Hali inavyojionyesha sasa ni kuwa filamu za kiswahili miaka michache ijayo zitakuja kuteka soko katika nchi nyingi duniani kuliko ilivyo sasa hivyo hakuna haja yoyote ya kutumia kiingereza katika filamu zetu sisi kama waafrika tunaopaswa kuendeleza na kukuza mila na tamaduni zetu ikiwemo lugha ya kiswahili ambayo ni lugha inayozungumzwa na mataifa mbalimbali.
Watengenezaji wa filamu nchini Denmark ni kama wanatupa ishara kuwa filamu za kiswahili ni lulu huko ulaya hivyo tufanye juu chini kuongeza ubora katika filamu zetu ili kuteka soko la dunia.
Tantine ambaye jina lake halisi ni Tatu Daniel Musa ni actress anayekubalika nchini Denmark akiwa tayari amecheza filamu chache tu huku filamu yake ya JABUKA ikiwa imemfanya akubalike vizuri kwa mashabiki. Filamu hiyo imetumia lugha ya kiswahili hivyo kuonyesha kuwa kiswahili kinatuunganisha watu wengi Afrika, ulaya na marekani.
Tantine muigizaji aliyejaaliwa mvuto wa aina yake ana asili ya Tanzania na Congo. SWP ilipomuuliza anavutiwa na kazi za actors gani katika nchi za africa mashariki alijibu kuwa anapenda kazi za Irene Uwoya and Wema Sepetu.

Actress huyu anayezungumza kiswahili, kidanish na kiingereza anasema kuwa filamu za kiswahili zinapendwa katika nchi za scandnavia lakini tatizo ni kuwa hazifiki huko hivyo wadau kukosa filamu hizo pengine ikiwa sababu kubwa kwa wao kuanza kutengeneza filamu kwa kiswahili ili kuwapa wadau kitu wanachotaka.
"Kwakweli filamu za kiswahili zina pendwa sana apa Scandinavia Kuna wadau wengi wanatamani movie za kiswahili ila wanakosa sehemu za kuzinunulia ili wazione".
Hilo linatokea hasa kutokana na nchi nyngi za scandinavia kuwa na ushirikiano wa karibu na nchi za africa mashariki na pia mara nyingi wanamuziki wa Tanzania wakialikwa kufanya show katika nchi hizo. Hata hivyo subtile ya kiingereza bado ni muhimu ili kuzidi kuwavutia wasiojua kiswahili ili kukuza soko zaidi.
Hili linatakiwa kuchukuliwa seriously kwa wasambazaji na watengenezaji wa filamu za kiswahili katika kusambaza filamu katika nchi ambazo kazi zao zinakubalika hii ndivyo inavyofanyika hata Hollywood na Bollywood kutoa kipaumbele na kufanya utafiti wa soko katika nchi wanazohisi kazi zao zinakubalika.
Serikali yetu nayo kupitia kwa rais Kikwete isikie kilio hiki cha wasanii wa filamu maana kama serikali ikiwa serious itakusanya mapato mengi sana kupitia filamu na wasanii kuwa na kipato kizuri zaidi kuliko ilivyo sasa. Pichani ni muigizaji Tantine anayeishi Denmark
Hapa UK filamu zinaonyeshwa kwenye lugha halisia isipokuwa wanaweka "Sub-title" ya kiingereza. Nchi nyengine ya Ulaya wanatafsiri kwa lugha yao. Wema Sepetu akionyeshwa Germany utamuona anazungumza kijerumani.
ReplyDeleteHALLO WATANZANIA TUACHE KUDANGANYANA, MIMI NI MKAZI WA DENMARK WA MIAKA MINGI TU ,ZAIDI YA MIAKA 20 KWA KWELI SIJAWAHI ONA FILAMU YEYOTE YA KISWAHILI HAPA DK. KIDOGO HUA FILAMU ZA KUTOKA WEST KAMA SENEGAL AU GAMBIA , HATA HIZO ZA KINAGERIA HAZINA MARKET WALA STORI ZA KUELEWEKA NI UCHAWI TU AU MALAYA ANADAIWA PESA ALIOKOPA KURUDISHA KWA AGENT ALIEMPA TIKETI YA KUJA ULAYA SPAIN,AU ITALY,.
ReplyDeleteSIO NAKATISHA TAMAA TUJIFUNGE WASANII WETU WAWEZE KUTUNGA STORY NZURI ZA KIMILA, ZAIDI YA HAO KINA WEMA SEPETU AU IRENE UYOWA, KUJIFANYA WAO NI SANA HATA ZAIDI YA KINA JULIA ROBERTS, HATA KUMSHINDA BEYONCE AMBAYE HAHAUGUA HATA MAFUA TANGUN AZALIWE. TUNAONYESHA MAKUBWA AMBAYO YANATUPITA KIMO TUWE TUNAONYESHA STORI ZINAZOENDEKA NA MAISHA YA KIAFRIKA. SIO JUMBA LA DHAHABU WAKATI MCHEZA FILAMU HIO KAKULIA MWANANYAMALA MAJI MACHAFU, AU YOMBO VITUKA SANA MJINI KWAKE TANDALE, NI AIBU TUNACHEKESHA
kwa hiyo huyo tantine kadanganya sio. hahaha kwa nini usifanyike utafiti wa kimasoko huko ulaya? tz hakuna chombo cha kueneza kiswahili ndani na nje va nchi tubadilike ha2wezi fanikisha kwa porojo. hahahaha
ReplyDeleteWaliofanikisha kuongea lugha yao katika filamu mbali na kiingereza au lugha nyingine maarufu sana duniani na sinema zao zikaendelea kuhit ni CHINA na INDIA tu...Sababu kubwa ya mafanikio yao ni kutengeneza stori zenye kuonesha mandhari halisia ya tamaduni zao pamoja na vionjo vingi vya asili.Mfano Sinema nyingi za Kihindi zinaonesha visa vya mapenzi katika uhalisia wa tamaduni zao na huweka vionjo vya nyimbo zao za asili kutoka kwa waimbaji wao(Angalia Andha Kanoon, Kuch kuch hota he,Hatya nk)Hata china pia...Tofauti na kwetu unakuta lugha inayotumika ktk Sinema fulani ni kiswahili lakini muziki unaowekwa ni wa Jay Z,West life,R.Kelly wakati tuna nyimbo nyingi sana za wasanii wetu wa kiswahili ambazo zingeweza kujazia na kuleta maana...Hivyo mtu wa Magharibi haoni tofauti ya sinema zetu na za kwao kwani tofauti pekee ni lugha ya kiswahili tu....Nadhani waigizaji wetu wanahitaji kubadilika la sivyo mtaendelea kutawala soko la tanzania tu NA KUENDELEA KUJISIFIA KUTOA SINEMA AROBAINI KWA MWAKA NA MAFANIKIO PEKEE IKIWA NI KUNUNUA HARRIER PEKEE KAMA ZAO LA SINEMA AROBAINI.
ReplyDeleteNI KWELI TUACHE KUDANGANYANA NANI ANA MUDA ULAYA WA KUANGALIA SINEMA YA MASAA MATATU WATU WANABISHANA KUHUSU ISHU AMBAZO SIO ISHU ULAYA? KUNYANG'ANYANA MIRATHI, KUGOMBEA WANAUME, WATOTO WENYE KURUDI NYUMBANI USIKU, MATAPELI, UGOMVI WA FAMILIA, BINTI KIKOJOZI/ UCHAWI/ KWA UJUMLA HIZO NDIO NYINGI YA SINEMA ZETU NA HATA WAHINDI NA KUWA SOKONI MUDA MREFU WANAJITAHIDI KUFUPISHA SINEMA ZAO NA KULETA 'REAL ISSUES' KAMA MFANO MY NAME IS KHAN - SINEMA INAYOONYESHA CURRENT PROBLEMS.
ReplyDelete