Naibu Meneja wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group iliyokuwa ikijenga majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Bw. Zhang Chengwei akitia saini hati ya makabidhiano kabla ya kukabidhi majengo hayo kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria (hayupo pichani).
 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bibi Christina Sonyi akitia saini hati ya makabidhiano ya majengo ya Law School of Tanzania wakati wa shughuli ya makabidhiano ya majengo hayo iliyofanyika jana Julai 16,2013 jijini Dar Es Salaam. Wanaoshuhudia ni Bw. Emmanuel Mayeji kutoka Wizara ya Katiba na Sheria (wa kwanza kulia), Mh. Jaji Gerald Ndika Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (wa pili kulia), na wa kwanza kushoto ni Bw. Aloyse P. Mushi Mkurugenzi Mtendaji kutoka Co-architecture.
 Naibu Meneja wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Bw. Zhang Chengwei akimkabidhi hati ya makabidhiano ya majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bibi Christina Sonyi jana Julai 16, 2013 jijini  Dar Es Salaam, baada ya ujenzi wa majengo hayo kukamilika. Anayepiga makofi katikati ni Bw. Aloyse P. Mushi Mkurugenzi Mtendaji wa Co-Architecture.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bibi Christina Sonyi akipokea funguo za majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo kutoka kwa Naibu Meneja wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Bw. Zhang Chengwei iliyokuwa ikijenga majengo hayo. Makabidhiano hayo yamefanyika Julai 16,2013 jijini Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2013

    Mambo yote ya ujenzi wa kati na mkubwa yanafanya na kampuni za kichina. Hivi hakuna makampuni ya wazawa yanayoweza?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2013

    Am happy to see my last project before l left the company BCEG was finally handed over for occupancy.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...