Mwenyekiti
wa
CCM mkoa wa Arusha,Onesmo Nangole (aliesimama) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mkutano wa
baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Arusha uliofanyika katika hotel ya golden rose,ambao ulikuwa ukizungumzia mambo mengi ikiwemo kuondoa
makundi yaliopo katika chama chao na kujipanga kikamilifu katika
kuimarisha chama chao.

Viongozi wa chama cha mapinduzi wakiimba wimbo wa chama kabla ya mkutano wa baraza la UVCCM mkoa wa Arusha.
wajumbe walikuwa makini kusikiliza nini haswa kinazungumzwa
Mmoja wa wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Arusha (Mounti Meru Hospital) akiwapa maelekezo viongozi wa Chama cha Mapinduzi pamoja na wanachama wa UVCCM waliotembelea hospitali hiyo kwa ajili ya kutoa misaada kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.wa kwanza kulia ni Katibu wa UVCCM mkoa wa Arusha Salus Kidima akifuatiwa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa Robson Meitinyiku
mjumbe wa baraza kuu la UVCCM taifa toka mkoa wa Arusha Benson Mollel wa kwanza kushoto akifuatiwa na mwenyekiti UVCCM mkoa Robson Meitinyiku wakitoa msaada kwa mtoto Frank aliyekuwa amelazwa kwenye hospitali ya mounti meru.
wajumbe wa UVCCM pia walikuwepo katika zoezi zima la kugawa misaada kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya mounti meru
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha,Robson Meitinyiku akimfariji mtoto mara baada ya kumkabidhi msaada.Picha na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii - Arusha.
Nimemmaindi huyu binti kulia kwa onesmo, details please.
ReplyDelete