Wakazi wa mikocheni, eneo la Regent Estate jijini Dar es salaam wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu katika kipindi hiki cha kuelekea mvua za masika kutokana na maji ya taka ikiwemo kinyesi, yanayotoka kwenye nyumba zote zilizoko mtaa wa Mgombani, kutiririka juu ya mtaro uliokuwa ukitumika kupeleka takataka hizo baharini kama inavyoonekana katika picha. 

Wakazi hao hasa waliopo katika makutano ya mtaa wa Mgombani na njia ya kuelekea mtaa wa Chwaku (nyuma ya Shoppers Plaza) wameieleza Globu ya Jamii kwamba wamepitia njia zote za uongozi kuanzia kwa serikali ya mtaa, diwani hadi uongozi wa juu wa manispaa ya Kinondoni bila mafanikio. 

Uongozi wa DAWASCO ambao ndio wanahusika na suala hili walipoambiwa na wakazi wa maeneo hayo walidai kwamba pump ya kunyonya maji hayo kuyapeleka baharini imeharibika na hawana namna nyingine ya kufanya ingawa Ankara zao za kila mwezi zinalipiwa huduma hiyo. Hali hii imekuwa hivyo toka mwezi wa nane 2012 hadi leo. 

Na jambo la hatari zaidi ni kwamba maungio ya mabomba ya maji masafi yapo katikati au yamefunikwa na kinyesi hicho. 

Wadau mnaombwa ushauri. Kama vipi tumepanga kuandamana...
 Mkazi wa mtaa wa mgombani.
Mtaa huo pia ni makao makuu ya taasisi za utafiti maarufu nchini, ikiwemo REPOA na IPSOS SYNOVATE ambazo bila shaka zitafanya na kutoa tafiti kuhusu madhara ya mitaro hiyo iliyojaa kinyesi....
Mtaro mchafu
Maji yaliyojaa kinyesi kutoka katika vyoo vya mitaa yote ya hapo
Hatari kwa wakaazi na hata wapita njia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Nilifikiri ni Manzese na Tandale tu kumbe hata Masaki kuna MIJITU ya mwaka 47? 'hongereni zenu'

    ReplyDelete
  2. Ingekuwa Mbagala wangepiga kelele ile mbaya. Ila hapa wataremba kwamba bomba zimepasuka bahati mbaya....

    ReplyDelete
  3. Junction ya mtaa huo na Chato si ndiyo ilipo nyumba ya mkuu wa nchi?

    ReplyDelete
  4. DAWASCO ni wauwaji na wezi, wanawezaje kuacha maji masafi yachanganyike na kinyesi kwa muda wote huo? Vile vile wanatakiwa kurudisha fedha walizolipwa za maji machafu kwa muda wote huo maana huduma haikutolewa vinginevyo ni wizi. Hata manispaa ya Kinondoni wanangoja watu waanze kufa ndio wachukue hatua. Jee baraza la mazingira ambao wapo jirani na eneo hilo wanayaona haya na wanasemaje? Mvua zimeanza kwa hiyo tungojee hatua za dharura kama tulivyozoea!!

    ReplyDelete
  5. Hilo jina REAGENT mnatakiwa mlibadili kwa kuwa halilingani na jinsi uchafu wa eneo lenyewe na mazingira!

    Mtashitakiwa na wenyewe Waingereza wakiona hivyo.

    ReplyDelete
  6. MBAGALA ni kusafi kuliko REGENT ya Bongo!

    Tatizo watu wanaishi kwa mapokeo kama mistari inavyochanwa na wanamuziki kama vile Mbagala huku nyumba huku jalalaaaa !!!

    ReplyDelete
  7. toa toa diskasi hizo watu tunakula maisha ughaibuni hatujaona hizo kitu for too long chagueni viongozi wa maana mpate mabadiliko alaaaa

    ReplyDelete
  8. Mimi kinachonishangaza zaidi nikwamba ofisi za Baraza la Taifa la Mazingira zipo jirani kabisa na eneo hilo. Baraza hilo limekuwa mstari wa mbele kuwafungia wachafuzi wengine wa mazingira hasa hoteli na wakazi wa karibu na fukwe za bahari. Sielewi linasubiri nini kuwashughulikia DAWASCO. Waathirika tumekuwa tukimfuatilia Dr Robert wa NEMC lakini hatupati jibu la kueleweka. Naomba na wengine mujaribu kumuuliza, simu yake ni 0769-526470 na email yake ni ntakamulenga@yahoo.com, labda atawasikiliza.

    ReplyDelete
  9. Kinachonishangaza ni kwamba hapa katika mtaa huu, tupo jirani kabisa na mheshimiwa JK. Sina uhakika kama DAWASCO na watu wa NEMC wanaona fahari kama Raisi wetu atapatwa na kipindupindu au la

    ReplyDelete
  10. Juzi niliona kuwa rent dar imefika hata $8000 kwa mwezi hivi ni viwango vya chelsie london na kumbe mazingira yenyewe ndio hayo da !

    ReplyDelete
  11. Hii ni hatari na uzembe wa hali ya juu yaani DAWASCO wanaweka afya za wananchi hatarini eti kwa sababu ya kukosa pump ya kuvuta maji kwenda baharini? Huu mtaa unatoa harufu mbaya sana maji yanafurika hadi milangoni mwa ofisi za watu. Nilitembelea ofisi za REPOA nikashindwa kuingia maana sikua na gari kinyesi kimetapakaa wakati wa mvua. Viongozi husika wachukue hatua wananchi wataugua vipindupindu

    ReplyDelete
  12. Hilo la kumwaga kinyesi baharini ni kosa kubwa sana na iko siku tutakuja lipa. Tujifunze kwa miji mingine duniani ambayo iliwahi kufanya hivyo. Na hivyo visima vya maji mlivyochimba basi mtavuna mlichopanda.

    ReplyDelete
  13. BONGO NI NEW YORK...HOVYOo..day dreams!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...