Afisa Habari Daraja II wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Edward Denis Nkomola amevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake Changanyikeni Dar es Salaam na kujeruhiwa vibaya mwilini.

Edward Nkomola ni bwana harusi mtarajiwa na maandalizi ya harusi yake yapo katika hatua za mwisho ambao ndoa yake ilitarajiwa kufungwa Juni 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na Afisa Habari mwenzake wa Wizara hiyo Ndugu Nicodemus Thom Mushi, tukio hilo lilimkuta Nkomola majira ya aa saba usiku, ambapo majambazi wanane wakiwa na silaha mbalimbali, walivamia nyumbani kwake na wakitaka wapewe fedha alizokusanya kwa ajili ya harusi yake.

Taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya majambazi hao kufanikisha adhma yao hiyo walivunja mlango wa chuma (grill) na mlango wa kawaida na kuanza kumshambulia kwa mapanga na kumjeruhi mara kadhaa kichwani, kumvunja mkono, kumjeruhi kwa panga pajani na kumwibia samani za ndani, fedha, simu na vifaa mbali mbali vya harusi.

Wiki iliyopita alitoka Wilayani Same kwenye Send Off ya mke wake mtarajiwa Elizabeth.

Nkomola amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kitengo cha Mifupa MOI akipatiwa matibabu na hali yake inaendelea kusimamiwa na madaktari kwa ukaribu zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2013

    Pole dogo, kikulacho kinguoni mwako.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2013

    oho, pole sana, nadhani aliyeuza CD ni ndugu yako wa karibu, maana anayekuua ni yule anayekujua, pole sana. Bwana akuponye.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2013

    nyie majambazi ebu kuweni na aibu nini kutaka kuharibu siku ya watu? mlaaniwe nyie si mngebeba hela msepe? sasa nini kumuachia majeraha aanze kujiuguza huku mmebeba hela yote? malipo ni hapahapa machozi ya bi harusi mtarajiwa hayatamwajika bure.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2013

    Pole sana. Sasa maisha yetu ni kumwachia Mungu tu. Hakuna tena amani TZ.Mauaji ,majambazi kila kukicha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2013

    Wapi na wapi bwana harusi kupewa michango? mara nyingi inafanyika hivyo na ni makosa makubwa.

    Pole Bwana harusi mtarajiwa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2013

    Pole sana Opel, Mungu akuponye haraka na kukusimamia katika kila jambo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2013

    Usikute ni mhasimu wako ktk kumchukua Elizabeth! Binti wa leo nao wana leta Shaka ktk kuchanyingi Vingunguti na ATM.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2013

    Halafu mnatuambia eti turudi, huku tunalala milango wazi, huduma nzuri za afya, shule nzuri.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2013

    hao walikuwa na yao bwana harusi na pesa za michango wapi na wapi?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 05, 2013

    POLE SANA SHEMEJI YANGU MTARAJIWA. MIMI NASIKITIKA SANA KWAMBA BINADAMU TUMEKUWA HATUNA UTU KABISA NDOA NI JAMBO ALILOPANGA MUNGU KAMA VILE BINADAMU ANAVYOZALIWA WATU WANAFURAHIA NA KISHA AKIKUA ANATAKIWA AWE NA MKE AU MUME. WALIYOKUFANYIA HAO MAJAMBAZI BASI MUNGU AMEONA MATENDO YAO KAMA WASIPOKUJA KUKURUDISHA VITU NA PESA NA KUKUOMBA MSAMAHA LAANA YAO ITABAKIA NAO DUNIANI NA WATAJIBU SIKU YA HUKUMU. POLE SANA SHEMEJI YANGU NA POLE SANA ELIZABETH MWANANGU KWA KUTESWA MCHUMBA WAKO.
    MUNGU ATAMWINUA NA KUMPONYESHA KATIKA JINA LA YESU, AMINA

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 05, 2013

    Pole ndugu na mfanyakazi mwenzangu kwa yaliyo kukuta! Asante Bw. Mushi kwa kutuhabarisha hili. Sasa itabidi kubadili mfumo wa upokeaji michango ya harusi kwenda kidigitali zaidi kama M-PESA!

    Nakubaliana na wajumbe walioeleza kuwa kikulacho kinguoni mwako kwa misingi ya kuwa aidha jamaa yake wa karibu alichoresha au wamegombea bibi harusi na hivyo mume mwenza anakinyongo. Kama hili la pili ndivyo, huyo aliyemdhuru mwenzie aache ujinga mabinti wapo wengi kiasi cha kutokugombea atambue hiyo ni laana na atapata majibu hapahapa duniani.

    Naungana na wengine kulaani majambazi wote waliohusika na uhalifu huu. Wakose amani mioyoni mwao maisha yote mpaka watakapobadili tabia na kutubia kwa mungu kwa waliyoyafanya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...