Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) amekutana na Baraza la Vyama vya Siasa nchini chini ya Mweneyekiti wake Bwana Peter Mziray (kushoto) na kumweleza kuwa Baraza hili linao mwarobaini wa kumaliza machafuko yanayojitokeza nchini kwa sasa. Aidha wajumbe wa Baraza hilo wamemwomba Spika ili wakutane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ili waweza kutoa ushauri wao kuhusu machafuko yanayotokea Mtwara, Arusha na kwingineko nchini na jinsi ya kukabiliana nayo.
Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini chini wakishiriki mkutano huo.Picha na Prosper Minja - Bunge


.jpg)
.jpg)
.jpg)
Haya sasa Hakika tupate solution ya kuondoa vurugu kali zinazojitokeza nchini kwetu kila kukicha na watu kupoteza maisha yao pasipo sababu kabisa. Amani ya nchi yetu inayumba kwa kiasi kikubwa sana sasa hiviiii. Natumaini kikao hiki kitakuja na suluhu ya Amani nchini. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
ReplyDeleteIt is still politics!
ReplyDelete