Picha na Habari na John Nditi.
WAKAAZI zaidi ya 1,000 wameuziwa mashamba na viwanja katika eneo la msitu wa hifadhi Mkundi ambao kwa asilimia kubwa upo katika wilaya ya Mvomero wametakiwa kuondoka kwa hiari yao baada ya kuvuna mazao yao na si vinginevyo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera akiwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wilaya ya Mvomero, pamoja na wataalamu wa Maliasili , Wakala wa Misitu Tanzania walifanya mkutano maalumu na wananachi hao ndani ya hifadhi hiyo na baada ya kusikiliza hoja zao alifikia uamuzi wa kuwataka watii sheria ya hifadhi ya misitu iliyotungwa na bunge .
Hata hivyo alisema, Serikali ya Mkoa itawachukulia hatua kali za kinidhamu kwa watendaji wa serikali za Vijiji, Kata na wengine ngazi ya wilaya ambao watabainika wamejihusisha kutoa vibali batiri ka kuwagawia mashamba na viwanja wananchi hao na kujipatia mamia ya fedha.
Msitu huo wa hifadhi wa Mkundi ulo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii na kusimamiwa na wakala wa hifadhi ya misitu Tanzania na ulianzishwa na Serikali kuu mwaka 1953 ukiwa na ukubwa za hekta 9, 298. 91.
Hata hivyo msitu huo wa hifadhi ulianza kuvamiwa na watu tangu mwaka 2008, ambapo walijitokeza wajanja wakishirikiana na viongozi wachache wasiowaminifu wa Serikali ya Kijiji cha Wami Sokoine ambacho kipo katika Kata ya Dakawa, kuwauzia wananchi wakidai eneo hilo si la hifadhi tena.

Wajanja hao wachache walidiriki hata kutumia njia ya udanganyifu kuomba eneo la Malamo kuwa ni kitongoji cha Kijiji cha Wami Sokoine na baadaye kufanikiwa kufungua shina la CCM na kutokana na idadi ya wanachama kuwa wengi liligeuzwa kuwa ni Tawi.
Hatua hiyo iliharalisha baaadhi ya wananchi kuamini kuwa eneo hilo limegeuzwa kuwa la makazi na mashamba ya kilimo na kusababisha wengi kujitokeza kununua mashamba ekari tano kila mmoja wao.
Hatua hiyo iliharalisha baaadhi ya wananchi kuamini kuwa eneo hilo limegeuzwa kuwa la makazi na mashamba ya kilimo na kusababisha wengi kujitokeza kununua mashamba ekari tano kila mmoja wao.
Mkuu wa Mkoa , Joel Bendera , kabla ya kutoa maamuzi alilazimika kwanza kutoa elimu kwa wananchi hayo watambue ain ya ardhi zilizopo hapa nchini.
Wakimsikiliza kwa makini, Mkuu wa Mkoa huo alisema ardhi imegwanyika makundi matatu, ardhi ya Kijiji ambayo ni kubwa zaidi, ardhi ya hifadhi iliyotengwa kwa madhumuni maalumu ya hifadhi ya misitu na wanyama na nyingine ni ardhi ya Umma.
Hivyo aliwaambia kuwa watambue kuwa wao wamevamia ardhi namba mbili ambayo ni ya Hifadhi ya taifa ambazo imepitishwa na Bunge na kuwataka waheshimu sheria kwa kuondoka kwa hiari kabla ya kutumia nguvu.
Hivyo alisema ,aneo walilojitwalia ni la Hifadhi ya Taifa ya Misitu na inatambuliwa kusheria baada ya kutangazwa kwenye gazeti la Serikali , ni jambo la busara likaamuliwa kwa hekima na uwazi.
“ Nilipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro niliapishwa nikiwa nimeshika biblia , wengi wanaapa kwa kushika Msahafu ...niliapa kuilinda Katiba , kusimamia Sheria na Kanuni zake zilizowekwa...na sasa siwezi kwenda kinyume na sheria iliyopitisha na bunge ya kuutambua msitu huu wa hifadhi” alisema Mkuu wa Mkoa.
Hivyo aliwataka kwanza kutambua wote wanaoendesha shughuli za kilimo, kujenga makazi wamevunja sheria na wanapaswa kundoka kwa hiari yao badala ya kutumia nguvu .
Hata hivyo alisema , hoja zao walizotoa ni za msingi hasa juu ya ongezeko la watu na uhaba wa maeneo ya kilimo na makazi ambapo aliwataka kwanza watii sheria bila shuruti ya kuondona na baadaye waunde timu ndogo ya wajumbe kuungana na serikali ya Kijiji, Kata na Wilaya kuweza kujenga hoja ya msingi itakayowasilishwa kwa Rais ya kuomba sehemu ya ardhi umengwe kutoka kwenye hifadhi ambayo haitaleta nmadhara ya lengo lilolokusudiwa.

Awali, Kiongozi wa wakulima hao , Michael Nanchalanga, alisema wao hawakuvamia eneo hilo bali walifuata taratibu zote katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji, Kata na Wilaya ya Mvomero na kuruhusiwa kupitia vikao vya serikali za Kijiji cha Wami Sokoine ilichopo Wilayani Mvomero.
Alisema, baada ya Serikali ya Kijjiji kuridhia kwao walikubali kwa umoja wao kuanzisha kitongozi kilichopewa jina la Maramo na kufunguliwa shina la Chama cha Mapinduzi ( CCM) na baadaye kuwa tawi na kujenga Ofisi ya Chama iliyozunduliwa rasmi .
“ Tumechangia shughuli mbalimbali za ujenzi wa Shule ya Sekondari Wami Dakawa na michango mingine...sisi si wavamizi , tumepewa eneo hilo na kila mmoja amepatiwa ekari tano ya ardhi “ alisema Kiongozi huyo.
Alibainisha kuwa hawana ubishi wa kuondoka , isipokuwa waliuomba uongozi wa Serikali ya Mkoa iwasilishe ombi lao kwa Rais Jakaya Kikwete aliye msikivu atambue kuwa kutokana na ongezeko la watu na ukosefu wa ardhi wapatiwe sehemu waendeleze shughuli za uzalishaji mali .
Kutokana na mapendekeo hayo ya Mkuu wa Mkoa, wananchi hao waliridhia ushauri hiyo na kuahidi kuwa baada ya kuvuna mazao hayo wanaondoka wakisubiri mchangato huyo uwezekutekelezwa na kupatiwa majawabu mengine.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera na ujumbe wake wakiangalia baadhi ya ya maeneo ya hifadhi ya msitu wa Kuni Morogoro yakiwa yamejengwa makazi ya kudumu.
Baadhi ya Wakuu wa Idara za Sekretarierti ya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza maelezo ya wananch
Baadhi ya wananchi wambao wanaendesha kilimo na ujenzi eneo la Hifadhi ya Msitu wa Mkundi Morogoro, wakimsikiliza RC Joel Bendera , hayupo pichani
Katibu wa Kitongoji cha malamo akitoa maelezo ya hali halisi
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, ( wakwanza kushoto) akisalimiana na mmoja wa viongozi wa Tawi la CCM Malamo, akifuatiwa ya DC Anthony Mtaka wa Mvomero
Jiwe la tahadhari kwa wananchi kuhusiana na msitu wa hifadhi Mkundi, Morogoro
Haya matatizo mengine serikali yetu huwa inajitakia; Hivi kweli watu wauziwe eneo la hifadhi ya Taifa na hata wakajenga makazi ya kudumu bila wao (serikali) kujua? Inatia shaka kubwa kuhusu umakini wa serikali yetu mkoani!!
ReplyDeleteChonde chonde Ndugu michuzi jaribuni ku balance vichwa vya habari. hivi kweli hawa unawapa kichwa cha habari kuwa ni wajanja??? je huu ni ujanja?? ujumbe gani unatuma kwa jamii tunayosoma??? bila shaka hawa ni Matapeli na wala si wajanja. please help on that!
ReplyDeleteKibao kinachoonyesha umiliki wa msitu ndio kwanza kipyaaaa!
ReplyDeleteDECI no. 2 ndio hii!!!
ReplyDeleteAhhh Tanzania Shamba la bibi!
ReplyDeleteKila kukicha mara,
1.Jakaya Foundation,
2.DECI
3.Bijampora
4.Mizambwa Enterprises Ltd.
5.UPATU
Na safari hii wameona wawashukie Wakulima Vijinini!