Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP. Mohammed R. Mpinga (kulia) na Mkurungezi wa Operesheni Upturn Group Co - Mr. Muhata Denis (kushoto) wakijadiliana jambo kuhusu kifaa cha kupimia ulevi (alcohol test) wakati wa semina ya Siku mbili ya kipima ulevi (alcohol test) yaliyohusisha maafisa na askari wawakilishi wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka baadhi ya mikoa Tanzania bara. Semina hiyo ilifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaam- Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP. Mohammed R. Mpinga (katikati) akipewa taarifa fupi kuhusu semina ya siku mbili ya kifaa cha kisasa cha kupima ulevi madereva kutoka kwa Mkurungezi wa Operesheni wa kampuni ya (Upturn) - Mr. Muhata Denis (kushoto kwa Kamanda). Semina hiyo ilifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaam - Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
Picha inayoonyesha kifaa cha kipimia ulevi madereva (alchol tester) wakati wa semina ya siku mbili ya kujifunza kifaa hicho iliyofanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaa - Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka baadhi ya mikoa Tanzania bara ambao ni washiriki wa semina ya siku mbili ya kifaa cha kupimia ulevi (alcohol tester) wakifanya mazoezi ya namna ya kutumia kifaa hicho. Semina hiyo ilifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaam - Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP. Mohammed R. Mpinga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja iliyohusisha maafisa na askari wawakilishi wa semina wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka baadhi ya mikoa Tanzania bara. Semina hiyo ilifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaam - Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
mbona kushea midomo tena, labda mimi nimekosea kuona...magonjwa mengi siku hizi
ReplyDeleteKweli sasa hapo naona madereva tutapeana TB, hivi kila mtu akiingiza domo lake hapo na kupuliza, Afya kwa wengine inakuaje??
ReplyDeletekwani hakuna aina zingine za kifaa kisichohusisha kulamba??
afya za madereva sasa naziona hatarini.
wahakikishe wanakuwa na midomo ile ya mbele ya hicho kipimo ya kubadilisha kwa kila atumiapo mtu mmoja wabadilishe na kuweka kipya maana wasije badili ya kupambana na ulevi wakageuka kuwa wasambazaji wa magonjwa.
ReplyDeleteSwali: Kila mtu hupumulia humo akitakiwa kufanya hivyo. Hii haina madhara kiafya (mfano maambukizi ya TB, n.k.)?
ReplyDeletehayo mambo si ukimwi utaenea sana!! kuweka domo sehemu moja.
ReplyDeletemmhhh!! marazi tu hapo kuambukizana
ReplyDeleteIla mbona walevi mnashea glass ambazo hazijaoshwa ipaswavyo kuua vijidudu vya magonjwa, hasa TB?
ReplyDeleteAcheni uoga wa bila evidence, TB is an airborne disease,inasambazwa wakati kuna TB kwenye mapafu halafu mgonjwa anakohoa au anapiga chafya,na vijidudu vya TB vinasepa hewani wewe ukivuta hiyo hewa ndo unaweza pata TB. halafu mara kwa mara inabidi uwe na mgonjwa kwenye chumba kisicho na mzungulo wa hewa mzuri kwa muda mrefu.
ReplyDeleteHutu to mashine twa kupima ulevi huwa wana "disposable caps" hivyo akimpima mmoja anaitupa, huku mamtoni wanampa aliyepimwa, kwa bongo bana matumizi basi mtapewa hata mia- Yuck!
they do put a fresh mrija for each person. I have seen and done it. And you are given the mrija if you pass, if you fail you are taken to a police station or health centre for blood alcohol test. But I am not sure it it is possible to be done huko bongo
ReplyDeleteMsiwe na wasiwasi hicho kifaa kitaibiwa baada ya siku chache, wabongo noma.
ReplyDeleteNa mie naona hivyo hivyo. Hebu kamanda atujuze usafi wake. Au ashauriane na watu wa afya wamuelimishe.
ReplyDeleteWarudishe walikotoa hicho kidude nani apige denda la mlevi mwenZake?
ReplyDeleteZaidi, mbona wavuta sigara mnashea sigara moja bila kuua vijidudu vya magonjwa, hasa TB, licha ya ukweli kuwa sigara is a lethal weapon of next to mass destructiont?
ReplyDeleteHiyo sio point wadau. Nawahakikishieni hata akikutwa dereva mlezi kesho yake anaachiliwa tu! Lini mkaona shereia za Tz zimekuwa enforced?
ReplyDeletepolis kama kawa wam epata ulaji.ningeye apenda hiki kifaa kifanye kazi kwa watu wote na si kwa public transport.
ReplyDeleteUlaji mwingine umeongezeka kwa hao wenzetu akina mimi afande. Hebu njoo huku tusungumse mazee kabla sijakofowadi kwa wakubwa huko.nipe changu kabisaaa tuachane.
ReplyDelete
ReplyDeleteMhh! Maradhi matupu! vimepitwa na wakati ulaya nini?