Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi.

Serikali wilayani Handeni mkoani Tanga, imewataka Wafanyabiasha wilayani humo, kuhakikisha kuwa wananunua na kutumia mashine za TRA za kielektroniki (EFD) katika kutoa risiti wakati wanapouza bidhaa zao kwani kutotoa stakabadhi ni kosa la jinai.

Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu, wakati alipokuwa akifanya uzinduzi wa matuminzi sahihi ya mashine hizo za kielektroniki (EFD) wilayani humo na kusema kuwa itakapobainika kwa mfanyabiashara anauza bidhaa bila ya kutoa stakabadhi atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Bw. Rweyemamu amesema 
kuwa mashine hizo ambazo pia zinahifadhi kumbukumbu za mauzo kwa wafanyabiashara, na hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani zimetengenezwa kwa ubora unaostahili na makampuni yanayoaminika kimataifa.

Amesema kuwa mbali ya kuwa kwa kutumia mashine hiyo Serikali haitakosa mapato yatokanayo na mauzo ya bidhaa za madukani, lakini pia itakuwa ni faida kwa watumiaji kwa vile inahifadhi kumbukumbu za mauzo yao.

Awali Meneja wa TRA wilayani Handeni Bw. Charles Kamuhanda, alimwambia Mkuu huyo wa wilaya kuwa, wafanyabiashara wwengi hawataki kutoa risti wanapouza bidhaa katika maduka yao kwa lengo la kukwepa ushuru.

Hivyo amewataka kujenga tabia ya kutoa risiti kwa kila mmteja atakayenunua bidhaa katika duka husika na kwa kutokufanya hivyo ni sawa na kukwepa ushuru wa Serikali.

Bw. Kamuhanda alisema kuwa mnunuzi yeyote anatakiwa kudai na kupewa risiti kama sehemu ya uwajibikaji kwa taifa na kwamba ni haki kwa kila mteja kudai na kupewa risiti kwani hata  wafanyabiashara wanapokwenda kufungasha wanatakiwa kudai na kupewa risiti pia.

Aidha Bw. Kamuhanda ameitaja faida nyingine za mashine hizo kuwa mbali ya kutunza kumbukumbu za mauzo kwa muda wa miaka mitano, lakini pia mfanyabiashara anaweza kudhibiti wizi endapo anamuachia muuzaji mwingine ambaye sie mwaminifu.       

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2013

    Muhingo kwa Lugha ya Kizigua ni Mpingo AU MTI MGUMU!

    Sasa kwa kitendo cha DC kuagiza wakazi wa Handeni kutumia Mashine za TRA za EFD hapo ndio amethibitisha Mhe.Rweyememu kuwa yeye ni Muhingo!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2013

    Wazigula weyangu muuona Muhingo uwo?

    Welewe nyuwe Yuno Mkulu wa Wilaya Zumbe Muhingo Rweyemamu kakola masa vidala!,

    Vino chikataga Makwazu Kwesoko hano Handeni chitumie izimashine za TRA izo zei EFD?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...