Mmoja wa waasisi wa Tanzania African National Union (TANU) na Chama cha Mapinduzi (CCM), Bi Halima Selengia maarufu kama 'Shangazi' (pichani) amefariki dunia leo mchana Moshi mjini nyumbani kwake Mtaa wa
Liwali.Amefariki akiwa usingizini. Marehemu ambaye alikuwa na miaka 94 ameacha watoto
wawili, wajukuu na vijukuu.
Msiba huu uko nyumbani kwa
marehemu na kwa mujibu wa Familia ya Selengia, mazishi yamepangwa kufanyika kesho baada ya Salaat Jumaa kwenye makaburi ya
waislam moshi mjini karibu na kuelekea na bohari ya BP.
Marehemu ni mmoja wa wazee waasisi wa chama cha TANU waliopambana bega kwa bega katika harakati za
Uhuru. Amekuwa kiongozi wa akina mama wa Moshi mjini kwa muda mrefu hususan
kuwa Mwenyekiti katika kuendesha mgahawa maarufu pale stendi ya moshi
ujulikanayo kama Shangazi Mgahawa.
Wakati wa harakati wa
uhuru mwaka 1956-57 Mwalimu Julius Nyerere alifikia nyumbani kwake katika
harakati za kudai uhuru..
Wow, RIP Halima. Yaani as Tanzanians we still fail to recognize women who have contributed significantly to our independence and freedom. This woman is truly among the heroes of our country. I am really grateful for all she and other women like her did for us to be where we are today. She deserves a state funeral. I used her and many other ladies to stress a point in my Masters thesis, a tribute to their positive feminism.
ReplyDeleteShangazi hotel moshi stendi ya long tyme sikujua km jina linatokana na marehemu. RIP
ReplyDeleteshangazi hotel niliwahi kunywa chai na mandazi enzi hizo nikiwa bado nipo Tanzania.Mungu amlaze marehemu pahali pema peponi ameni.
ReplyDeleteMungu ailaze roho ya mwenze huyu mahara pema peponi amina
ReplyDeleteKweli wa kazi wa Moshi mjini tumempoteza kiongozi shujaa, shangazi jasiri RIP shangazi, watuwa wa Moshi mjini tulianza ushirika miaka mingi kutoka shangazi hotel stand ya mabasi kwa kununua shares kwenye hiyo hotel chini ya uongozi wake na gawio la faida lilikuwa linagawanywa kwa wanashare chini ya kiongozi huyu. We will miss you shangazi..
ReplyDelete