unafuu.jamani hawa watu kuweni nao makini,tujifunze kwa makosa ya waliopigwa kama sisi.Ningeandika jina la ile garage bahati mbaya silikumbuki.
ReplyDeleteNyie mlifikiri mchina anawapenda! hawamanjano kwanza wabaguzi saana, bora hata skin head anaweka vitu bayana, haya MIPINGO wezangu, tuwatoe baruti hawa manjano watatumaliza wajameni.
ReplyDeletetena hao wanaweka hata vitu vya wizi!!unaweza kushangaa ukapeleka gari lako uwekewe kitu kipya baada ya kuibiwa, wakakuwekea hicho hicho cha kwako maana huwa vibaka wanawapelekea!!!
ReplyDelete
ReplyDeleteMchina mchina tuu jamani hao watu sio wazuri kabisaa ni wabaguzi vibaya mno sio Malaysia, Singapore wala China na Hong Kong woote wana hakuna yenye afadhali ya mwenzake ni watu wabaya sanaaa
Na nyie mmezidi kudharau weusi wenzenu mchina mchina kama mwandishi uliambiwa lakini ulizidi kuuwaamini wachina na ukapeleka gari. nawemekufundisha.
ReplyDeleteNi kweli mdau hata mimi yalinikuta pale garage ya wachina Shekilango!
ReplyDeleteHawa jamaa ni wasanii sana ni bora tupeleke magarin yetu kwa wabongo wenzetu kisha tubanane nao gari linatoka BOMBA!
Ukiona hivyo ndugu yangu ni kuwa "wanakula nao". Kaa ufikiri nani wa kumvika paka kengele. Ichube
ReplyDeletepole sana ndugu lakini hata useme vipi hakuna kitakacho fanyika kazi bure ndugu yangu.
ReplyDeleteHaya wale wachina waliokamatwa wakichakachua umeme kiwandani kwao hapo mwenge njia ya ITV yalifikia wapi? si walitumia umemme buru miaka 5? hakuna cha mahakamani wala nini hatuambiwi kinachofanyika ila watu wangine wakifanya makosa wataonyesha hadi mahakamani ila wachina yanaishia hewani!! mfano pia wachina wa mikocheni viwanda nyumbani kwao yalishia wapi? wachina wa mabibo viwanda vya taka yako wapi? huwezi kuja kujua hatima yao ndo imetoka hiyo
mi sina hamu nazo garage za kichina kwa sasa.
ReplyDeleteKuna moja iko pale mwenge inaitwa David Auto (kama waenda hosp ya mama ngoma)ndio kimeo hadi nourmer. nilipeleka gari yangu ikifika wanakuandikia form inayoonyesha vifaa wanavyoreplace but hawabadilishi kitu wanapiga nyundo tu. na ukibadilishiwa utawekewa na vibovu. gari yangu iliumia mbele sehemu ndogo tu (invoice 5.7m)lkn baada ya kuichukua garage nililazimika kurudi mara kibao. gari imetoka garage rejeta imewekwa mbovu maji hayakai, shokap zinagonga,poor painting,hata kunyoosha hawakunyoosha kwa kiwango.ikawa nenda leo kesho unarudi garage, nenda leo kesho unarudi garage hadi nkachoka. Hapa najipanga nipate mkwaja nikamalizie baadhi ya matatizo sehemu nyingine tu. kwa kipindi ambacho nilikuwa nenda rudi nikabahatika kushuhudia malalamiko ya customers wengine wengi km mm nikaconclude jamaa ni vimeo, kumbe ni wachina wote sasa utaratibu wao kutuumiza. hivi kwani hizi garage hakuna mamlaka husika inayozisimamia?
Chinnese garages more than worse nowdays. Kuna ambao wapo pale Mwenge kama waenda kwa mama Ngoma hosp wanaitwa David Auto Garage walinifanyia kitu mbaya sana. Parts hawabadilishi, wakibadilisha wanaweka mbovu. nyundo kwa sana na kunyoosha sio kwa quality hata kdg, poor painting. Gari unachukua leo kesho umerudi tena garage nenda rudi mpaka nikachoka. unaambiwa gari tayari ukiendesha hata km sio mtaalam/fundi unaona mapungufu fasta. nilipewa gari shokap zinagonga, rejeta inavuja maji, rangi mbovu. nilikonfirm ukimeo wao pia baada ya kuona complains za wateja wengine. kuna haja serikali ianzishe mamlaka husika kuwasimamia hawa wachina wanatuumiza sana. its too much now.
ReplyDeleteYaliyoandikwa hapo juu ni kweli kabisa yaliyonikuta kuna gari ya ofisini ilipata ajali february 03,2015 na insurance walishughulikia kila kitu na waliambiwa watengeneze kwa kuandikiwa barua na watu wa insurance toka May 12,2015 lakini mpaka ninavyoandika gari haijatengenezwa na nikikuonyesha picha yake utasikitika sana sikutegemea hawa jamaa kunizungusha kiasi hiki.
ReplyDeleteWalinunua kipande cha mbele kilichooza kabisa ili wakiunge pale yaani kazi zao ni za ajabu sijawahi kuona na sijui kwanini hawa jamaa wanaachwa tu wakati wanatuliza vibaya