Wakazi wa mikocheni, eneo la Regent Estate jijini Dar es salaam wanakabiliwa na hatari ya
kupatwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu katika kipindi hiki
cha kuelekea mvua za masika kutokana na maji ya taka ikiwemo kinyesi,
yanayotoka kwenye nyumba zote zilizoko mtaa wa Mgombani, kutiririka juu
ya mtaro uliokuwa ukitumika kupeleka takataka hizo baharini kama
inavyoonekana katika picha.
Wakazi hao hasa waliopo katika makutano ya
mtaa wa Mgombani na njia ya kuelekea mtaa wa Chwaku (nyuma ya Shoppers
Plaza) wameieleza Globu ya Jamii kwamba wamepitia njia zote za uongozi
kuanzia kwa serikali ya mtaa, diwani hadi uongozi wa juu wa manispaa ya
Kinondoni bila mafanikio.
Uongozi wa DAWASCO ambao ndio wanahusika na
suala hili walipoambiwa na wakazi wa maeneo hayo walidai kwamba pump ya
kunyonya maji hayo kuyapeleka baharini imeharibika na hawana namna
nyingine ya kufanya ingawa Ankara zao za kila mwezi zinalipiwa huduma
hiyo. Hali hii imekuwa hivyo toka mwezi wa nane 2012 hadi leo.
Na jambo
la hatari zaidi ni kwamba maungio ya mabomba ya maji masafi yapo
katikati au yamefunikwa na kinyesi hicho.
Wadau mnaombwa ushauri. Kama vipi tumepanga kuandamana...
Mkazi wa mtaa wa mgombani.
Mtaa huo pia ni makao makuu ya taasisi za utafiti maarufu nchini, ikiwemo REPOA na IPSOS SYNOVATE ambazo bila shaka zitafanya na kutoa tafiti kuhusu madhara ya mitaro hiyo iliyojaa kinyesi....
Mtaro mchafu
Maji yaliyojaa kinyesi kutoka katika vyoo vya mitaa yote ya hapo
Hatari kwa wakaazi na hata wapita njia
Nilifikiri ni Manzese na Tandale tu kumbe hata Masaki kuna MIJITU ya mwaka 47? 'hongereni zenu'
ReplyDeleteIngekuwa Mbagala wangepiga kelele ile mbaya. Ila hapa wataremba kwamba bomba zimepasuka bahati mbaya....
ReplyDeleteJunction ya mtaa huo na Chato si ndiyo ilipo nyumba ya mkuu wa nchi?
ReplyDeleteDAWASCO ni wauwaji na wezi, wanawezaje kuacha maji masafi yachanganyike na kinyesi kwa muda wote huo? Vile vile wanatakiwa kurudisha fedha walizolipwa za maji machafu kwa muda wote huo maana huduma haikutolewa vinginevyo ni wizi. Hata manispaa ya Kinondoni wanangoja watu waanze kufa ndio wachukue hatua. Jee baraza la mazingira ambao wapo jirani na eneo hilo wanayaona haya na wanasemaje? Mvua zimeanza kwa hiyo tungojee hatua za dharura kama tulivyozoea!!
ReplyDeleteHilo jina REAGENT mnatakiwa mlibadili kwa kuwa halilingani na jinsi uchafu wa eneo lenyewe na mazingira!
ReplyDeleteMtashitakiwa na wenyewe Waingereza wakiona hivyo.
MBAGALA ni kusafi kuliko REGENT ya Bongo!
ReplyDeleteTatizo watu wanaishi kwa mapokeo kama mistari inavyochanwa na wanamuziki kama vile Mbagala huku nyumba huku jalalaaaa !!!
toa toa diskasi hizo watu tunakula maisha ughaibuni hatujaona hizo kitu for too long chagueni viongozi wa maana mpate mabadiliko alaaaa
ReplyDeleteMimi kinachonishangaza zaidi nikwamba ofisi za Baraza la Taifa la Mazingira zipo jirani kabisa na eneo hilo. Baraza hilo limekuwa mstari wa mbele kuwafungia wachafuzi wengine wa mazingira hasa hoteli na wakazi wa karibu na fukwe za bahari. Sielewi linasubiri nini kuwashughulikia DAWASCO. Waathirika tumekuwa tukimfuatilia Dr Robert wa NEMC lakini hatupati jibu la kueleweka. Naomba na wengine mujaribu kumuuliza, simu yake ni 0769-526470 na email yake ni ntakamulenga@yahoo.com, labda atawasikiliza.
ReplyDeleteKinachonishangaza ni kwamba hapa katika mtaa huu, tupo jirani kabisa na mheshimiwa JK. Sina uhakika kama DAWASCO na watu wa NEMC wanaona fahari kama Raisi wetu atapatwa na kipindupindu au la
ReplyDeleteJuzi niliona kuwa rent dar imefika hata $8000 kwa mwezi hivi ni viwango vya chelsie london na kumbe mazingira yenyewe ndio hayo da !
ReplyDeleteMasaki?
ReplyDeleteHii ni hatari na uzembe wa hali ya juu yaani DAWASCO wanaweka afya za wananchi hatarini eti kwa sababu ya kukosa pump ya kuvuta maji kwenda baharini? Huu mtaa unatoa harufu mbaya sana maji yanafurika hadi milangoni mwa ofisi za watu. Nilitembelea ofisi za REPOA nikashindwa kuingia maana sikua na gari kinyesi kimetapakaa wakati wa mvua. Viongozi husika wachukue hatua wananchi wataugua vipindupindu
ReplyDeleteHilo la kumwaga kinyesi baharini ni kosa kubwa sana na iko siku tutakuja lipa. Tujifunze kwa miji mingine duniani ambayo iliwahi kufanya hivyo. Na hivyo visima vya maji mlivyochimba basi mtavuna mlichopanda.
ReplyDeleteBONGO NI NEW YORK...HOVYOo..day dreams!!
ReplyDelete