Afisa Habari Daraja II wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Edward Denis Nkomola amevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake Changanyikeni Dar es Salaam na kujeruhiwa vibaya mwilini.
Edward Nkomola ni bwana harusi mtarajiwa na maandalizi ya harusi yake yapo katika hatua za mwisho ambao ndoa yake ilitarajiwa kufungwa Juni 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na Afisa Habari mwenzake wa Wizara hiyo Ndugu Nicodemus Thom Mushi, tukio hilo lilimkuta Nkomola majira ya aa saba usiku, ambapo majambazi wanane wakiwa na silaha mbalimbali, walivamia nyumbani kwake na wakitaka wapewe fedha alizokusanya kwa ajili ya harusi yake.
Taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya majambazi hao kufanikisha adhma yao hiyo walivunja mlango wa chuma (grill) na mlango wa kawaida na kuanza kumshambulia kwa mapanga na kumjeruhi mara kadhaa kichwani, kumvunja mkono, kumjeruhi kwa panga pajani na kumwibia samani za ndani, fedha, simu na vifaa mbali mbali vya harusi.
Wiki iliyopita alitoka Wilayani Same kwenye Send Off ya mke wake mtarajiwa Elizabeth.
Nkomola amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kitengo cha Mifupa MOI akipatiwa matibabu na hali yake inaendelea kusimamiwa na madaktari kwa ukaribu zaidi.
Pole dogo, kikulacho kinguoni mwako.
ReplyDeleteoho, pole sana, nadhani aliyeuza CD ni ndugu yako wa karibu, maana anayekuua ni yule anayekujua, pole sana. Bwana akuponye.
ReplyDeletenyie majambazi ebu kuweni na aibu nini kutaka kuharibu siku ya watu? mlaaniwe nyie si mngebeba hela msepe? sasa nini kumuachia majeraha aanze kujiuguza huku mmebeba hela yote? malipo ni hapahapa machozi ya bi harusi mtarajiwa hayatamwajika bure.
ReplyDeletePole sana. Sasa maisha yetu ni kumwachia Mungu tu. Hakuna tena amani TZ.Mauaji ,majambazi kila kukicha.
ReplyDeleteWapi na wapi bwana harusi kupewa michango? mara nyingi inafanyika hivyo na ni makosa makubwa.
ReplyDeletePole Bwana harusi mtarajiwa.
Pole sana Opel, Mungu akuponye haraka na kukusimamia katika kila jambo.
ReplyDeleteUsikute ni mhasimu wako ktk kumchukua Elizabeth! Binti wa leo nao wana leta Shaka ktk kuchanyingi Vingunguti na ATM.
ReplyDeleteHalafu mnatuambia eti turudi, huku tunalala milango wazi, huduma nzuri za afya, shule nzuri.
ReplyDeletehao walikuwa na yao bwana harusi na pesa za michango wapi na wapi?
ReplyDeletePOLE SANA SHEMEJI YANGU MTARAJIWA. MIMI NASIKITIKA SANA KWAMBA BINADAMU TUMEKUWA HATUNA UTU KABISA NDOA NI JAMBO ALILOPANGA MUNGU KAMA VILE BINADAMU ANAVYOZALIWA WATU WANAFURAHIA NA KISHA AKIKUA ANATAKIWA AWE NA MKE AU MUME. WALIYOKUFANYIA HAO MAJAMBAZI BASI MUNGU AMEONA MATENDO YAO KAMA WASIPOKUJA KUKURUDISHA VITU NA PESA NA KUKUOMBA MSAMAHA LAANA YAO ITABAKIA NAO DUNIANI NA WATAJIBU SIKU YA HUKUMU. POLE SANA SHEMEJI YANGU NA POLE SANA ELIZABETH MWANANGU KWA KUTESWA MCHUMBA WAKO.
ReplyDeleteMUNGU ATAMWINUA NA KUMPONYESHA KATIKA JINA LA YESU, AMINA
Pole ndugu na mfanyakazi mwenzangu kwa yaliyo kukuta! Asante Bw. Mushi kwa kutuhabarisha hili. Sasa itabidi kubadili mfumo wa upokeaji michango ya harusi kwenda kidigitali zaidi kama M-PESA!
ReplyDeleteNakubaliana na wajumbe walioeleza kuwa kikulacho kinguoni mwako kwa misingi ya kuwa aidha jamaa yake wa karibu alichoresha au wamegombea bibi harusi na hivyo mume mwenza anakinyongo. Kama hili la pili ndivyo, huyo aliyemdhuru mwenzie aache ujinga mabinti wapo wengi kiasi cha kutokugombea atambue hiyo ni laana na atapata majibu hapahapa duniani.
Naungana na wengine kulaani majambazi wote waliohusika na uhalifu huu. Wakose amani mioyoni mwao maisha yote mpaka watakapobadili tabia na kutubia kwa mungu kwa waliyoyafanya.