Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi.
Serikali wilayani Handeni mkoani Tanga, imewataka Wafanyabiasha wilayani humo, kuhakikisha kuwa wananunua na kutumia mashine za TRA za kielektroniki (EFD) katika kutoa risiti wakati wanapouza bidhaa zao kwani kutotoa stakabadhi ni kosa la jinai.
Agizo
hilo limetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw.
Muhingo Rweyemamu, wakati alipokuwa akifanya uzinduzi wa matuminzi
sahihi ya mashine hizo za kielektroniki (EFD) wilayani humo na kusema
kuwa itakapobainika kwa mfanyabiashara anauza bidhaa bila ya kutoa
stakabadhi atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Bw. Rweyemamu amesema kuwa mashine hizo ambazo pia zinahifadhi kumbukumbu za mauzo kwa wafanyabiashara, na hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani zimetengenezwa kwa ubora unaostahili na makampuni yanayoaminika kimataifa.
Bw. Rweyemamu amesema kuwa mashine hizo ambazo pia zinahifadhi kumbukumbu za mauzo kwa wafanyabiashara, na hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani zimetengenezwa kwa ubora unaostahili na makampuni yanayoaminika kimataifa.
Amesema
kuwa mbali ya kuwa kwa kutumia mashine hiyo Serikali haitakosa mapato
yatokanayo na mauzo ya bidhaa za madukani, lakini pia itakuwa ni faida
kwa watumiaji kwa vile inahifadhi kumbukumbu za mauzo yao.
Awali
Meneja wa TRA wilayani Handeni Bw. Charles Kamuhanda, alimwambia Mkuu
huyo wa wilaya kuwa, wafanyabiashara wwengi hawataki kutoa risti
wanapouza bidhaa
katika maduka yao kwa lengo la kukwepa ushuru.
Hivyo
amewataka kujenga tabia ya kutoa risiti kwa kila mmteja atakayenunua
bidhaa katika duka husika na kwa kutokufanya hivyo ni sawa na kukwepa
ushuru wa Serikali.
Bw. Kamuhanda alisema kuwa mnunuzi yeyote anatakiwa kudai na kupewa risiti kama sehemu ya uwajibikaji kwa taifa na kwamba ni haki kwa kila mteja kudai na kupewa risiti kwani hata wafanyabiashara wanapokwenda kufungasha wanatakiwa kudai na kupewa risiti pia.
Aidha
Bw.
Kamuhanda ameitaja faida nyingine za mashine hizo kuwa mbali ya kutunza
kumbukumbu za mauzo kwa muda wa miaka mitano, lakini pia mfanyabiashara
anaweza kudhibiti wizi endapo anamuachia muuzaji mwingine ambaye sie
mwaminifu.



Muhingo kwa Lugha ya Kizigua ni Mpingo AU MTI MGUMU!
ReplyDeleteSasa kwa kitendo cha DC kuagiza wakazi wa Handeni kutumia Mashine za TRA za EFD hapo ndio amethibitisha Mhe.Rweyememu kuwa yeye ni Muhingo!
Wazigula weyangu muuona Muhingo uwo?
ReplyDeleteWelewe nyuwe Yuno Mkulu wa Wilaya Zumbe Muhingo Rweyemamu kakola masa vidala!,
Vino chikataga Makwazu Kwesoko hano Handeni chitumie izimashine za TRA izo zei EFD?