Waziri Mkuu Mizengo Pinda,(kulia)akidilishana mawazo na Mkurugenzi wa Kampuni za Msama,Alex Msama aliesimama kushoto,walipokutana nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dododma,katikati ni John Shibuda Mbunge wa Maswa Mashariki (CHADEMA). 
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda,akipewa pole kwa kazi na Mkurugenzi wa Kampuni za Msama,Alex Msama, walipokutana kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, mara baadaya kuahirishwa kikao cha kujadili bajeti ya Wizara ya kilimo na Ushirika . 

 Mbunge wa Simanjilo (CCM)Ole Sendeka,mwenye suti(kulia)akipeana mkono wa salamu na Naibu Meya wa Jiji la Mbeya,Fungo Mwambe,nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma,katikati ni Dk,Mary Mwanjelwa,Mbunge wa Viti maalum,(CCM) wegine ni Madiwani wa Jiji la Mbeya,waliotembelea Dodoma ili kujionea vikao vya bunge la bajeti vinavyoendelea Bungeni mjini Dodoma.

 Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM)Nimrod Mkono,(kushoto)akitafakari hoja mbali mbali za kikao cha bajeti ya wizara ya Kilimo na Ushirika,sambamba na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion,Alex Msama walipokutana kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma,mara baadaya kuahirishwa kwa kikao cha kujadili bajeti ya kilimo kwa mwaka wa 2013..2014.

 Wabunge wa Viti maalum (CCM)rI Ritha Kabati,(kushoto)na Dk,Mary Mwanjelwa(kulia)wakifurahia pamoja na Madiwani wa Jiji la Mbeya nje ya ukumbi wa bunge, waliowatembelea Bungeni mjini Dodoma kujionea vikao vya bunge la bajeti vinavyoendelea mjini Dodoma.
.Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa,Shamsi Vuai Nahodha,(kushoto)akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Alex Msama,walipokutana nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma,mara baadya kuahirishwa kwa kikao cha kujadili hotuba ya bajeti ya wizara ya kilimo na ushrika,katikati ni Mbunge wa Igalula,(CCM)Dk,Athumani  Mfutakamba..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. huyu msama anatemebelea bunge kama nani?

    ReplyDelete
  2. Mbona picha ni Msama tu Ankal naomba unijuze huyu jamaa ni nani? Mimi ndiyo kwanza namsikia

    ReplyDelete
  3. Acheni wivu nanyi katembeleeni bunge kujifunza mambo ya huko mkiweza mkauze sura kama wenzenu, tena nyie sitashangaa hata mlima kilimanjaro hamjaupanda.

    ReplyDelete
  4. Jamani bungeni hata wewe unaweza kwenda....labda tumuulize tu Ankal mbona kapewa globu-time hivyo?

    ReplyDelete
  5. Kweli tatizo la wabongo kila kitu wivu tu

    ReplyDelete
  6. What is special to alex msama? Viongoz wanamjua vizuri au wanakubali tu kuuza nae sura? Tafakari, chukua hatua!

    ReplyDelete
  7. Wewe Anony. wa tatu kwani kupanda k'njaro ndo nini? mbona pumba sana?

    ReplyDelete
  8. Wewe unayesema kuwa tuna wivu hujui kitu kinaitwa "Special interest group" Huyu bwana ni mfanyabiashara yupo hapo ku-lobby au kuwalaghai watunga sheria. Wewe unasema mtu yeyote anaweza kwenda bungeni, basi wewe nenda tuone kama utapiga picha na Pinda na baraza lote la mawaziri huku ankal akikupaisha hewani. Hii tabia ya lobbists kuanza kuwepo Tanzania ni mbaya. Wanyonge watakosa mtetezi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...