Michuzi,
Mimi ni mdau wa blog hii tangu imefunguliwa nataka nipeleke ujumbe kwa wadau wote pale geti la kuingilia standi ya ubungo ni hatari sana kuna vibaka amabao ukiingia umebeba mizingo hasa miwili lazima wakusachi na watatimiza azma yao. Ngoja niwape kisa changu cha kusikitisha sana: Weekend iliyopita nikitokea dar kuja Arusha nilifika pale na bajaj mishale ya saa 12 kasorobo.
Hapa vibaka wanasoma kila anayeingia. Nililipa bajaji na kurudishiwa chenji nikafunga mfuko wangu wa nyuma vizuri nikaaza kuhangahika na mizingo yangu. Kumfikia anayekagua tiketi lilikuwa ni kosa nikahisi kupapaswa makalio kucheki mfuko umeshafunguliwa na pesa inachungulia niligeuka ghafla kijana aliyekuwa nyuma yangu akema kwa uungwana sana " angalia mzee kuwa makini" nikamwangalia anayekagua tiketi nikaona yupo attention anasikiliza nikawa na amani nikamwamini kijana na nikafunga mfuko wangu vizuri kabisa kwani wakati huo nikahisi kwamba labda nilisahau kufunga mfuko wakati natoa nauli ya bajaj nikaendelea mbele mara mtu (mmoja watu kwenye hiyo foleni) akaniambia kama kwa kunisaidia; pitia mlango wa kushoto; nikijaribu huku nasukumana na mizingo yangu mlango hauzunguki kufungua.
Mara sauti nyingine ikatoka nahisi hii ni ya mkaguzi pitia gei la mkono wa kulia.Kweli nikapita kiulaini kabisa. Kabla sijapiga hatua mbili mbele nikakumbuka je mfuko wangu bado uko salama? salaleeeeeeee! pesa yangu yote 155,000/= imeondoka!Baada ya kuomba wasamalia waiangalizie mizigo yangu nihangahike kutafuta hela ya nauli tena nilirudi pale geti nikwambia wamba nyie kama waangalizi wa hapa mmehusika kuibiwa hela zangu akanijibu...
kama uliona mfuko wa nyuma umefunguliwa kwanini usibadilishe mfuko mwingine nikagundua kuwa kumbe mechi yote jamaa alikuwa naishuhudia.
Wadau kaeni chonjo na hapo mlangoni usithubutu weka pochi au pesa mfuko wa nyuma na mbaya zaidi ukitoa nauli wanakuwa wanakuchora.Wakaguzi wa tiketi ubungo bus stand wanashirikiana na wezi.
Wako mdau,
Emma Kanindo
Arusha.
Nikija Dar, pesa za nauli naweke mfuko wa mbele nagawa nusu mfuko mmoja na nusu mwengine, pia kama nina mfuko wa shati pia naweka zengine humo. Pia naweka zengine kwenye soksi. Kwa sasa sitembei na cash nyingi baada ya kupata card yangu ya Umoja. Nafikiri sasa bongo waweke mashine za POS katika maduka ili mambo ya cash yamalizike.
ReplyDeletepole sana,lakini nawewe kwanini unaweka pesa mfuko wa nyuma?tena zote sehemu moja?nadhani wewe ni wa kuja hujawahi kuishi miji mikubwa.mdau CHATHAM.
ReplyDeleteSioni cha ajabu hapo hiyo ndiyo bongoland. Umenusulishwa kuibiwa mara ya kwanza na bado unaweka pesa mfuko ule ule!!! uzembe. Kwamba wakaguzi wa tiketi wanahusika hiyo siwezi kushangaa, hata hivyo utakuwa makini wakati mwingine
ReplyDeleteMazee Chalii wa Arusha Emma Kanindo !
ReplyDeleteUmejichanganya mwenyewe, kwani hujasikia Kituo cha Mabasi kimehamishiwa Kibamba mwisho?
Mzee huo ni uzembe wa hali ya juu kabisa. Mwenzetu unaishi nchi gani hata unaweka mafedha yote hayo kwenye pochi mfuko wa nyuma?
ReplyDeleteTayari walishakushtua mara ya kwanza bado ulikuwa umelala usingizi tu.
Kusudi haiambiwi pole.
Asante kwa taarifa mkuu na pole kwa kulambwa hizo 155,000/=.Lakini kwa upande mwingine mimi nakulaumu wewe mwenyewe!.Siku hizi bwana,mambo yamekuwa rahisi kiasi kwenye kuhifadhi fedha.Unaweza kusafiri na pesa kwa njia nyingi siyo lazima uziweke mfukoni.Dar-Arusha kwa basi unaweza kuweka mfukoni 30,000-50000/= tu ya dharura.Siwatetei hao vibaka ila tuwe makini zaidi.Si vema kutoka Mikoani kwenda Daresalaam na Mil.15 kwenye Soksi,zama hizo zimepitwa na wakati.Tubadilike,twende na Teknolojia
ReplyDeletePole sana walijua huyu ni mgeni kutoka mkoani ss anarudi kwao, wakakuaga na staili hiyo.lengo ni kukuonyesha ukanjanja wa Arusha kujifanya wajuaji kuna wajuaji zaidi. Pole sana na krb tena dar.
ReplyDeleteKosa ni lako mwenyewe, hela haiwekwi mfuko wa nyuma, hela inawekwa mfuko wa mbele, na kwingine siwezi kusema hapa hadharani.
ReplyDeleteInasikitisha sana na bahati mbaya watu wa usalama hawana tofauti sana na hao. Watu wamekuwa wanyama kuliko wanyama.
ReplyDelete
ReplyDeleteHakuna jipya hapo wizi wa aina hyo uko every were hata China kwenye train stations wameandika "BE AWARE OF PICK POCKETS" ukienda thailand wameandika hvyo ukienda Malaysia ndo usiseme wameandika avoid travelling with money, avoid standing in congested areas
sasa hapo bongo ndo usiseme kama ulijiweka ki hasara ndo ishakula kwako huo wizi uko kila mahali hata Arusha stand upo
Pole sana ndugu, 'wanaopigwa' pale kwa style hiyo ni wengi sana pale ubungo. wenyewe wanawaita wanaowaibia ni 'MAMBWIGA'
ReplyDeleteHiyo ilikua byebye Dar kaka, pole sana.
ReplyDeleteMbegu
sasa wewe mdau pamoja na kutuasa baada ya kuuonamfuko wako marayakwanza umefunguliwa kwanini hukuwa makini zaidi ulitakiwa uwe makini maana tiyali ilishakuwa bahati yako.ila tu hapo ubungo mimi nilishauziwa gazeti la mwezi wa sita huku ikiwa ni mwezi wa tisa wakati nimeishapanda basi,nikajidai kununua gazeti lo!nilikoma hivyo pale kilakitu ni wizi wakati mwingine unaibiwa kwa sababu ya haraka wakati mwingine ni uzembe kutokuwa makini
ReplyDeleteKaka kuwa makini wewe kweli unadhubutu kutoa hela watu wanakuona tena hapo Ubungo Terminal. Wakati unasafiri jaribu Kuvaa jeans na usunde hela zako mifuko ya mbele. Ustaarabu huo wa kuweka pesa miuko ya nyuma umeliza wengi weka hata kwenye soksi
ReplyDeleteMdau pole sana,
ReplyDeletehapo getini ndio mtindo wao hasa kwa wasafiri wanosafiri alfajiri. Mimi niliibiwa pochi ikiwa na 120,000/- na document zangu muhimu sana. Uzuri huwa siweki kadi zangu za benki kwenye pochi hata siku moja. Ila leseni, kadi ya matibabu. vyote vilondoka. Nikaripoti hapo Kituo cha Polisi ndani wakaniambia niandike maelezo ili wanze kufuatilia, nilikuta wasafiri wengine kama watatu naio wanamalalamiko hayo hayo wamewekwa tu pending hapo kituoni. Nikaoana najisumbua nikakubali yaishe nikarudi pale ubungo kwenye Kitu cha Mafuta nikatoa pesa nyingine kwenye ATM nikarudi stend nikasafiri kwa uchungu sana. Sio hapo getini hata polisi wanawajua hao vibaka na wanakula nao kwa kuwakatia kidogo wanapakamatwa.
Hovyoooo kabisa.
Masela wakale wapi?
ReplyDeleteUmekutana na Majembe,
Umeonyeshwa kuwa Dar ni zaidi ya Arusha!
Haya ndio madhara ya muda wooote kufungulia Stesheni za Muziki katika Runinga na Redio!
ReplyDeleteIna maana huwa husikilizi hata Taarifa ya Habari!
Wewe Emma Kanindo hivi Arusha ni msituni ya kuwa Habari hazifiki kwa Televisheni, Redio na Magazeti?
Ina maana taarifa zilizozagaa nchi nzima kuwa Kituo cha Mabasi kinahamia Kibamba kutoka Ubungo wewe ulikuwa manyasini hukuzipata?