Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokelewa na viongozi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha kwa ajili ya kuongoza harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ukarabati wa kanisa hilo,iliyofanyika leo Mkoani humo.

===========     =========   =========
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amesisitizia tena kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni jambo la hatari kwa usalama wa nchi,wakati alipokuwa katika harambee ya kuchangia ukarabati wa kanisa la kilutheri usharika wa Akyeri Meru mkoani Arusha, Mh lowassa ameonya kuwa suala hilo lisiposhughulikiwa haraka litasababisha hali ya hatari.

''tunashuhudia maandamano katika mataifa ya ulaya vijana wakidai hali bora ya maisha pamoja na ajira.hali hiyo tusipoangalia inaweza kutokea hapa nchini kwetu.

huko nyuma niliwahi kusema kuwa makanisa, mashirika na watu binafsi wasaidie juhudi za serikali kutatua suala hilo''alisema Lowassa.

Lowassa ambaye katika harambee hiyo aliongozana na marafiki zake, ambapo yeye na familia yake pamoja na marafiki zake wamechangia kiasi cha shilingi millioni 33.2.

Zaidi ya shilingi millioni 160 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana katika harambee hiyo.

Kwa upande wake askofu Akyoo wa jimbo la Meru alimsifu Lowassa kwa uchapakazi wake popote alipokuwa.''Wakati ulipokuwa Waziri Mkuu ukimsaidia rais tulishuhudia uwezo wako mkubwa katika kufuatilia majukumu yako''alisema na kuongeza kuwa Lowassa ni mtu wa ibada

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa tatu kushoto) akiongozana na Askofu wa Kanisha hilo la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha,Askofu Akyoo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia muda mfupi kabla ya kuanza kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea ahadi ya mchango kutoka kwa mmoja wa wamini wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...