Msanii
wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C, leo mchana amefika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais
Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika
jijini Dar-Es-Salaam chini ya uangalizi maalum.
Ray C
amefika Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve ambaye pia
amemshukuru Rais Kikwete kwa msaada huo mkubwa ambao umesaidia kurudisha hali
ya kawaida ya Ray C.
Rais
amempongeza Ray C kwa kukubali hali
yake ya kiafya na hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo
chini ya uangalizi maalum.
Rais
amemtaka mwanamuziki huyo kufuata masharti ya madaktari ili aweze kupona kabisa
na hatimaye kurudia hali yake ya mwanzo na kurejea katika shughuli zake za
kujitafutia kipato na maisha.
Kwa
vile Ray C bado yuko katika
matibabu, hatutaweka wazi sehemu anayotibiwa hadi atakapokuwa tayari kabisa
kurudi katika shughuli zake rasmi hivyo tunaomba jamii impe ushirikiano huo na
kuheshimu taratibu zake za matibabu ili hatimaye aweze kupona kikamilifu.
Imetolewa
na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-DSM
10 Desemba, 2012
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa kumsaidia matibabu,alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C wa kwanza kushoto ni Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu
mheshimiwa raisi wetu mtukufu anasaidia sana watu wengi ingawa wabongo awana shukrani. Hasa hasa vijana, inapendeza pale mzee wakaya anavyokuwa karibu na taifa lake la kesho
ReplyDeletei have nothing to add bt God has blessed you president
ReplyDeleteKikwete, I will cry when you leave our nation. You are a millenium President of Tanzania. No one in Africa is like you president. You care about the common people(poor) and listen to them. No one like you. I like you Kikwete, GOD Bless you President KIKWETE
ReplyDeleteYou are the best president ever Tanzania have ever had.
ReplyDeleteYou are the best Kikwete, we like you
ReplyDeleteYaaaaaaani! Dah! Prezidaaa JK hakika tutakukumbuka. Yaaaaani hadi machozi yananitoka. Ray C tuliyevumishiwa kuwa ndio basi tena umemsevu namna hii, hadi anaoneka mtu mbele ya watu. MUNGU AKUBARIKI JK. Wanaobeza mambo yako wale nyembe wafe! Wewe ni bonge la Prezidaaaaaaa!!!! JK Oye!!!!!! Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!
ReplyDeleteYaani sikutegemea utabend this low kusaidia watu wako. nalia! nalia!
Dear Ray C,
ReplyDeleteHii heshima uliyopata si ya kawaida. Tunajua ulikuwa unasumbuliwa na madawa ya kulevya. Usikonde mwanawane. Na hii inaonesha kuwa Rais wetu Kipenzi anafuatilia kila jambo nchini mwake. Na hili lako limemgusa si kidogo, kaisi cha kuweka hadharani kuwa amekusaidia. Na wewe na mama mmeonesha uungwana wa hali ya juu kuja kumshukuru. Angalia ulivyo mrembo. Kipaji bado unacho. Jiweke sawa na usimuangushe JK na sisi WaTZ wote kwa kuerejea ulikoookolewa. Plizzzzz tunangoja kali ya kiuno bila mfupa. Tumekumiss sana RAY C. We love U and we will always love JK for this
JK oyeeeee!
ReplyDeleteChambua, uliyesema kuwa JK atalipwa na Mungu, nakubali. Hivi nimekuta comments nane zote zinasema ukweli kwa moyo wa Rais wetu huyu ila wengi hawampi sifa zinazostahili. Yeye kwenda kutoammkono wa pole kwa wafiwa, kuzika na sasa kijana mabaye ilikuwa ndio anaondoka, inaonyesha Rais huyo yupo karibu na watu wake. Ndivyo inatakiwa kuwa Mzee wa kaya. Haya nimeona wengine wanakuablia kabisa kuwa kuendela miradi ya bara bara ni hatua kubwa kwa maendeleo..hivyo tutamkumbuka JK kwa mazuri mengi japo watu wachache wanakuwa wanakandianjuhudi zake. Shukrani JK, na Mola atakujazia kibaba chako
ReplyDeleteNimesisimkwa kwa kitendo hiki, tena msingetangaza hata tusingejua. MUNGU AKUBARIKI JK WANGU. Hata kama wengine wanakusema najua wakiumwa utakuwepo kuwasaidia. Wale waliomuombea mabaya RAY C bila kutoa msaada wowote Mungu amewaaibisha. Kwako RAY C TAFADHALI zingatia matibabu, masharti na usirudi huko kwakuwa sisi tunaokuja tunahuzunika sana kuona kiuno bila mfupa kinaangamia kwa mambo ambayo yanazuilika. Mungu akuponye
ReplyDeleteMungu akupe nini tena wewe Ray C. Ni kama unazaliwa upya. Ukiharibika tena ndio basi...
ReplyDeleteGood job President.. As a father I am sure he knows this can happen to any of our kids regardless of background.....Please this new epidemic ya mateja is real......And this is a disease like any other disease....I just hope she waasnt shooting ohhh lord na sindano za kushare..
ReplyDeleteMungu amnusuru na kumpa afya, na Mungu amzidishie huyo aliyemsaidia kuondoka na janga alilokuwa nalo. Hawa vijana, they always seem to be at war with their own dark demons, but some are lucky and recognise and accept their problems. Nakuomba ewe binti, ukipona uwasaidie jamaa wengine waepuke matatizo hayo. You should become a good-will ambassador or the president's special representative, a sort of a tsar
ReplyDeleteAlhamdulilah namshukuru mheshimiwa na wengine pia waliojaaliwa kuchangia kurudisha afya ya mwenzetu sisi ni soteni wamoja na kupotea hakuchagui leo yeye kesho mimi au wewe kama binadamu lazima tuwe na roho ya simanzi mwenzetu anapofikwa na matatizo na sio kumlaani au kumkimbia.Kesho RC atatu
ReplyDeletemika vizuri kama balozi mwakilishi ili kuweza kuwarudisha na wengine ambao bado wanataabika.Nashukuru pia kwa kupatikana hizi habari hapa maana nilipokua nazisoma ktk magazeti yale ya mitaani yenye kuvuma kwa taarifa za utata nilikua nachanganikiwa chumvi chumvi hata picha zao sijui walikua wanazitoa wapi.
Watu na bahati zao bwana. Langa na alihangaika mwenyewe. ia nasikia kuna wasanii wengine waliozama katika lindi la madawa. Na vijana wengine ambao sio wasanii ndio usipime.
ReplyDeleteMheshimiwa Raisi anastahili pongezi kwa kumsaidia huyu mwanadada, ila aangalie jinsi ya kuwasaidia na waathirika wengine wa haya madawa.
Tanzania, siku zote ni nchi yenye amani na upendo. Thanx JK for this may God be with you.
ReplyDeleteningekuwa raisi ningemwambia RC ataje waliomuuzia madawa hili wakamatwe
ReplyDeletembona jamani kama mmoja anasema kuna waliokuwa wanamwombea mabaya RC ,nani alimwombea sasa tutajanane hapa hapa au unataka RC akujue kama wewe ndio wa karibu kwake tutajuaje kama sio wewe uliyemwombea mabaya
ReplyDeletenaomba address ya huyo dadake>..maana du kwenye ukweli uongo hujitenga nimemnanihi kwelikweli..
ReplyDeleteSafi Sana na nimfano bora kwa Viongozi bora.
ReplyDeleteIla jambo moja, Ray C ni maarufu sana na huwenda kuna urafiki wa karibu na raisi wetu.Maoni yangu nikuwa kama ni tatizo la madawa ya kulevya,kuna watanzania wengi wenye hayo matatizo, nenda magomeni na sehemu nyingine,Je nao watapata huu msaada?
Jambo zuri ni la Ray C kuanzisha kampeni ya kuwasaidia wengine na Raisi wetu hawe ndio muhamasishaji.
Mdau,California
Ni vizuri JK kusaidia, Nasifu sana juhudi za rais ambazo zinaonyesha anajali maisha ya watanzania. Ningeomba ombi moja kwako mheshimiwa rais; Huduma ya afya ni ghali sana kwa watanzania kuweza kumudu, kama rais wetu tumia nguvu zako mheshimiwa rais wetu ili huduma ziende chini ili wananchi waweze kuishi, watanzania tu masikini sana na wengi hawana kazi hivyo kumudu gharama hata za hospitali za serikali zipo juu sana, wananchi wengi hawaziwezi.
ReplyDelete
ReplyDeleteTHANK YOU MR. PRESIDENT, THANK YOU STATE HOUSE.
BINADAMU ANAPOOMBA MSAADA NI WAJIBU KUMSAIDIA.
TUKO PAMOJA MOKONZI JK.
Kikwete sio mtu mbaya.Ana mapungufu yake,na kikwete hakutakiwa kuwa kiongozi wa nchi sisemi hivi,kumvua heshima laa hasha nikutokana na huruma yake na ubinadamu alionao.
ReplyDeleteKwa namna nyingine wajanja wanatumia mgongo wake kujinufaisha ndo maana rushwa haishi.
Pamoja na hayo amejitahidi kama kiongozi.na kwa hili ni swala la kumpongeza kwa kumsaidia huyu dada.
NAPENDA KUTOA RAI YANGU KWA RAY C KWAMBA.SASA HIVI ATAKUWA ANAJUA NANI MWEMA KWAKWE NA NANI RAFIKI.HAIWEZEKANI MSAANII MKUBWA KAMA YEYE KUKOSA USHIRIKIANO KUTOKA KWA WENZAKE TENA WENYE UWEZO.
RAYC USIJALI MAMA KILA MTU ANAPITA MAMBO KATIKA MAISHA.HAKUNA ALIYE SALAMA.MWENYEZI MUNGU AMEKUWEZESHA UMEPATA NAFASI YA PILI KUISHI KAMA BINADAMU,ISHIKE KIKAMILIFU NA KUWAHESHIMU WALE WALIOKUWA NAWE KIPINDI KIGUMU.
NAKUOMBA ANZA UPYA MAISHA,UPYA.ACHANA NA WANAUME WAKISHENZI,IKIWEZEKANA NENDA UOLEWE KABISA.
MIMI NAKUPENDA LAKNI NDO HIVYO SIWEZI KUKUPATA.Sjunearusha@yahoo.com
UTU NA UTANZANIA KWANZA.JK OYEE.
ahsante MISUPU.
Hongera RAis kwa kumsaidia RAY C,lakini hiyo naona haitoshi,vijana na watu wenye tatizo hili la kutumia dawa za kulevya wako wengi sana mtaani.
ReplyDeleteMimi napendekeza wewe ukiwa kama RAIS ingefaa kama ungeanzisha kituo cha kuwatibia wahanga wa tatizo hili
Father of the nation,big up Jk you are the man.
ReplyDeleteMh. Kikwete ubinadamu ndo huo, kuna mengi ya kuijifunza kukoka kwako. Tumezoea kwenye blogu watu wakiponda hta kama mtu atafanya mema kiasi gani lakini kwa hili ulilofanya ni la kipekee naona watu wote wankusifia. Big up! Tanzania itajengwa na watu wenye mioyo kama yako.
ReplyDeleteBuguruni watumia dawa za kulevya wako wengi sanaaa pale, kama Kikwete ana huruma kwanini hakuwasaidia hawa wa buguruni???? Why Ray C?
ReplyDeleteTunamtakia Ray C kila la heri na amalize matibabu yake salama. Pia tunamuomba awe balozi wa vijana wengine wenye matatizo kama yake.
ReplyDeleteThanx mr. kikwete, pse do the same for the rest of the tejas there are so many of them even in tabora songea, bkb, arsha, mtwara
ReplyDeletewaite wote ikulu uone kama patatosha!
It good work Mr. President...
ReplyDeleteMy advice is that we need to deep down to the source. We can't cut branches while roots are still there.....
Thanks
Safi sana JK. Sasa tunaomba tutolee na Lulu.
ReplyDeleteNi afadhali kugharamia matibabu kuliko kuhudhuria mazishi
ReplyDeleteTunamshukuru President kwa hilo, lakini tunakuomba muheshimiwa utusaidie kuumaliza mtandao huu wa madawa ya kulevya.
ReplyDeleteKuna Vijana wengi sana ambao wanataabika huku mitaani hawana misaada yeyote zaidi ya kupora vitu vya watu na kuuza hata kama nivyathamani WAMEFIKIA HATUA YA KUVUNJA MAGARI NA KUIIBA ili mradi wapate PESA YA kununua madawa hayo. Tunaomba muheshimiwa, utusaidie kutuondolea balaa hili, tunafahamu si rahisi wote waje kwako kuomba msaada wa tiba nawe sijui kama utaweza!!! LAKINI, KUNA NJIA MOJA TU, NAYO NIKUSAFISHA MTANDAO HUU KWA GHARAMA YEYOTE, KINGA NI BORA KULIKO TIBA.
Kwanza kabisa tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kitendo alichokifanya cha kumsaidia matibabu kipenzi cha wengi Ray C. Mungu akubariki Mheshimiwa Rais. Isipokuwa Ikulu hapakuwa mahali sahihi pa kuingia kwa kila anayepata msaada kutoka kwa Rais, sababu Ikulu ni mahali Patakatifu. Ray C angeweza kwenda kwenye vyombo vya habari kutoa shukrani zake kwa Rais bila kwenda Ikulu.
ReplyDeleteMheshimiwa Rais, ningependekeza kwamba, umkabidhi Ray C kwenye vyombo vya Usalama asaidie Serikali namna alivyokuwa anapata dawa za kulevya ili njia hiyo isaidie kupunguza ongezeko la matumizi ya madawa ya kulevya.
Elbafra Dito, Dar es Salaam. Tanzania.
Napenda kutoa shukrani za kipekee kwa Rais wetu kipenzi kwa msaada alioutoa kwa dada yetu Ray C. Ama kwa hakika ni ushupavu wa hali ya juu aliouonyesha na pia jamii isiwe na wasi wasi kwa Mkuu wetu huyu wa nchi kwani ni msikilizaji na mtekelezaji wa haja kwa wananchi wake. Kuhusu kuhudumia na vijana wengine ambao wamezama kwenye janga hili la madawa ya kulevya ameruhusu viwekwe vituo maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wale walioathirika tunachotakiwa kama wanajamii ni sisi kutilia mkazo maana kwa kila familia lazima kutakuwa na mtoto japo mmoja aliyepotea njia hivyo ni vizuri wahusika wafuatilie kwa karibu hizo fursa ili vijana wao walioathirika waweze kutibiwa. Maana kwa kila kituo kinatakiwa kitoe takwimu sahihi ili waweze kupatiwa msaada kupitia kwenye serikali zao za mitaa. Raisi wetu kwa kupitia kitengo maalumu anapeleka misaada huko ila sasa wale watendaji hawatoi ushirikiano mzuri na pia wote wenye watoto waathirika wangepewa ushuhuda kama mama Ray C. Amehakikisha amesimama kidete mpaka mwanawe karudi kwenye mstari, Nakupa Big up mama Ray C Mungu akupe nguvu hizo mpaka ujuwe mwisho wa binti yako.
ReplyDeleteKWAKO RAY C,
NAFASI HII NI YA PILI AMBAYO MUNGU AMEKUPA SASA ITUMIE VIZURI NA PINDIPO UTAPOPONA NAOMBA UWE BALOZI WA NCHI YETU KWENYE MASUALA YA MADAWA YA KULEVYA. UTAPATA CHANGAMOTO NYINGI SANA LAKINI MUNGU ATAKUPA UWEZO NA NGUVU ZA KUSHINDA MAJARIBU NA UTARUDI SALAMA USALIMINI ULINGONI. WEWE UWE UNAWAKEMEA WALE WATAKAOJARIBU KUKURUDISHA TENA HUKO ULIKOKUWA MUNGU ATAKUEPUSHA ZAIDI NA UTAFAULU MTIHANI HUU ULIOPEWA.
KWETU SISI
Kabla hujafa hujaumbika. Kama huna mtoto basi atakuwa wa nduguyo au wa jirani yako au kaka/dada yako hivyo mtoto wa mwenzio anapokuwa kateleza, muombee arudi kwenye mstari. Sivyema kumbeza kwani dunia ni duara huwa inazunguka, leo kwake na huenda ikawa kesho kwako. Tuombeane dua tuishi kwa upendo wa hali ya juu kwani MWANA WA MWENZIO NI WAKO.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE WOTE. asante. Mama Abbas, Magomeni, Lango la Jiji.
Kiukweli nimesisimka na nimelengwa na machozi baada ya kuona kazi nzuri na yenye upendo iliyofanywa na mheshimiwa Raisi Jaka Mrosho Kikwete. Hili ni jambo jema sana haswa ukinzingatia wewe ndo baba wa Tanzania kwa wakati huu hivyo unapaswa kuangalia wanao kwa jicho la kipekee kabisa kama ulivyo amua kufanya kwa huyu dada yetu mpendwa ambaye alikwisha potea kwenye ulimwengu wa NURU. Ahsante sana Raisi wetu Mungu akuzidishie kila ulipopungukiwa. Mungu akuzidishie amani, upendo, ucheshi na hata busara katika kipindi hiki unachoelekea kumalizia ngwe yako ya URAISI, Ningetamani sana uendelee lakini maadili tuliyojiwekea hayaruhusu na ndio nguzo kubwa ya kutotutumbukiza kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe hakika wewe ni MTUMISHI mwema usiyejali rangi wala kabila wala dini. Allah akubariki
ReplyDeleteMdau
Ray C taja waliokuuzia kuonesha kweli upo siriazzzz....na unawatakia mema vijana wengine wanao angamia...langa kapona ila mbona hajataja waliomuuzia?..so yaleyale tuu...kampeni ya madawa ya kulevya kwa kuhamasisha vijana wasitumie huku huyo alieacha hataki kutaja walio kwenye chain ya kuuza ni unafiki!!
ReplyDeleteshukran kwa JK kwa kusaidia jamii
Ray C mdau hapo juu katoa ushauri mzuri sana.Achana na hao sijui akina MACHO MUNGU Sijui BARABARA MACHO sijui MZIGO MACHO(Kwa kidhungu inaleta maana)...Hawana future hao.Watakuharibu tu.Wamebaki kuiba POWER WINDOW ili wabwie SEMBE.
ReplyDeleteMimi ni kijana mcha mungu sana na nina kipato chakawaida.Sio maskini wala tajiri ila ninachojivunia ni MAADILI MEMA...Sio lazima uolewe na Mtu maaufu.Nitafute niko serious nakupenda kwa dhati tangu enzi ukiimba nyimbo ile ukiwa japani(UKO WAPI NIKUFUATE)...Na kila nilipokua nakuona katika video zako naishia kusononeka tu.Kukufuata siwezi ila Naamini kuna siku M.Mungu atatuunganisha tu hata UZEENI...Nakusubiri REHEMA.
cibmannamdun@yahoo.com
Pole RC Mimi nakushauri kuwa ukipona vizuri, achana na kazi ya muzic kwa sababu kwa sasa umri wako ni mkubwa na game la muziki linaushindani mkubwa sana. kazi nzuri unayoweza kufanya ni kuwa PR yaani afisa uhusiano au afisa habari hasa kwenye NGO zinazopambana na madawa ya kulevya, unyanyapaa n.k. hii ni nzuri kwako kwa kuwa pia uliwahii kuwa mtangazaji, na uko presentable mbele ya hadhara na jamii kwa ujumla ona unavyopendeza kwa mavazi hayo sio zile za vitovu njee kwa umri wako kwa sasa.
ReplyDeletenajua NGOs nyingi watakukubali bila ya usaili, maana unalipa kwa sasa.
MWATANGE MUWINA MUNYA KILUNGA/KAYE, NYONGISE NDEMUYAGO ISAYO SINDIPILUKILA NG'OO.
I m speechless....I Love it My President. God Bless u, and God Bless Tanzania.
ReplyDeleteAhsante sana Raisi JK kwa ubinaadamu mkubwa kwetu!
ReplyDeleteJe, hao walikuwa wanampimia hayo madawa ya kulevya mbona hatukuwaona kutoa chochote?
Jamani tukio hili la mkasa wa RC liwe ni mwamko na fundisho kwetu Watanzania licha ya Kumshukuru Raisi wetu Mpendwa, tuangalie ni jinsi gani MADAWA YA KULEVYA HAYAKUBALIKI, TUSEME HAPANA KWA MADAWA YA KULEVYA!
Hongera sana Raisi Jakaya Kikwete,
ReplyDeleteLohhh RC jamani mzuri, mnaona sasa uzuri wake unarejea tena baada ya kupata nafuu za matumizi ya madawa ya kulevya.
Raisi JK hongera sana na umetusaidia kuirudisha nuru ya uzuri wa RC ambayo sasa inerejea tena!
mi sijapenda hii kitu alofanya JK
ReplyDeleteutasaidiaje watu wanaojitakia wenyewe bana wkati kuna wanaokufa kwa kukosa matibabu????? huyu mtu mzima kabisa hajui kwamba madawa ni sumu???
Ngojea mtoto wako awe teja ndo utajua na kuea humble ....
DeleteTunakushukuru saaana raisi wetu mpendwa Jakaya Kikwete, hatuna cha kukulipa ila mwenyezi mungu atakuzidishia, Ray C sote tunakupenda na tumefarijika kukuona ktk hali hii, m/mungu atakusaidia sote tunakuombea dua mtu wetu , tupo pamoja sana..
ReplyDeleteRay C she is talented, Ray C ni star, Ray among the legend muziki wa kizazi kipya. Sisi ni binadamu mwenyezi Mungu kila mtu amemuandikia nini kitamtokea mbele ya maisha yake. Ila hakuna anayejua muda gani.
ReplyDeleteRais Kikwete siyo kwamba hapendi kusaidia wananchi wake hapana anasaidia sana, ila akisema aanze kutangaza hawataisha. Ila ni mwenye huruma aliona binti wa watu ni mdogo na kipaji anacho ila mambo ya dunia. Basi kama binafsi kuchukua jukumu hilo la kumtibia basi kushkuru Mungu.
Ray C bado ni msichana ambaye anaudai muziki wa kizazi hela nyingi sana. Sasa arekodi nyimbo za kutosha nina imani Mungu yupo nasi sote na atafanikiwa zaidi hata ya zamani.
Naomba watanzania tusihukumu na tuendele kuelemishana maana hujui wewe kesho utaangukia wapi.
Mungu Mbariki Ray C, Mungu Mbariki J. Kikwete, Mungu wabariki Watanzania wote. Ameen
UUNGWANA NI VITENDO!
ReplyDeleteTunaweza kumpima Mhe. Raisi wetu kwa mambo kama hili suala la Ray C, mara zote Mhe. JK amekuwa mbele kuhakikisha mwelekeo wa nchi unaimarika, ISIPOKUWA NI DHAHIRI UNAPOKUWA MSIMAMIZI MKUU HUWEZI KUFANYA KILA KITU MWENYEWE, UNALAZIMIKA KUMPA MSAIDIZI MWAMINIFU MAJUKUMU KWA NIABA YAKO.
SASA KIBAYA ZAIDI INAPOKIFIKA NAFASI HII YA KUAMINIWA NDIO TUNAKUTA BAADHI YA VIONGOZI WASIO WAADILIFU WANAHARIBU!
HIKI NDIO KITU KINAMPONZA RAISI WETU MUUNGWANA JK, !!!
LAITI INGELIKUWA KILA KITU ANAFANYA RAISI JK YEYE MWENYEWE, NADHANI KUSINGEKUWEPO NA WA KUMLAUMU, NA ENDAPO ATATOKEA WA KUMLAUMU KWA NINI TUSIMWONE MTU HUYO SIO MWENZETU?
Inshallah ,
ReplyDeleteMwenyezi Mungu atakurahisishia Raisi JK kwa kukupunguzia mitihani na kuwashinda maadui zako!
Ahsante sana Kiongozi wetu Raisi Mhe. JK kwa hisani yako kwetu sisi wananchi!
ReplyDeleteUmemfanyia Ray C lakini hisani yako imetufikia Watanzania wote!
TUCHUKUE NAFASI HII TUYAANGALIE MADAWA YA KULEVYA KWA PANDE 2 ZA SARAFU:
WAKATI ATHARI IKIWEPO:
-Bibie Ray C alionekana kama bata aliyenyeshewa na mvua.
-Bibie Ray C mboni za macho yake zilikuwa kama mbuzi aliyekoswa koswa na radi.
-Bibie Ray C alikuwa amezeeka ghafla akiwa na umri wa miaka 29 akaonekana kama ana miaka 92!
BAADA YA KUKOMBOLEWA KTK MADAWA:
-Bibie Ray C anarudi na nuru yake.
-Bibie Ray C mboni za macho yake zinarejea kung'ara tena.
-Bibie Ray C amerudi mbichiiii !!!
AHHH TUYACHUKIE MADAWA YA KULEVYA YALITAKA KUTUHARIBIA MREMBO WETU!
DAH MTOTO MZURI JAMANI RAY C !!!
Mwenyezi Mungu akubariki sana Mheshimiwa Rais kwa kumsaidia dada yetu.
ReplyDeleteKwa Ray C pia Mwenyezi Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu, ili uweze kukipita salama. Mama Ray C pia Mweneyzi Mungu akubariki na kukupa nguvu zaidi maana hukuacha kuhangaika kutafuta msaada kwa mwanao, pia usiache pia kumweka mbali na marafiki wasio wazuri. Kwani naamini katika kipindi hiki, hao waliokua wanajiita ni marafiki zake, watakua hawaonekani kumpa Ray C msaada wa hali na mali... God Bless you all.
Kwenye matatizo ndio utamjua nani rafiki na nani mnafiki!
ReplyDeleteUnakuta mtu unamwita rafiki akipita kuisikia kuwa hali yako iko vinaya ama pana yaliyo kukuta anakuja akionana na wewe anakuwa kijino pembe akiona kuwa umekwama.
Mungu si Athumani, mfikwa hupata muamala na akakomboka na masahibu yaliyomkuta kitu ambacho watu wanafiki daima hawaelewi ya kuwa kama Mungu ndiye aliyeleta hali fulani na Mwenyezi ndiye mponyaji wa shida zote!
Mhe.asante kwa kumsaidia RAY C wetu.Binafsi nampenda sana,nilipomwona gazetini nilila sana ,hatimaye nikaona kuwa umemsaidia,nikalia tena kwa furaha.Endelea na moyo huo,kwa mungu una fungu lako.KWA HILI I LOVE U MR, PRESIDENT LONG LIVE.
ReplyDeleteTHANKS