Mashindano ya kwanza ya ulimbwende nchini yalifanyika mwaka 1967 katika hoteli ya Kilimanjaro ambapo mshindi aliibuka mrembo Theresia Shayo (namba 5) kabla ya kupigwa marufuku kwa kile kilichosemekana wakati huo kukosa maadili
 Miss Tanzania wa kwanza Theresia Shayo akipita pembeni mwa bwawa la kuogelea
Huko Zanzibar nako mashindano ya ulimbwende yalifanyika kwa mara ya kwanza (na ya mwisho, kwani hayajafanyika tena hadi leo) na mshimdi alikuwa Bi Hediye Khamis Mussa (katikati) hii ilikuwa Januari 13, 1968
 Mwaka 1994 Miss Tanzania ikaibuka tena na mshindi alikuwa Aina Maeda
Miss Tanzania 1994 Aina Maeda akiwa na mshindi wa pili Lucy Ngongoseke Kihwele (shoto) na wa tatu alikuwa Dotto Abuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Totos za kilimanjaro kumbe sio siku hizi tu! Enzi hizo ndo walimbwende walikuwa wa kweli maana mafuta yao wote yalikuwa petroleum jelly! full stop. Michu watafute hawa walimbwende wa kwanza wanaweza wakatupatia historia nzuri sana ya namna ulimbwende ulivyobadilika.

    Mdau Edmonton

    ReplyDelete
  2. kipindi hicho hakuna Tv ni gazeti la uhuru na mzalendo! Hivyo picha hizi tusinge ziona ng'oo watu wengine ! Asante sana Ankal!

    ReplyDelete
  3. Eh tumetoka mbali na hii Miss Tanzania.

    Kwa wakati ule walikuwa sahihi kupiga marufuku hii, kwani wasichana walikuwa wanashindana kwa viswimsuit!

    ReplyDelete
  4. Heeeee kumbe mambo haya yalianza zamani ! Sio siri Warembo wa zamani walikuwa wapo kiasili sana kwa kweli walipendeza sana na wana mvuto sio mambo ya kubandika nywele za bandia

    ReplyDelete
  5. Du, nimemuona hayati nyanya angu kumbe naye alishiriki! Babu langu lilijua kuchagua.Vema sana.

    ReplyDelete
  6. da huyo miaka na 1960s kale kaugonjwa hakakuwepo - Da!

    ReplyDelete
  7. Hiyo picha ya chini mshindi wa pili alijulikana katika mashindano hayo kama Tabasamu Ngongoseke, ingawa baadaye tulimfahamu kama Lucy Kihwele.

    ReplyDelete
  8. ANKAL, YOU ROCK! HIZI KUMBUKUMBU NI HAZINA ISYOOZA, KEEP UP.

    ReplyDelete
  9. Halafu hizo designs za nguo za walimbwende wa Zanzibar ndo ziko juu sasa hivi....kweli hakuna jipya chini ya jua.

    ReplyDelete
  10. Ankal
    1st Runner up alikuwa anaitwa Tabasamu Ngongoseke sio Lucy Kihwele kwanza hata sis wadau tulishangaa baadae kusikia anaitwa Lucy

    ReplyDelete
  11. Wewe anon wa 08:58:00 una maana gani unavyosema ilikuwa sawa kupigwa marufuku kwa sababu ya swim suit? usifanye kila anafuata dini yako....kwani kuna mtu anakulazimisha uangalie hata wakivaa vichupi? Muwe wastaarabu siyo kila kitu mnafanya reference ya dini, kwanza wengi wetu hatutoki kwenye hiyo dini inayokataza swim suit...hiyo ni dini yako tu. Hulazimishwi kuangalia, kuna vipindi vingi unaweza kuangalia na siyo lazima uangalie kila kitu kinachorushwa na Television.

    ReplyDelete
  12. Na wewe anonymous wa 05:45:00 kwani unajua dini yangu ni ipi? Nani amefanya reference ya dini kama si wewe?

    Haya nenda kanisani na hicho kiswimsuit tuone kama utaruhusiwa kuabudu.

    Wacha ushamba wewe.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 01, 2013

    Ohhh Wachagga sio wazuri!

    Sasa mnaona Miss wa mwaka 1967 ktk Mashindano ya mwisho na Miss wa mwaka 1994 Mashindano yalipoanza tena?

    Acheni zenu hizo Mademu wa KICHAGGA watamu !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...