Kamishina
Msaidizi wa Madini, (Leseni), John Nayopa na wajumbe alioongozana nao kutoka Ofisi ya Madini Kanda ya Kusini- Magharibi na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya wakiwa katika
picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mafunzo kwa wachimbaji wadogo
cha Katundasi wilayani Chunya, Injinia Paul Gongo (wa pili toka kushoto) mara
baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kituo hicho kwa ajili ya kupata taarifa
ya mafunzo kwa wachimbaji wadogo yanayoendeshwa na kituo hicho.
Serikali
imesema kuwa itahakikisha inaendelea kutoa fursa za mafunzo kwa wachimbaji
wadogo nchini ili wapate utaalam utakaowawezesha kufanya shughuli za uchimbaji
madini kwa tija.
Hayo
yamesemwa na Kamishina Msaidizi anayeshughulia Leseni katika Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi
John Nayopa, katika Kituo cha Mafunzo kwa Vitendo cha Matundasi wilayani Chunya
ambacho hutoa mafunzo ya uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu kwa wachimbaji
wadogo.
Mhandisi
John Nayopa aliusisitiza uongozi wa kituo hicho kuhakikisha wanajitangaza kwa
umma ili watu wenye uhitaji wa mafunzo waweze kufika kituoni hapo na kupata
huduma zao kwani lengo la Wizara ya Nishati na Madini na Serikali ni
kuhakikisha elimu kuhusu madini inawafikia wanachi wengi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...