Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP
Said Mwema, akimkabidhi zawadi yenye nembo ya Jeshi Polisi Tanzania, Naibu
Kamishina wa UNAMID Dkt. Syed Kaleem Imam, kutoka nchini Sudan, jimbo la
Darfur, alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es
salaam, akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku sita hapa nchini. (Picha na
Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi Dar es salaam.)
Naibu Kamishina wa UNAMID Dkt. Syed
Kaleem Imam, kutoka nchini Sudan, jimbo la Darfur (wapili kutoka kulia), akitoa
mada katika kikao cha kubadilishana uzoefu kilichowashirikisha makamishina na
maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi Nchini. Kutoka kulia ni Kamishina wa
utawala na fedha wa jeshi la polisi, CP Clodwig Mtweve, Kamishina wa Operesheni
na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Paul Chagonja, Mkuu wa tathmini na
ufuatiliaji Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) Omar Rashid pamoja na Mkuu wa
Utawala na rasilimali wa jeshi la Polisi (DCP)Thobias Andengenye.( Picha na
Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi Dar es salaam.)
hizi tashwira za ufunguzi au makabidhiano ya majengo, matawi ni vizuri zikatuonyesha na majengo husika sio taswira za handshakes tu.
ReplyDeleteUsalama kwa Walinzi wa Amani Darfur?
ReplyDeleteHuku Majeshi yetu yanateketea kule?
Kamishina wa Polisi Darfur?
ReplyDeleteJe Majeshi yetu yamekufa vipi huko?