Naibu Meneja wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group
iliyokuwa ikijenga majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa
Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Bw. Zhang Chengwei akitia
saini hati ya makabidhiano kabla ya kukabidhi majengo hayo kwa Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria (hayupo pichani).
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bibi Christina Sonyi
akitia saini hati ya makabidhiano ya majengo ya Law School of Tanzania
wakati wa shughuli ya makabidhiano ya majengo hayo iliyofanyika jana
Julai 16,2013 jijini Dar Es Salaam. Wanaoshuhudia ni Bw. Emmanuel Mayeji
kutoka Wizara ya Katiba na Sheria (wa kwanza kulia), Mh. Jaji Gerald
Ndika Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (wa pili
kulia), na wa kwanza kushoto ni Bw. Aloyse P. Mushi Mkurugenzi Mtendaji
kutoka Co-architecture.
Naibu Meneja wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Bw.
Zhang Chengwei akimkabidhi hati ya makabidhiano ya majengo ya Taasisi ya
Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba
na Sheria Bibi Christina Sonyi jana Julai 16, 2013 jijini Dar Es
Salaam, baada ya ujenzi wa majengo hayo kukamilika. Anayepiga makofi
katikati ni Bw. Aloyse P. Mushi Mkurugenzi Mtendaji wa Co-Architecture.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bibi Christina Sonyi
akipokea funguo za majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa
Vitendo kutoka kwa Naibu Meneja wa Kampuni ya Beijing Construction
Engineering Group Bw. Zhang Chengwei iliyokuwa ikijenga majengo hayo.
Makabidhiano hayo yamefanyika Julai 16,2013 jijini Dar Es Salaam.
Mambo yote ya ujenzi wa kati na mkubwa yanafanya na kampuni za kichina. Hivi hakuna makampuni ya wazawa yanayoweza?
ReplyDeleteAm happy to see my last project before l left the company BCEG was finally handed over for occupancy.
ReplyDelete