Mahmoud Ahmad Arusha.
 
Magavana kutoka nchi za Afrika Mashariki na nchi majirani zao wamekutana jijini hapa katika mkutano wao wa 13 pamoja na mengine kujadili mtangamano wa kuwa na sarafu moja ya bara la Afrika kwa kuanzia na kuwa na mtangamano wa sarafu za kikanda.

Akizungumza kwenye mkutano huo Gavana wa Tanzania Beno Ndulu alisema kuwa kuna chama cha mkutano huu ujulikanao kama (CENTRAL BANK OF AFRICA SUMMIT) na kuwa mkutano huo ni wa 13 unaowakutanisha magavana na manaibu gavana kutoka kwenye wanachama wa chama hicho.

Akazitaja nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuwa  ni nchi za jumuiya ya Afrika mashariki na majirani zao nchi za congo drc,Ethiopia, Sudan, Komoro,Mauritius,na Ghana mada kuu ya mkutano huo ikiwa ni kujenga mtangamano wa sarafu ya pamoja kwa kuanzia na ukanda na baadae Afrika nzima.

Gavana Ndulu alisema kuwa baada ya mawazo ya wakuu wa nchi wanachama wa AU kupitisha maadhimio yao ya kutaka kuwa na sarafu za pamoja hivyo wao kama wadau wa sekta ya fedha wanakutana kujadili mtangamano huo.

“Tunajiangalia tutafikaje huko na je tumejiandaaje kufika huko hili ndio lengo la kukutana hapa leo kwani timu hii ndiyo inadhamana ya kutufikisha huko”alisema ndulu

Mkutano huo wa siku tatu unaowashirikisha wadau wa fedha kutoka kwenye nchi za afrika  ulinza tangia juzi na kufunguliwa leo jijini hapa na Gavana Ndulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2013

    MU-Monetary Union,

    Ni suala zuri licha ya changamoto nyingi zinazoambatana nazo.

    Ipo mifano mingi ya Umoja wa Sarafu iliyowahi kutokea Mfano ule wa Sarafu ya Afrika ya Magharibi, hadi huu wa Sarafu ya Ulaya.

    Mazingatio makubwa ni:


    (1.)Ukubwa wa Kiuchumi na Kasi ya kukua Uchumi unaotofautiana kwa nchi wanachama, kama tunavyoona GDP zipo tofauti ile ktk nchi 5 za Afrika ya Mashariki.

    -Tanzania GDP 23US$ Billion, GDP rate of growth 6.9%
    -Kenya GDP 33US$ Billion, GDP rate 4.5%
    -Uganda GDP 16US$ Billion, GDP rate 5.2%
    -Rwanda GDP 10US$Billion, GDP rate 7.1%
    -Burundi GDP 6.7US$ Billion, GDP rate 6.2%

    (2.)Tofauti ya Mfumuko wa Bei (INFLATION RATE)
    -Kenya 3.9%
    -Tanzania 7.1%
    -Rwanda 4.7%
    -Uganda 4.9%
    -Burundi 12.3%

    (3.)RASILIMALI ZA KIUCHUMI (RESOURCES BASE)
    -TANZANIA, Gold,Uranium,Diamonds,Gas,Oil,Steel and so on.
    -KENYA,Majani ya Chai, Mauwa, Kahawa, Mirungi
    -UGANDA, Oil,Kahawa,Chai
    -BURUNDI, Kahawa na Chai
    -RWANDA, Chai, Kahawa,(Coltan-Tantalite....HATI HATI INASEMEKANA MADINI HAYA YANAIBIWA KUTOKA CONGO DRC KULETWA RWANDA NA SI MALI ASILIA YA KUTOKA RWANDA)

    (4.)DIFFERENT FISCAL PILICIES AND MONETARY POLICIES, Nchi za Afrika ya Mashariki zinapishana ktk Sera zao za Kifenda na Kiajira, HAZINA MFUMO MMOJA KILA NCHI NA WA KWAKE.

    PIA INATAKIWA NCHI ZIWE NA KIWANGO SAWA CHA MFUMUKO WA BEI (INFLATION RATE ISIYOZIDI 1.5% WAKATI NCHI NYINGI ZA EAC ZILIZOJITAHIDI ZIPI KTK 3%-4% INFALTION RATE, Kenya,Rwanda na Uganda.

    (5.)KANUNI ZA SARAFU MOJA ZINAHITAJI NCHI WANACHAMA KUSHIRIKIANA KTK SUALA LA RASILIMALI MIONGONI MWA NCHI (RESOURCES BASE) MFANO HIZO MALI NO. 3 HAPO JUU...SASA JE WATANZANIA TUTAKUBALI KUSHIRIKIANA REVENUES (MAPATO) YA MALI ZETU HIZO HAPO JUU WAKATI NCHI ZINGINE WAO MALI ZAO NI MAJANI YA CHAI, MAUWA NA MIRUNGI?

    Hivyo changamoto ndio kama hizo ili kuupata Muungano wa Sarafu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...