Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP. Mohammed R. Mpinga (kulia) na Mkurungezi wa Operesheni Upturn Group Co - Mr. Muhata Denis (kushoto) wakijadiliana jambo kuhusu kifaa cha kupimia ulevi (alcohol test) wakati wa semina ya Siku mbili ya kipima ulevi (alcohol test) yaliyohusisha maafisa na askari wawakilishi wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka baadhi ya mikoa Tanzania bara. Semina hiyo ilifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaam- Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP. Mohammed R. Mpinga (katikati) akipewa taarifa fupi kuhusu semina ya siku mbili ya kifaa cha kisasa cha kupima ulevi madereva kutoka kwa Mkurungezi wa Operesheni wa kampuni ya (Upturn) - Mr. Muhata Denis (kushoto kwa Kamanda). Semina hiyo ilifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaam - Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
Picha inayoonyesha kifaa cha kipimia ulevi madereva (alchol tester) wakati wa semina ya siku mbili ya kujifunza kifaa hicho iliyofanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaa - Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka baadhi ya mikoa Tanzania bara ambao ni washiriki wa semina ya siku mbili ya kifaa cha kupimia ulevi (alcohol tester) wakifanya mazoezi ya namna ya kutumia kifaa hicho. Semina hiyo ilifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaam - Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP. Mohammed R. Mpinga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja iliyohusisha maafisa na askari wawakilishi wa semina wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka baadhi ya mikoa Tanzania bara. Semina hiyo ilifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaam - Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2013

    mbona kushea midomo tena, labda mimi nimekosea kuona...magonjwa mengi siku hizi

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2013

    Kweli sasa hapo naona madereva tutapeana TB, hivi kila mtu akiingiza domo lake hapo na kupuliza, Afya kwa wengine inakuaje??

    kwani hakuna aina zingine za kifaa kisichohusisha kulamba??

    afya za madereva sasa naziona hatarini.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2013

    wahakikishe wanakuwa na midomo ile ya mbele ya hicho kipimo ya kubadilisha kwa kila atumiapo mtu mmoja wabadilishe na kuweka kipya maana wasije badili ya kupambana na ulevi wakageuka kuwa wasambazaji wa magonjwa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2013

    Swali: Kila mtu hupumulia humo akitakiwa kufanya hivyo. Hii haina madhara kiafya (mfano maambukizi ya TB, n.k.)?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2013

    hayo mambo si ukimwi utaenea sana!! kuweka domo sehemu moja.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2013

    mmhhh!! marazi tu hapo kuambukizana

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2013

    Ila mbona walevi mnashea glass ambazo hazijaoshwa ipaswavyo kuua vijidudu vya magonjwa, hasa TB?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2013

    Acheni uoga wa bila evidence, TB is an airborne disease,inasambazwa wakati kuna TB kwenye mapafu halafu mgonjwa anakohoa au anapiga chafya,na vijidudu vya TB vinasepa hewani wewe ukivuta hiyo hewa ndo unaweza pata TB. halafu mara kwa mara inabidi uwe na mgonjwa kwenye chumba kisicho na mzungulo wa hewa mzuri kwa muda mrefu.
    Hutu to mashine twa kupima ulevi huwa wana "disposable caps" hivyo akimpima mmoja anaitupa, huku mamtoni wanampa aliyepimwa, kwa bongo bana matumizi basi mtapewa hata mia- Yuck!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2013

    they do put a fresh mrija for each person. I have seen and done it. And you are given the mrija if you pass, if you fail you are taken to a police station or health centre for blood alcohol test. But I am not sure it it is possible to be done huko bongo

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2013

    Msiwe na wasiwasi hicho kifaa kitaibiwa baada ya siku chache, wabongo noma.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2013

    Na mie naona hivyo hivyo. Hebu kamanda atujuze usafi wake. Au ashauriane na watu wa afya wamuelimishe.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2013

    Warudishe walikotoa hicho kidude nani apige denda la mlevi mwenZake?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2013

    Zaidi, mbona wavuta sigara mnashea sigara moja bila kuua vijidudu vya magonjwa, hasa TB, licha ya ukweli kuwa sigara is a lethal weapon of next to mass destructiont?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 04, 2013

    Hiyo sio point wadau. Nawahakikishieni hata akikutwa dereva mlezi kesho yake anaachiliwa tu! Lini mkaona shereia za Tz zimekuwa enforced?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2013

    polis kama kawa wam epata ulaji.ningeye apenda hiki kifaa kifanye kazi kwa watu wote na si kwa public transport.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2013

    Ulaji mwingine umeongezeka kwa hao wenzetu akina mimi afande. Hebu njoo huku tusungumse mazee kabla sijakofowadi kwa wakubwa huko.nipe changu kabisaaa tuachane.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 05, 2013


    Mhh! Maradhi matupu! vimepitwa na wakati ulaya nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...