Wanafunzi
wa skuli ya Laureate International wakiwa nje ya Sobber house ya wanawake Kwa
Mchina, walikokwenda kwa ajili ya kujifunza namna na kujikinga na matumizi ya
dawa za kulevya.
Wanafunzi wa skuli ya Laureate International
wakiwa ndani ya Sobber house ya wanawake
Kwa Mchina, walikokwenda kwa ajili ya kujifunza namna na kujikinga na matumizi
ya dawa za kulevya.
======== ======== ========
Wanafunzi na walimu wa
skuli ya Laurete International, wamefanya ziara ya kimasomo katika nyumba za
kurekebisha tabia kwa vijana walioamua kuachana na dawa za kulevya “sober houses”,
na kusema kuwa ziara hiyo imewapa uwezo mkubwa wa kuelewa athari zitokanazo na
matumizi ya dawa za kulevya.
Mkuu wa kitengo cha
Sekondari katika skuli hiyo, Mwalimu Moh’d Saleh alisema wamefurahishwa kwa namna
wanafunzi wao walivyopokewa na kupatiwa mashirikiano, jambo lililopelekea
kuweza kujifunza kwa mafanikio makubwa.
Kufuatia ziara hiyo Mwalimu
Mohd ameahidi kuwa walimu na wanafunzi wa skuli hiyo watakuwa mabalozi wazuri
wa kuipeleka elimu hiyo katika jamii iliyowazunguka, ili iwe hatua muhimu ya kampeni ya kuwakinga
vijana na utumiaji wa dawa za kulevya.
Wanafunzi na walimu
hao walipata fursa ya kufanya majadiliano na vijana walioamua kuachana na dawa
za kulevya katika nyumba ya vijana hao iliyoko Bububu pamoja na nyumba
wanayoishi vijana wa kike iliyoko Kwa Mchina.
Wametoa wito kwa
skuli nyengine kutembelea nyumba hizo ili kujifunza kwa vitendo juu ya sababu
zilizopelekea vijana hao kujiingiza katika vitendo hivyo, ili waweze kusaidia
mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Hivi karibuni Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alizindua kampeni ya
mapambano dhidi ya dawa za kulevya maskulini, na kusema kuwa hatua hiyo
itasaidia kuwapa vijana wengi elimu inayohusiana na dawa za kulevya, na kufikia
azma ya serikali na kutokuwepo kabisa kwa matumizi ya dawa za kulevya Zanzibar.
Hassan
Hamad, OMKR
Kwa hiyo hapa ni wapi?? Mbona gabari inaandikwa nusunusu??
ReplyDelete