Mbinu hii imefanikiwa kuthibiti wizi wa mfuniko wa barabarani kwa asilimia mia moja sasa kwani yapata mwezi sasa mfuniko huu uliopo mtaa wa Jamhuri jijini Dar es salaam una mwezi na ushee hivi haujachapwa.
Pongezi kwa waliobuni mbinu hii ambayo pia inatumika kama kip-lefti kwenye barabara hiyo nyembamba
Hahahaaa hapo pana tundu kubwa ambalo ni hatari kwa watumiaji wa barabara. Lengo si kudhibiti wizi wa chuma chakavu. Anyways imesaidia kunusuru hicho kipande kilichobaki.
ReplyDeleteHello ndugu zangu sio tuu NCHI yetu Tanzania hata huku niishio London mifuniko inaibiwa nakuuzwa kama chuma chakavu mbuni yanayo tumia ni kuweka mifuniko migumu ya plastic .. nchi yetu wamebuni mbuni hii ambayo nihatari zaidi ...
ReplyDeletekwa nini wasiweke mfuniko husikuwa wa chuma kuna mengine unaweza kutengeneza kwa zenge iliyochangwa na chuma..
ReplyDeleteUbunifu hapo ni SIFURI!
ReplyDeleteAngalau wangechomea na WELDING kwa mbali kiasi kwamba ili kufanya wezi washindwe kuchukua.
Ni aibu kubwa saaana kwa sisi Wa-TZ kuwa wavivu wa kufikiri kufikia kiasi hiki.
ReplyDeleteHapo Ofisa amekaa Ofisini, ametafakari amevuta sigara labda akanywa na Pombe kidogo, ananyanyuka anapata jibu na akili hiyo, anawatuma Mgambo na matairi na matofali waende kuziba!
Kama kutafuta mbinu za kufanya wizi wa Mifuniko ya vyuma barabarani usifanyike inatutoa kamasi, je tutaweza kutafuta mbinu za kukabiliana na changamoto mbalimbali NGUMU na TETE zaidi za Kimaisha?