Na Ripota Wetu,Arusha
Jeshi la Polisi nchini linawasaka Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Mkuu wa kambi ya upinzani bungeni,Mh. Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Mh. Godbless Lema kwa kosa la kuendesha mkutano wa hadhara bila kibali .
Aidha Jeshi hilo linawashikilia watu 67 wakiwemo wabunge wanne wa Chadema kwa kosa la kufanya mkusanyiko usiokuwa na kibali katika uwanja cha Soweto jijini hapa.
Akiongea na waandishi wa habari,Kamishna wa Polisi, Paul Chagonja Alisema kuwa wanawasaka wabunge hao baada ya kukimbia kusiko julikana mapema jana mara baada ya kufanya mkutano pasipo kuwa na kibali cha mmiliki wa kiwanja (AICC) pamoja na Jeshi la Polisi .
Aliwataja wabunge ambao wamekamatwa na jeshi hilo kuwa ni pamoja na mbunge wa singida,mh. Tundu Lissu ,Mbunge viti maalumu Joyce Nkya,mbunge wa Mbulu Mustafa Akunay pamoja na Saidi Arifu ambapo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mapema kesho mara baada ya kupata Dhamana wakiwa katika kituo kikuu cha polisi mkoa.
Sanjari na hilo pia kamishna huyo alisema kuwa jeshi hilo linawataka viongozi hao wawili wa Chadema kuja kutoa ushahidi wa mlipuko wa bomu uliotokea Jun 15 katika kiwanja cha Soweto wakati mkutano wa chadema wa kufunga kampeni ulipokuwa unafanyika kwani viongozi hao walidai kuwa wanao ushaidi wa kutosha wa picha na video zinazoonyesha muhusika wa kitendo hicho cha ulipuaji .
“kama kweli Mbowe na Lema wanamapenzi mema na wakazi wa Arusha na uchungu wa damu ya wananchi iliyomwagika wajitokeze kulisaidia jeshi la polisi kutoa ushahidi huo ,ili muhusika aweze kufikishwa kwenye vyombo vya dola, kwani polisi sio wauaji bali wasimamia ulinzi na haki ya wananchi wake na kama basi wataona hawataki kutoa ushaidi kwetu na wanatuhisi vibaya kama wanavyo sema basi wapeleke ushaidi huo kwa Rais wa nchi maana yeye ndie Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchi”alisema Chagonja.
Aliongeza kuwa kama wataona pia huko hapafai kupeleka basi watafute shehe au padre wapeleke ushahidi huo na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu huyo ambaye amehusika.
Aidha alibainisha kuwa endepo hawata fanya hivyo sheria itafata mkondo wake kama inavyosema kuwa iwapo mtu anaushaidi wa kosa la jinai na anakaa nao pasipo kuutoa kwa vyombo vya dola basi mtu Yule nae atachukuliwa hatua za kisheria ya yeye pia kufunguliwa mashtaka ya kosa la jinai.
Pia aliwataka wakazi wa mkoa wa Arusha kuendela na shughuli zao huku wakijiepusha na makundi ya kisiasa pamoja na mikusanyiko isiyokuwa na kibali kwani kufanya hivyo ni kuendeleza machafuko huku wahusika wakiwa wanatafuta mkono wao kwenda kinywani .
Aidha aliwataka waandishi wa habari kuwa wazalendo kwa nchi yao na kutumia kalamu pamoja na kamera zao kulinda na kutunza amani ya nchi ikiwemo kuheshimimu sheria kwa kuandika habari za kweli zenye kulinda amani kuliko kuleta machafuko.
Cha ajabu kwanini iwe arusha tu.Mbowe na chama chake wanatafuta uhuru,wakati uhuru wa Tanzania ulipatikana mwaka 1961 bila kumwaga damu.yani ukiwafatilia sana viongozi wa chadema utaona mwenyekiti wao unashindwa kuelewa ni hasa ni nini?anahitaji?Wakazi wa arusha ni wajibu wao kujiuliza kwa nini arusha ndiyo mbowe anahasisha fuju isiwe kilimanjaro?kila kitu anajua yeye du kazi kweli?
ReplyDeleteKwani hawajulikani walipo? Vyombo vya dola mpaka sasa vimeshindwa kuwakamata, SERIOUSLY?!!!
ReplyDelete1.Arusha ndugu zetu mnakwenda wapi?
ReplyDelete2.Kwa nini mumruhusu huyo Mwenyekiti wa Chama cha Siasa kuitumia Arusha vibaya?
3.Kwa nini msijiulize huyo Mwenyekiti wa Chama cha Siasa asiendeshe Siasa zake za kiusanii Dar aje kufanyia kwenu Arusha?
4.Kweli mnakubali Uchumi wenu usimame na muishi kwa shida kwa ajili ya Siasa za vurugu?
5.Arusha jiuliz,hivi Arusha ya leo ni ileile ya mapato ya DOLLA ZA KIMAREKANI kwa Madini na Utalii?
...SIO BURE PANA JAMBO...!
Ni ajabu kuona MAKAO MAKUU YA SIASA ZA TANZANIA YAKIWA JIJINI ARUSHA WAKATI BUNGE LA TANZANIA LINA MAKAZI YAKE DODOMA!