Msanii wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C, leo mchana amefika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini Dar-Es-Salaam chini ya uangalizi maalum.
Ray C amefika Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve ambaye pia amemshukuru Rais Kikwete kwa msaada huo mkubwa ambao umesaidia kurudisha hali ya kawaida ya Ray C.
Rais amempongeza Ray C kwa kukubali hali yake ya kiafya na hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo chini ya uangalizi maalum.
Rais amemtaka mwanamuziki huyo kufuata masharti ya madaktari ili aweze kupona kabisa na hatimaye kurudia hali yake ya mwanzo na kurejea katika shughuli zake za kujitafutia kipato na maisha.
Kwa vile Ray C bado yuko katika matibabu, hatutaweka wazi sehemu anayotibiwa hadi atakapokuwa tayari kabisa kurudi katika shughuli zake rasmi hivyo tunaomba jamii impe ushirikiano huo na kuheshimu taratibu zake za matibabu ili hatimaye aweze kupona kikamilifu.

Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-DSM
10 Desemba, 2012
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa kumsaidia matibabu,alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C wa kwanza kushoto ni Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 52 mpaka sasa

  1. mheshimiwa raisi wetu mtukufu anasaidia sana watu wengi ingawa wabongo awana shukrani. Hasa hasa vijana, inapendeza pale mzee wakaya anavyokuwa karibu na taifa lake la kesho

    ReplyDelete
  2. i have nothing to add bt God has blessed you president

    ReplyDelete
  3. Kikwete, I will cry when you leave our nation. You are a millenium President of Tanzania. No one in Africa is like you president. You care about the common people(poor) and listen to them. No one like you. I like you Kikwete, GOD Bless you President KIKWETE

    ReplyDelete
  4. You are the best president ever Tanzania have ever had.

    ReplyDelete
  5. You are the best Kikwete, we like you

    ReplyDelete
  6. Yaaaaaaani! Dah! Prezidaaa JK hakika tutakukumbuka. Yaaaaani hadi machozi yananitoka. Ray C tuliyevumishiwa kuwa ndio basi tena umemsevu namna hii, hadi anaoneka mtu mbele ya watu. MUNGU AKUBARIKI JK. Wanaobeza mambo yako wale nyembe wafe! Wewe ni bonge la Prezidaaaaaaa!!!! JK Oye!!!!!! Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!
    Yaani sikutegemea utabend this low kusaidia watu wako. nalia! nalia!

    ReplyDelete
  7. Dear Ray C,
    Hii heshima uliyopata si ya kawaida. Tunajua ulikuwa unasumbuliwa na madawa ya kulevya. Usikonde mwanawane. Na hii inaonesha kuwa Rais wetu Kipenzi anafuatilia kila jambo nchini mwake. Na hili lako limemgusa si kidogo, kaisi cha kuweka hadharani kuwa amekusaidia. Na wewe na mama mmeonesha uungwana wa hali ya juu kuja kumshukuru. Angalia ulivyo mrembo. Kipaji bado unacho. Jiweke sawa na usimuangushe JK na sisi WaTZ wote kwa kuerejea ulikoookolewa. Plizzzzz tunangoja kali ya kiuno bila mfupa. Tumekumiss sana RAY C. We love U and we will always love JK for this

    ReplyDelete
  8. JK oyeeeee!

    ReplyDelete
  9. Chambua, uliyesema kuwa JK atalipwa na Mungu, nakubali. Hivi nimekuta comments nane zote zinasema ukweli kwa moyo wa Rais wetu huyu ila wengi hawampi sifa zinazostahili. Yeye kwenda kutoammkono wa pole kwa wafiwa, kuzika na sasa kijana mabaye ilikuwa ndio anaondoka, inaonyesha Rais huyo yupo karibu na watu wake. Ndivyo inatakiwa kuwa Mzee wa kaya. Haya nimeona wengine wanakuablia kabisa kuwa kuendela miradi ya bara bara ni hatua kubwa kwa maendeleo..hivyo tutamkumbuka JK kwa mazuri mengi japo watu wachache wanakuwa wanakandianjuhudi zake. Shukrani JK, na Mola atakujazia kibaba chako

    ReplyDelete
  10. Nimesisimkwa kwa kitendo hiki, tena msingetangaza hata tusingejua. MUNGU AKUBARIKI JK WANGU. Hata kama wengine wanakusema najua wakiumwa utakuwepo kuwasaidia. Wale waliomuombea mabaya RAY C bila kutoa msaada wowote Mungu amewaaibisha. Kwako RAY C TAFADHALI zingatia matibabu, masharti na usirudi huko kwakuwa sisi tunaokuja tunahuzunika sana kuona kiuno bila mfupa kinaangamia kwa mambo ambayo yanazuilika. Mungu akuponye

    ReplyDelete
  11. Mungu akupe nini tena wewe Ray C. Ni kama unazaliwa upya. Ukiharibika tena ndio basi...

    ReplyDelete
  12. Good job President.. As a father I am sure he knows this can happen to any of our kids regardless of background.....Please this new epidemic ya mateja is real......And this is a disease like any other disease....I just hope she waasnt shooting ohhh lord na sindano za kushare..

    ReplyDelete
  13. Mungu amnusuru na kumpa afya, na Mungu amzidishie huyo aliyemsaidia kuondoka na janga alilokuwa nalo. Hawa vijana, they always seem to be at war with their own dark demons, but some are lucky and recognise and accept their problems. Nakuomba ewe binti, ukipona uwasaidie jamaa wengine waepuke matatizo hayo. You should become a good-will ambassador or the president's special representative, a sort of a tsar

    ReplyDelete
  14. Alhamdulilah namshukuru mheshimiwa na wengine pia waliojaaliwa kuchangia kurudisha afya ya mwenzetu sisi ni soteni wamoja na kupotea hakuchagui leo yeye kesho mimi au wewe kama binadamu lazima tuwe na roho ya simanzi mwenzetu anapofikwa na matatizo na sio kumlaani au kumkimbia.Kesho RC atatu
    mika vizuri kama balozi mwakilishi ili kuweza kuwarudisha na wengine ambao bado wanataabika.Nashukuru pia kwa kupatikana hizi habari hapa maana nilipokua nazisoma ktk magazeti yale ya mitaani yenye kuvuma kwa taarifa za utata nilikua nachanganikiwa chumvi chumvi hata picha zao sijui walikua wanazitoa wapi.

    ReplyDelete
  15. Watu na bahati zao bwana. Langa na alihangaika mwenyewe. ia nasikia kuna wasanii wengine waliozama katika lindi la madawa. Na vijana wengine ambao sio wasanii ndio usipime.

    Mheshimiwa Raisi anastahili pongezi kwa kumsaidia huyu mwanadada, ila aangalie jinsi ya kuwasaidia na waathirika wengine wa haya madawa.

    ReplyDelete
  16. Tanzania, siku zote ni nchi yenye amani na upendo. Thanx JK for this may God be with you.

    ReplyDelete
  17. ningekuwa raisi ningemwambia RC ataje waliomuuzia madawa hili wakamatwe

    ReplyDelete
  18. mbona jamani kama mmoja anasema kuna waliokuwa wanamwombea mabaya RC ,nani alimwombea sasa tutajanane hapa hapa au unataka RC akujue kama wewe ndio wa karibu kwake tutajuaje kama sio wewe uliyemwombea mabaya

    ReplyDelete
  19. naomba address ya huyo dadake>..maana du kwenye ukweli uongo hujitenga nimemnanihi kwelikweli..

    ReplyDelete
  20. Safi Sana na nimfano bora kwa Viongozi bora.

    Ila jambo moja, Ray C ni maarufu sana na huwenda kuna urafiki wa karibu na raisi wetu.Maoni yangu nikuwa kama ni tatizo la madawa ya kulevya,kuna watanzania wengi wenye hayo matatizo, nenda magomeni na sehemu nyingine,Je nao watapata huu msaada?

    Jambo zuri ni la Ray C kuanzisha kampeni ya kuwasaidia wengine na Raisi wetu hawe ndio muhamasishaji.

    Mdau,California

    ReplyDelete
  21. Ni vizuri JK kusaidia, Nasifu sana juhudi za rais ambazo zinaonyesha anajali maisha ya watanzania. Ningeomba ombi moja kwako mheshimiwa rais; Huduma ya afya ni ghali sana kwa watanzania kuweza kumudu, kama rais wetu tumia nguvu zako mheshimiwa rais wetu ili huduma ziende chini ili wananchi waweze kuishi, watanzania tu masikini sana na wengi hawana kazi hivyo kumudu gharama hata za hospitali za serikali zipo juu sana, wananchi wengi hawaziwezi.

    ReplyDelete

  22. THANK YOU MR. PRESIDENT, THANK YOU STATE HOUSE.

    BINADAMU ANAPOOMBA MSAADA NI WAJIBU KUMSAIDIA.
    TUKO PAMOJA MOKONZI JK.

    ReplyDelete
  23. Kikwete sio mtu mbaya.Ana mapungufu yake,na kikwete hakutakiwa kuwa kiongozi wa nchi sisemi hivi,kumvua heshima laa hasha nikutokana na huruma yake na ubinadamu alionao.
    Kwa namna nyingine wajanja wanatumia mgongo wake kujinufaisha ndo maana rushwa haishi.
    Pamoja na hayo amejitahidi kama kiongozi.na kwa hili ni swala la kumpongeza kwa kumsaidia huyu dada.


    NAPENDA KUTOA RAI YANGU KWA RAY C KWAMBA.SASA HIVI ATAKUWA ANAJUA NANI MWEMA KWAKWE NA NANI RAFIKI.HAIWEZEKANI MSAANII MKUBWA KAMA YEYE KUKOSA USHIRIKIANO KUTOKA KWA WENZAKE TENA WENYE UWEZO.
    RAYC USIJALI MAMA KILA MTU ANAPITA MAMBO KATIKA MAISHA.HAKUNA ALIYE SALAMA.MWENYEZI MUNGU AMEKUWEZESHA UMEPATA NAFASI YA PILI KUISHI KAMA BINADAMU,ISHIKE KIKAMILIFU NA KUWAHESHIMU WALE WALIOKUWA NAWE KIPINDI KIGUMU.
    NAKUOMBA ANZA UPYA MAISHA,UPYA.ACHANA NA WANAUME WAKISHENZI,IKIWEZEKANA NENDA UOLEWE KABISA.
    MIMI NAKUPENDA LAKNI NDO HIVYO SIWEZI KUKUPATA.Sjunearusha@yahoo.com

    UTU NA UTANZANIA KWANZA.JK OYEE.
    ahsante MISUPU.

    ReplyDelete
  24. Hongera RAis kwa kumsaidia RAY C,lakini hiyo naona haitoshi,vijana na watu wenye tatizo hili la kutumia dawa za kulevya wako wengi sana mtaani.

    Mimi napendekeza wewe ukiwa kama RAIS ingefaa kama ungeanzisha kituo cha kuwatibia wahanga wa tatizo hili

    ReplyDelete
  25. Father of the nation,big up Jk you are the man.

    ReplyDelete
  26. Mh. Kikwete ubinadamu ndo huo, kuna mengi ya kuijifunza kukoka kwako. Tumezoea kwenye blogu watu wakiponda hta kama mtu atafanya mema kiasi gani lakini kwa hili ulilofanya ni la kipekee naona watu wote wankusifia. Big up! Tanzania itajengwa na watu wenye mioyo kama yako.

    ReplyDelete
  27. Buguruni watumia dawa za kulevya wako wengi sanaaa pale, kama Kikwete ana huruma kwanini hakuwasaidia hawa wa buguruni???? Why Ray C?

    ReplyDelete
  28. Tunamtakia Ray C kila la heri na amalize matibabu yake salama. Pia tunamuomba awe balozi wa vijana wengine wenye matatizo kama yake.

    ReplyDelete
  29. Thanx mr. kikwete, pse do the same for the rest of the tejas there are so many of them even in tabora songea, bkb, arsha, mtwara
    waite wote ikulu uone kama patatosha!

    ReplyDelete
  30. It good work Mr. President...

    My advice is that we need to deep down to the source. We can't cut branches while roots are still there.....

    Thanks

    ReplyDelete
  31. Safi sana JK. Sasa tunaomba tutolee na Lulu.

    ReplyDelete
  32. Ni afadhali kugharamia matibabu kuliko kuhudhuria mazishi

    ReplyDelete
  33. Tunamshukuru President kwa hilo, lakini tunakuomba muheshimiwa utusaidie kuumaliza mtandao huu wa madawa ya kulevya.

    Kuna Vijana wengi sana ambao wanataabika huku mitaani hawana misaada yeyote zaidi ya kupora vitu vya watu na kuuza hata kama nivyathamani WAMEFIKIA HATUA YA KUVUNJA MAGARI NA KUIIBA ili mradi wapate PESA YA kununua madawa hayo. Tunaomba muheshimiwa, utusaidie kutuondolea balaa hili, tunafahamu si rahisi wote waje kwako kuomba msaada wa tiba nawe sijui kama utaweza!!! LAKINI, KUNA NJIA MOJA TU, NAYO NIKUSAFISHA MTANDAO HUU KWA GHARAMA YEYOTE, KINGA NI BORA KULIKO TIBA.

    ReplyDelete
  34. Kwanza kabisa tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kitendo alichokifanya cha kumsaidia matibabu kipenzi cha wengi Ray C. Mungu akubariki Mheshimiwa Rais. Isipokuwa Ikulu hapakuwa mahali sahihi pa kuingia kwa kila anayepata msaada kutoka kwa Rais, sababu Ikulu ni mahali Patakatifu. Ray C angeweza kwenda kwenye vyombo vya habari kutoa shukrani zake kwa Rais bila kwenda Ikulu.

    Mheshimiwa Rais, ningependekeza kwamba, umkabidhi Ray C kwenye vyombo vya Usalama asaidie Serikali namna alivyokuwa anapata dawa za kulevya ili njia hiyo isaidie kupunguza ongezeko la matumizi ya madawa ya kulevya.

    Elbafra Dito, Dar es Salaam. Tanzania.

    ReplyDelete
  35. Fatma shariffDecember 11, 2012

    Napenda kutoa shukrani za kipekee kwa Rais wetu kipenzi kwa msaada alioutoa kwa dada yetu Ray C. Ama kwa hakika ni ushupavu wa hali ya juu aliouonyesha na pia jamii isiwe na wasi wasi kwa Mkuu wetu huyu wa nchi kwani ni msikilizaji na mtekelezaji wa haja kwa wananchi wake. Kuhusu kuhudumia na vijana wengine ambao wamezama kwenye janga hili la madawa ya kulevya ameruhusu viwekwe vituo maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wale walioathirika tunachotakiwa kama wanajamii ni sisi kutilia mkazo maana kwa kila familia lazima kutakuwa na mtoto japo mmoja aliyepotea njia hivyo ni vizuri wahusika wafuatilie kwa karibu hizo fursa ili vijana wao walioathirika waweze kutibiwa. Maana kwa kila kituo kinatakiwa kitoe takwimu sahihi ili waweze kupatiwa msaada kupitia kwenye serikali zao za mitaa. Raisi wetu kwa kupitia kitengo maalumu anapeleka misaada huko ila sasa wale watendaji hawatoi ushirikiano mzuri na pia wote wenye watoto waathirika wangepewa ushuhuda kama mama Ray C. Amehakikisha amesimama kidete mpaka mwanawe karudi kwenye mstari, Nakupa Big up mama Ray C Mungu akupe nguvu hizo mpaka ujuwe mwisho wa binti yako.

    KWAKO RAY C,
    NAFASI HII NI YA PILI AMBAYO MUNGU AMEKUPA SASA ITUMIE VIZURI NA PINDIPO UTAPOPONA NAOMBA UWE BALOZI WA NCHI YETU KWENYE MASUALA YA MADAWA YA KULEVYA. UTAPATA CHANGAMOTO NYINGI SANA LAKINI MUNGU ATAKUPA UWEZO NA NGUVU ZA KUSHINDA MAJARIBU NA UTARUDI SALAMA USALIMINI ULINGONI. WEWE UWE UNAWAKEMEA WALE WATAKAOJARIBU KUKURUDISHA TENA HUKO ULIKOKUWA MUNGU ATAKUEPUSHA ZAIDI NA UTAFAULU MTIHANI HUU ULIOPEWA.

    KWETU SISI
    Kabla hujafa hujaumbika. Kama huna mtoto basi atakuwa wa nduguyo au wa jirani yako au kaka/dada yako hivyo mtoto wa mwenzio anapokuwa kateleza, muombee arudi kwenye mstari. Sivyema kumbeza kwani dunia ni duara huwa inazunguka, leo kwake na huenda ikawa kesho kwako. Tuombeane dua tuishi kwa upendo wa hali ya juu kwani MWANA WA MWENZIO NI WAKO.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE WOTE. asante. Mama Abbas, Magomeni, Lango la Jiji.

    ReplyDelete
  36. Kiukweli nimesisimka na nimelengwa na machozi baada ya kuona kazi nzuri na yenye upendo iliyofanywa na mheshimiwa Raisi Jaka Mrosho Kikwete. Hili ni jambo jema sana haswa ukinzingatia wewe ndo baba wa Tanzania kwa wakati huu hivyo unapaswa kuangalia wanao kwa jicho la kipekee kabisa kama ulivyo amua kufanya kwa huyu dada yetu mpendwa ambaye alikwisha potea kwenye ulimwengu wa NURU. Ahsante sana Raisi wetu Mungu akuzidishie kila ulipopungukiwa. Mungu akuzidishie amani, upendo, ucheshi na hata busara katika kipindi hiki unachoelekea kumalizia ngwe yako ya URAISI, Ningetamani sana uendelee lakini maadili tuliyojiwekea hayaruhusu na ndio nguzo kubwa ya kutotutumbukiza kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe hakika wewe ni MTUMISHI mwema usiyejali rangi wala kabila wala dini. Allah akubariki
    Mdau

    ReplyDelete
  37. Ray C taja waliokuuzia kuonesha kweli upo siriazzzz....na unawatakia mema vijana wengine wanao angamia...langa kapona ila mbona hajataja waliomuuzia?..so yaleyale tuu...kampeni ya madawa ya kulevya kwa kuhamasisha vijana wasitumie huku huyo alieacha hataki kutaja walio kwenye chain ya kuuza ni unafiki!!

    shukran kwa JK kwa kusaidia jamii

    ReplyDelete
  38. Ray C mdau hapo juu katoa ushauri mzuri sana.Achana na hao sijui akina MACHO MUNGU Sijui BARABARA MACHO sijui MZIGO MACHO(Kwa kidhungu inaleta maana)...Hawana future hao.Watakuharibu tu.Wamebaki kuiba POWER WINDOW ili wabwie SEMBE.

    Mimi ni kijana mcha mungu sana na nina kipato chakawaida.Sio maskini wala tajiri ila ninachojivunia ni MAADILI MEMA...Sio lazima uolewe na Mtu maaufu.Nitafute niko serious nakupenda kwa dhati tangu enzi ukiimba nyimbo ile ukiwa japani(UKO WAPI NIKUFUATE)...Na kila nilipokua nakuona katika video zako naishia kusononeka tu.Kukufuata siwezi ila Naamini kuna siku M.Mungu atatuunganisha tu hata UZEENI...Nakusubiri REHEMA.
    cibmannamdun@yahoo.com

    ReplyDelete
  39. Pole RC Mimi nakushauri kuwa ukipona vizuri, achana na kazi ya muzic kwa sababu kwa sasa umri wako ni mkubwa na game la muziki linaushindani mkubwa sana. kazi nzuri unayoweza kufanya ni kuwa PR yaani afisa uhusiano au afisa habari hasa kwenye NGO zinazopambana na madawa ya kulevya, unyanyapaa n.k. hii ni nzuri kwako kwa kuwa pia uliwahii kuwa mtangazaji, na uko presentable mbele ya hadhara na jamii kwa ujumla ona unavyopendeza kwa mavazi hayo sio zile za vitovu njee kwa umri wako kwa sasa.
    najua NGOs nyingi watakukubali bila ya usaili, maana unalipa kwa sasa.

    MWATANGE MUWINA MUNYA KILUNGA/KAYE, NYONGISE NDEMUYAGO ISAYO SINDIPILUKILA NG'OO.

    ReplyDelete
  40. I m speechless....I Love it My President. God Bless u, and God Bless Tanzania.

    ReplyDelete
  41. Ahsante sana Raisi JK kwa ubinaadamu mkubwa kwetu!

    Je, hao walikuwa wanampimia hayo madawa ya kulevya mbona hatukuwaona kutoa chochote?

    Jamani tukio hili la mkasa wa RC liwe ni mwamko na fundisho kwetu Watanzania licha ya Kumshukuru Raisi wetu Mpendwa, tuangalie ni jinsi gani MADAWA YA KULEVYA HAYAKUBALIKI, TUSEME HAPANA KWA MADAWA YA KULEVYA!

    ReplyDelete
  42. Hongera sana Raisi Jakaya Kikwete,

    Lohhh RC jamani mzuri, mnaona sasa uzuri wake unarejea tena baada ya kupata nafuu za matumizi ya madawa ya kulevya.

    Raisi JK hongera sana na umetusaidia kuirudisha nuru ya uzuri wa RC ambayo sasa inerejea tena!

    ReplyDelete
  43. mi sijapenda hii kitu alofanya JK
    utasaidiaje watu wanaojitakia wenyewe bana wkati kuna wanaokufa kwa kukosa matibabu????? huyu mtu mzima kabisa hajui kwamba madawa ni sumu???

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ngojea mtoto wako awe teja ndo utajua na kuea humble ....

      Delete
  44. Tunakushukuru saaana raisi wetu mpendwa Jakaya Kikwete, hatuna cha kukulipa ila mwenyezi mungu atakuzidishia, Ray C sote tunakupenda na tumefarijika kukuona ktk hali hii, m/mungu atakusaidia sote tunakuombea dua mtu wetu , tupo pamoja sana..

    ReplyDelete
  45. Ray C she is talented, Ray C ni star, Ray among the legend muziki wa kizazi kipya. Sisi ni binadamu mwenyezi Mungu kila mtu amemuandikia nini kitamtokea mbele ya maisha yake. Ila hakuna anayejua muda gani.

    Rais Kikwete siyo kwamba hapendi kusaidia wananchi wake hapana anasaidia sana, ila akisema aanze kutangaza hawataisha. Ila ni mwenye huruma aliona binti wa watu ni mdogo na kipaji anacho ila mambo ya dunia. Basi kama binafsi kuchukua jukumu hilo la kumtibia basi kushkuru Mungu.

    Ray C bado ni msichana ambaye anaudai muziki wa kizazi hela nyingi sana. Sasa arekodi nyimbo za kutosha nina imani Mungu yupo nasi sote na atafanikiwa zaidi hata ya zamani.

    Naomba watanzania tusihukumu na tuendele kuelemishana maana hujui wewe kesho utaangukia wapi.

    Mungu Mbariki Ray C, Mungu Mbariki J. Kikwete, Mungu wabariki Watanzania wote. Ameen

    ReplyDelete
  46. UUNGWANA NI VITENDO!

    Tunaweza kumpima Mhe. Raisi wetu kwa mambo kama hili suala la Ray C, mara zote Mhe. JK amekuwa mbele kuhakikisha mwelekeo wa nchi unaimarika, ISIPOKUWA NI DHAHIRI UNAPOKUWA MSIMAMIZI MKUU HUWEZI KUFANYA KILA KITU MWENYEWE, UNALAZIMIKA KUMPA MSAIDIZI MWAMINIFU MAJUKUMU KWA NIABA YAKO.

    SASA KIBAYA ZAIDI INAPOKIFIKA NAFASI HII YA KUAMINIWA NDIO TUNAKUTA BAADHI YA VIONGOZI WASIO WAADILIFU WANAHARIBU!

    HIKI NDIO KITU KINAMPONZA RAISI WETU MUUNGWANA JK, !!!

    LAITI INGELIKUWA KILA KITU ANAFANYA RAISI JK YEYE MWENYEWE, NADHANI KUSINGEKUWEPO NA WA KUMLAUMU, NA ENDAPO ATATOKEA WA KUMLAUMU KWA NINI TUSIMWONE MTU HUYO SIO MWENZETU?

    ReplyDelete
  47. Inshallah ,

    Mwenyezi Mungu atakurahisishia Raisi JK kwa kukupunguzia mitihani na kuwashinda maadui zako!

    ReplyDelete
  48. Ahsante sana Kiongozi wetu Raisi Mhe. JK kwa hisani yako kwetu sisi wananchi!

    Umemfanyia Ray C lakini hisani yako imetufikia Watanzania wote!

    TUCHUKUE NAFASI HII TUYAANGALIE MADAWA YA KULEVYA KWA PANDE 2 ZA SARAFU:

    WAKATI ATHARI IKIWEPO:
    -Bibie Ray C alionekana kama bata aliyenyeshewa na mvua.
    -Bibie Ray C mboni za macho yake zilikuwa kama mbuzi aliyekoswa koswa na radi.
    -Bibie Ray C alikuwa amezeeka ghafla akiwa na umri wa miaka 29 akaonekana kama ana miaka 92!

    BAADA YA KUKOMBOLEWA KTK MADAWA:
    -Bibie Ray C anarudi na nuru yake.
    -Bibie Ray C mboni za macho yake zinarejea kung'ara tena.
    -Bibie Ray C amerudi mbichiiii !!!

    AHHH TUYACHUKIE MADAWA YA KULEVYA YALITAKA KUTUHARIBIA MREMBO WETU!

    DAH MTOTO MZURI JAMANI RAY C !!!

    ReplyDelete
  49. Mwenyezi Mungu akubariki sana Mheshimiwa Rais kwa kumsaidia dada yetu.

    Kwa Ray C pia Mwenyezi Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu, ili uweze kukipita salama. Mama Ray C pia Mweneyzi Mungu akubariki na kukupa nguvu zaidi maana hukuacha kuhangaika kutafuta msaada kwa mwanao, pia usiache pia kumweka mbali na marafiki wasio wazuri. Kwani naamini katika kipindi hiki, hao waliokua wanajiita ni marafiki zake, watakua hawaonekani kumpa Ray C msaada wa hali na mali... God Bless you all.

    ReplyDelete
  50. Kwenye matatizo ndio utamjua nani rafiki na nani mnafiki!

    Unakuta mtu unamwita rafiki akipita kuisikia kuwa hali yako iko vinaya ama pana yaliyo kukuta anakuja akionana na wewe anakuwa kijino pembe akiona kuwa umekwama.

    Mungu si Athumani, mfikwa hupata muamala na akakomboka na masahibu yaliyomkuta kitu ambacho watu wanafiki daima hawaelewi ya kuwa kama Mungu ndiye aliyeleta hali fulani na Mwenyezi ndiye mponyaji wa shida zote!

    ReplyDelete
  51. Mhe.asante kwa kumsaidia RAY C wetu.Binafsi nampenda sana,nilipomwona gazetini nilila sana ,hatimaye nikaona kuwa umemsaidia,nikalia tena kwa furaha.Endelea na moyo huo,kwa mungu una fungu lako.KWA HILI I LOVE U MR, PRESIDENT LONG LIVE.
    THANKS

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...