Mashindano ya kwanza ya ulimbwende nchini yalifanyika mwaka 1967 katika hoteli ya Kilimanjaro ambapo mshindi aliibuka mrembo Theresia Shayo (namba 5) kabla ya kupigwa marufuku kwa kile kilichosemekana wakati huo kukosa maadili
Miss Tanzania wa kwanza Theresia Shayo akipita pembeni mwa bwawa la kuogelea
Huko Zanzibar nako mashindano ya ulimbwende yalifanyika kwa mara ya kwanza (na ya mwisho, kwani hayajafanyika tena hadi leo) na mshimdi alikuwa Bi Hediye Khamis Mussa (katikati) hii ilikuwa Januari 13, 1968
Mwaka 1994 Miss Tanzania ikaibuka tena na mshindi alikuwa Aina Maeda
Miss Tanzania 1994 Aina Maeda akiwa na mshindi wa pili Lucy Ngongoseke Kihwele (shoto) na wa tatu alikuwa Dotto Abuu.
Totos za kilimanjaro kumbe sio siku hizi tu! Enzi hizo ndo walimbwende walikuwa wa kweli maana mafuta yao wote yalikuwa petroleum jelly! full stop. Michu watafute hawa walimbwende wa kwanza wanaweza wakatupatia historia nzuri sana ya namna ulimbwende ulivyobadilika.
ReplyDeleteMdau Edmonton
kipindi hicho hakuna Tv ni gazeti la uhuru na mzalendo! Hivyo picha hizi tusinge ziona ng'oo watu wengine ! Asante sana Ankal!
ReplyDeleteEh tumetoka mbali na hii Miss Tanzania.
ReplyDeleteKwa wakati ule walikuwa sahihi kupiga marufuku hii, kwani wasichana walikuwa wanashindana kwa viswimsuit!
Heeeee kumbe mambo haya yalianza zamani ! Sio siri Warembo wa zamani walikuwa wapo kiasili sana kwa kweli walipendeza sana na wana mvuto sio mambo ya kubandika nywele za bandia
ReplyDeleteDu, nimemuona hayati nyanya angu kumbe naye alishiriki! Babu langu lilijua kuchagua.Vema sana.
ReplyDeleteda huyo miaka na 1960s kale kaugonjwa hakakuwepo - Da!
ReplyDeleteHiyo picha ya chini mshindi wa pili alijulikana katika mashindano hayo kama Tabasamu Ngongoseke, ingawa baadaye tulimfahamu kama Lucy Kihwele.
ReplyDeleteANKAL, YOU ROCK! HIZI KUMBUKUMBU NI HAZINA ISYOOZA, KEEP UP.
ReplyDeleteHalafu hizo designs za nguo za walimbwende wa Zanzibar ndo ziko juu sasa hivi....kweli hakuna jipya chini ya jua.
ReplyDeleteAnkal
ReplyDelete1st Runner up alikuwa anaitwa Tabasamu Ngongoseke sio Lucy Kihwele kwanza hata sis wadau tulishangaa baadae kusikia anaitwa Lucy
Wewe anon wa 08:58:00 una maana gani unavyosema ilikuwa sawa kupigwa marufuku kwa sababu ya swim suit? usifanye kila anafuata dini yako....kwani kuna mtu anakulazimisha uangalie hata wakivaa vichupi? Muwe wastaarabu siyo kila kitu mnafanya reference ya dini, kwanza wengi wetu hatutoki kwenye hiyo dini inayokataza swim suit...hiyo ni dini yako tu. Hulazimishwi kuangalia, kuna vipindi vingi unaweza kuangalia na siyo lazima uangalie kila kitu kinachorushwa na Television.
ReplyDeleteNa wewe anonymous wa 05:45:00 kwani unajua dini yangu ni ipi? Nani amefanya reference ya dini kama si wewe?
ReplyDeleteHaya nenda kanisani na hicho kiswimsuit tuone kama utaruhusiwa kuabudu.
Wacha ushamba wewe.
Ohhh Wachagga sio wazuri!
ReplyDeleteSasa mnaona Miss wa mwaka 1967 ktk Mashindano ya mwisho na Miss wa mwaka 1994 Mashindano yalipoanza tena?
Acheni zenu hizo Mademu wa KICHAGGA watamu !