Mhe Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe
Pandu Ameir Kificho (mwenye shati jeupe) akiwa na Balozi wa Tanzania Jumuiya ya
Ulaya Balozi Dr. Diodorus Kamala (mwenye tai) wakiwa katika picha ya pamoja na
ujumbe uliofuatana na Mhe Spika na Uongozi wa kampuni ya Damen ya Uholanzi. Mhe
Spika na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wako kwenye ziara siku nne nchini
Uholanzi.
Mhe. Pandu Ameir Kificho Spika wa Baraza la Wawakilishi akiwa
na Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Kamala (mwenye tai) wakiwa
ndani ya Boat iendayo kasi iliyotengezwa na kampuni ya Damen. Kushoto kwa Mhe
Spika ni Mhe Omar Yusuph Mzee waziri wa Fedha Zanzibar. Na kulia kwa Dr. Kamala
ni Mhe. Mohamed Abdala Mohamed Mkurugenzi wa Nishati Zanzibar. Ujumbe wa
Zanzibar unaendelea na ziara ya kikazi nchini Uholanzi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...