Na Mwandishi Wetu

MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ameendelea kung’ara kimataifa baaada ya kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super model na kuwa mwanamitindo bora barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding Model 2012).

Tuzo hiyo utolewa kwa wanamitindo ambao bado wanailetea sifa Afrika kimataifa na Flaviana amekuwa katika chati ya juu. Mwaka jana Desemba, Flaviana alishinda tuzo nyingine ya uwanamintindo bora kutoka kwa diaspora ya Waafrika.

Flaviana kwa ambaye kwa sasa anaishi na kufanya kazi ya uanamitindo New York nchini Marekani kupitia shirika la Wilhelmina Models, mpaka sasa ameweza kuitangaza Tanzania kimataifa kutokana na umahiri wake katika maonyesho ya mavazi.

Tangu ashinde taji la Miss Universe Tanzania mwaka 2007, Flaviana amekuwa aking’ara katika kona zote za dunia na hasa baada ya kumaliza katika nafasi ya sita katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe, huku Tanzania ikishiriki kwa mara ya kwanza.



Ameweza kushiriki katika maonyesho ya mavaz mengi Ulaya na Amerika huku akitoa misaada mingi kwa Watanzania wenzake ambao wamekuwa na ndoto ya kufika mbali katika fani hiyo.

Kwa sasa Flaviana anaendesha taasisi yake, Flaviana Matata Foundation ambayo inasomesha watoto wa kike 16 na mwaka jana alitoa msaada wa vifaa vya kuokoa maisha kama sehemu ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba huku ikiwa kumbukumbu ya kifo cha mama yake mzazi katika ajali hiyo ya mwaka 1996.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Compass Communication Tanzania Limited, Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa wamejisikia faraja sana kwa kumvumbua mwanamitindo huyo ambaye kwa sasa anashika chati ya juu Tanzania na nje ya nchi.

Maria alisema kuwa Flaviana amedhihirisha ubora wake na mpaka sasa amepitiliza kiwango cha kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake, ndoto ambayo alikuwa nayo muda mrefu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. nilipo kua nasoma hii habari mwili wote ulikua unasisimka kwa furaha.yaani namfurahia sana hongera sana flavi tuna taka na wengine kwenye filam,mziki watoke sio wana kaa tu kusubiri muda unakwenda angalau kidogo diamond lakini bado ajitahidi kuweka sim on na kuja kutembea mwenyewe sehem za europe watu wanakuhitaji lakini hajui wakupateje sababu watu wakitafutwa hakuna kinacho fanya kazi si wesite sim email nk,sasa mtu unabaki kutafuta marafiki wakutafutie wanamziki huu ni usumbufu halafu wanakutajia hela ambayo sio.flaviana ametoka mwenyewe kaenda sehem zote zinazo fanya model akajarib kuacha contact zake kila mahali na vingine alijitolea ili kuonyesha uwezo wake.fanyeni kama yeye msilale.

    ReplyDelete
  2. Hongera Sana kwa ushindi na kuitangaza nchi yetu
    It can be done play your part

    ReplyDelete
  3. We Maria hukusikia mwenyewe anasema hakuna alomfikisha hapo alipo...fuatilia mahojiano na Salama...msije onekana mnadandia mafanikio ya mwenzenu wakati ashasema hakuna alimbeba ilikuwa business na amesota na ku fight kufika hapo alipo yeye kama yeye; hakuna mkono wa mtu

    ReplyDelete
  4. hongera sana Flaviana kwa kupeperusha bendera ya TZ. Mwenyezi Mungu akulinde ufanikiwe katika kila jambo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...