Mmoja wa waasisi wa Tanzania African National Union (TANU) na Chama cha Mapinduzi (CCM), Bi Halima Selengia maarufu kama 'Shangazi'  (pichani) amefariki dunia  leo mchana Moshi mjini nyumbani kwake Mtaa wa Liwali.Amefariki akiwa usingizini. Marehemu ambaye alikuwa na miaka 94 ameacha watoto wawili, wajukuu na vijukuu.

Msiba huu uko nyumbani kwa marehemu na kwa mujibu wa Familia ya Selengia, mazishi yamepangwa kufanyika  kesho baada ya Salaat Jumaa kwenye makaburi ya waislam moshi mjini karibu na kuelekea na bohari ya BP.

Marehemu ni mmoja wa wazee waasisi wa chama cha TANU  waliopambana bega kwa bega katika harakati za Uhuru. Amekuwa kiongozi wa akina mama wa Moshi mjini kwa muda mrefu hususan kuwa Mwenyekiti katika kuendesha mgahawa maarufu pale stendi ya moshi ujulikanayo kama Shangazi Mgahawa.



Wakati wa harakati wa uhuru mwaka 1956-57 Mwalimu Julius Nyerere alifikia nyumbani kwake katika harakati za kudai uhuru..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2013

    Wow, RIP Halima. Yaani as Tanzanians we still fail to recognize women who have contributed significantly to our independence and freedom. This woman is truly among the heroes of our country. I am really grateful for all she and other women like her did for us to be where we are today. She deserves a state funeral. I used her and many other ladies to stress a point in my Masters thesis, a tribute to their positive feminism.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2013

    Shangazi hotel moshi stendi ya long tyme sikujua km jina linatokana na marehemu. RIP

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 20, 2013

    shangazi hotel niliwahi kunywa chai na mandazi enzi hizo nikiwa bado nipo Tanzania.Mungu amlaze marehemu pahali pema peponi ameni.

    ReplyDelete
  4. Mungu ailaze roho ya mwenze huyu mahara pema peponi amina

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2013

    Kweli wa kazi wa Moshi mjini tumempoteza kiongozi shujaa, shangazi jasiri RIP shangazi, watuwa wa Moshi mjini tulianza ushirika miaka mingi kutoka shangazi hotel stand ya mabasi kwa kununua shares kwenye hiyo hotel chini ya uongozi wake na gawio la faida lilikuwa linagawanywa kwa wanashare chini ya kiongozi huyu. We will miss you shangazi..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...