Ubao  wa matangazo  ukionyesha namna  ambavyo kila Nchi ilivyopiga  Kura yake   Azimio  Kuhusu hali ya  Syria,  upigaji kura huo ulifanyika wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipokutana siku ya Jumatano. Azimio hilo lilipitishwa kwa kura za ndiyo 107,  za hapana 12 na 59 za kutofungamana na upande wowote.  Madhumuni ya  Azimio hilo ni kuchagiza usitishaji wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchi humo. Ingawa Azimio hilo limepita lakini limelalamikiwa  kwamba mchakato wake haukuwa wazi, shirikishi,  halikuzingatia ushauri wa wajumbe wengine na  lilikuwa limeegema upande mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...