Afisa wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania inayoshughulika na Mradi wa Uchimbaji Madini aina ya Uranium,uliopo kwenye Kijiji Mkuju,Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma,Fredrick Kriel akitoa mada ya maswala ya Usalama Mgodini wakati wa Semina fupi kwa Baadhi ya Wanahabari waliofanikiwa kutembelea Mradi huo uliopo pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seluu na kufahamu mambo mbali mbali juu ya Madini hayo ya Uraniuam.
Afisa wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel akionyesha moja ya mambo muhimu na yanayotakiwa kuzingatiwa kwa mtu yeyote awapo Mgodini.
Meneja Mkuu wa Maswala ya Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Cornelis Van Den Berg akifafanua jambo kuhusu mradi huo wa Madini ya aina ya Uranium wakati wa semina fupi na baadhi ya Wanahabari walioweza kutembelea Mgodi huo leo,na kuweza kujionea na kufahamu mambo mbali mbali juu ya Mgodi huo.
Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Palangyo akielezea namna Kampuni yake inavyoweza kutoa kipaumbele katika kusaidia jamii inayouzunguka mradi huko.
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wahusika wa Mradi huo.Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda ambaye ameambatana na wanahabari hao,na wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Palangyo.
Wanahabari hao wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wasimamizi wa Mradi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2013

    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  2. je hao wamarekani wanalipo kodi sitahiki au mambo ya yetu yaleyale sisi shida yetu ni kodi sio kusaidia jamii inayowanguka jaman kusaidia ni iyali yao lakin kod ni maendeleo ya taifa letu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 18, 2013

    Kumbe haya madini yameshaanza kuchimbwa? Kama nchi tunafaidikaje au ndiyo hao wajanja wanajichotea na kutuacha na umasikini wetu?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 18, 2013

    Haya punde mtasema wanatuibia madini yetu. Wazungu hapo wawili tu wengine wabongo, semeni!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...