.Meneja wa benki ya FBME LTD mkoa wa Arusha Ramadhani Lesso  akikabidhi misaada mbalimbali kwa mama mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Abu-Abdulrahamani kilichopo Jr  jijini Arusha leo kwa ajili ya sikukuu ya Idd El Fitiri,misaada hiyo inadhamani ya shilingi laki saba na nusu kwa vituo viwili pamoja na cha Matonyok kilichopo Olasiti.
 Meneja wa benki ya FBME LTD mkoa wa Arusha Ramadhani Lesso  akikabidhi misaada mbalimbali kwa mama mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Matonyok kilichopo Olasiti Bi.Emmy Sitayo kwa ajili ya sikukuu ya  Idd El Fitiri,misaada hiyo ina thamani ya shilingi laki saba na nusu kwa vituo viwili pamoja na cha Abu-Abdulrahamani kilichopo Jr  jijini Arusha.
Afisa wa benki ya FBME LTD, Mnukwa Ally akiongea na watoto waishio katika mazingira magumu katika kituo cha Matonyok kilichopo Olasiti,mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali  iliyotolewa na benki hiyo kwaajili ya sikuu ya Idd El Fitiri.Picha na Pamela Mollel.

========  =======  ======
Na Pamela Mollel,Arusha

JAMII nchini imeaswa kuwajali watoto waishio katika mazingira magumu na wale walioko kwenye vituo vya kulelea watoto yatima kwa kuwapatia misaada mbalimbali ili waweze kuishi kama watoto wengine waishivyo majumbani 

Rai hiyo ilitolewa jana na Meneja wa  FBME Benki LTD mkoa wa Arusha Ramadhani Lesso wakati akikabidhi misaada mbalimbali ya vyakula kwaajili ya sikukuu ya Idd El Fitiri katika vituo viwili vya kulelea  watoto yatima cha Matonyok kilichopo Olasiti na kituo cha Abu-Abdulrahamani kilichopo Jr jijini Arusha

Alisema ni vyema jamii ikatambua uwepo wa watoto waishio katika mazingira magumu na wale walioko kwenye vituo, kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali kama wanavyopata watoto wa majumbani kwani ni haki yao ya msingi na kuondokana na tabia mbaya ya kuwanyanyapaa na kuwaona ni mzigo kwa jamii

“Tukiwajali hawa watoto hata kwa Mungu tunapata dhawabu kwani wengi wao hawajapenda kuwa katika mazingira haya,wengine wamefiwa na wazazi wao hivyo kujikuta wakiwa watoto wa mitaani”alisema Lesso

Aidha alitaja moja ya sababu iliyowafanya kutoa msaada huo ni pamoja na kuguswa kwa hali ya watoto waishio katika mazingira magumu hivyo kuamua kutoa faida kidogo waliyopata kama benki ili wawezekurudisha katika jamii

Meneja huyo alikabidhi misaada yenye dhamani ya  shilingi laki sabana na nusu katika vituo viwili ambapo kila kituo walitoa sukari,mafuta ya kupikia,mchele,sabuni za kufulia,madaftari na penseli

Mlezi katika kituo cha Matonyok kilichopo Olasiti chenye watoto(40) Bi.Emmy Sitayo  na Mlezi wa kituo cha Abu-Abdulrahamani chenye watoto(21) kilichopo Jr ,  Mama Abdulrahamani kwa nyakati tofauti walishukuru benki hiyo ya FBME kwa kuwakumbuka kipindi hichi cha sikukuu ya Idd na kuwataka makampuni na jamii kuiga mfano huo huku wakitaka  zoezi hilo liwe endelevu kwa watoto yatima na wasiojiweza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. MSAADA TUTANI.

    Mimi mdau nipo hapa saudia na leo ni Sikukuu ya Eid nakumbuka tulianza kufunga pamoja. Je ni sayansi gani inatumika tulianza pamoja ila Bongo nasikia ni kesho?

    Cha ajabu hatujapishana saa "yaani hapa kama ni saa tano" na Bongo ni muda huohuo.

    Wenye kujua naomba sayansi yake.

    EID MUBARAQ.

    ReplyDelete
  2. Nyinyi munafuata sera ya 'mwezi ni po pote' na sisi tunafuata sera ya 'mwezi ni kuonekana'.

    Kwa mujibu wa 'moonsighting.com' mwezi ule wa jana usingeweza kuonekana po pote katika bara la Afrika, Arabia wala Europe. Ni ncha ya South America tu ndiyo ungeweza kuonekana kwa urahisi. Na ndiyo maana sisi tumeendelea kufunga lakini nyinyi mumefungua.

    ReplyDelete
  3. Great Job Lesso (Hamuchaa). Mungu akuzidishie kwa kwaangalia watoto yatima.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...